Tanzania yapokea msaada wa shilingi bilioni 116.4 kutoka Japan

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.

Mkataba wa pili unahusu masuala ya kiufundi yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.

Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.

Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.

Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania.

Adha Balozi Yoshida amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500.
 
Likwelile inabidi aanze uzunguka kwa donors na Paris club ,WB na IMF kujaribu kushawishi donors kujazilizia kwenye bajeti ijayo maana JPM atatumia nguvu hesabu zitagoma ku balance zile ahadi zenu zile hamtaweza kwa kusubiria za Bandari pekee kama chanzo kikuu...angalia kwenye Tril 1 : 550Bil ni mishahara na posho zake,tunahitaji vyanzo vingine ili aweze kuleta maendeleo kwa kasi na ahadi alizoahidi kila mkoa na wilaya
 
SI TUMESEMA HATUTAKI KUWA TEGEMEZI AU HADI WATUNYIME NDIO TUNAKATAA?!
 
Ha ha ha ha ha ha haaaa! Mnafanya masihara Na kujitegemea Nini? Eti sitaki Kuoa! Lakini unaishi nae mwaka wa 10 huu Sasa!

Mambo ya nyama ya kitimoto Siri Ila mchuzi wake nakunywa!
 
Likwelile inabidi aanze uzunguka kwa donors na Paris club ,WB na IMF kujaribu kushawishi donors kujazilizia kwenye bajeti ijayo maana JPM atatumia nguvu hesabu zitagoma ku balance zile ahadi zenu zile hamtaweza kwa kusubiria za Bandari pekee kama chanzo kikuu...angalia kwenye Tril 1 : 550Bil ni mishahara na posho zake,tunahitaji vyanzo vingine ili aweze kuleta maendeleo kwa kasi na ahadi alizoahidi kila mkoa na wilaya

HATA ZA BANDARI NAWAHAKIKISHIE KUANZIA MWEZI UJAO ZITAPOLOMOKA. KWA NINI SABABU HIZI HAPA.

1. UCHUMI WETU ULIKUWA WA KIFISADI, WATEJA WA BIDHAA (CEMENT, MALUMALU, MAGARI MAKUBWA NK) NI WATU WALIO FANYA DEAL NA KUIBA SERIKALINI NA SASA MILIJA HIYO IMEKATWA.

2. WAFANYA BIASHARA/WAIGIZAJI NI WAKWEPA USHURU NA USHURU UNADHIBITIWA HAWAWEZI AGIZA WAKATI UHAKIKA WA SOKO KUNUNULIWA BIDHAA ZAO KWA BEI KUBWA HAUPO MAANA VYANZO VYAO VYA MAPATO VIMEDHIBITIWA. HAWAAGIZI KAMA MAPAMBO, HAWATAAGIZA KAMA ZAMANI, MAANA HAWANA WA KUMUUZIA.

MAPATO YANATARAJIWA KUPOROMOKA TOKA 1.4 BILIONI YA MWEZI HUU HADI CHINA YA YALIYOKUSANYWA WAKATI WA KIKWETE. NA NAWEZA TABILI ITAKUWA KATI YA 500-750 BILIONI TU.
 
Tuna ges itawaleta wengi pia

Hizi hadithi za gas huwa zinanichekesha sana, Wakati wa Mkapa na JK tuliimbishwa mapambio ya madini kwamba ndio mkombozi, tukaona sera na sijui mikurabita, mikukuta tukajua tumetoka kimaisha kama nchi. Baada ya muda takaanza kusikia tunapata mrahaba 3%, mikataba mingine imefungiwa mpaka mahotelini!! Leo hii unasikia gesi tunayo lakini tutaanza kufaidika kama nchi baada ya miaka 20 ijayo mpaka deni sijui mazingira ya mkataba na hekaya za namna hiyo. Vichekesho ni pale unapoona propaganda za kizee eti mataifa ya nchi yanatuonea gele kwa raslimali tulizo nazo, sasa huwa najiuliza mfano hayo madini tuliyopigwa porojo tunaambiwa mikataba ilikuwa mibovu na madini ndio hayo yanakaribia kuisha hayo mataifa yanatuonea gele kwa lipi? Leo gas tumewapa tena kiulani ni gele ipi yanatuonea wakati hata gas sasa hivi bado ni mali yao japo iko kwetu? Hapa husikii hadithi ya wanyama pori wala nini!! Ni kweli gas itawaleta wengi lakini tujue taifa letu limefaidika na nini kwa upande wa madini, na wanyama pori mpaka sasa kiasi tuamini kwamba hiyo gas itatusaidia. Vioja vingine vya mchana, wanasiasa wanachomoka kama risasi wanawaongopea wananchi kuhusu neema ya gas wakati wananchi maskini ya Mungu hawajui hata hiyo mikataba ina vifungu vipi vya kuwanufaisha.

CC: Lizaboni, Yehodaya
 
Zije kwa watu wenye heshima zao siyo kutuwekea masharti ya kutudhalilisha. Lakini mwishowe tunahitaji kujitegemea
kwa kwa si mumesema munaweza kujitegemea ccm hamna akili kabisa yakukuza uchumi wa nchi hii halafu hamna akili ya propaganda nani atakupa hela yake bila masharti munadhani za mama zenu hizo mutatoa vijaruba vya dhahabu magogo na mashamba kwa wachina na wajapani na wote mukijuwa wanawategemea wamerekani ndio wanunuzi wakubwa
 
Poa tu

Back
Top Bottom