Tanzania yapokea msaada kutoka Sweden ili kuboresha sekta ya elimu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
4b7c463fff0f3fd9b6a0ab9a753cfbe8

Serikali ya Tanzania imetiliana saini mikataba miwili ya msaada na serikali ya Sweden kwa kupatiwa fedha kiasi cha dola milioni 90 sawa na shilingi Bilioni 240.95 kutoka mfuko wa ushirikiano wa Elimu Duniani GPE.

Akizungumzia msaada huo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wizara ya fedha na mipango Dotto James ameitaja miradi hiyo kuwa ni shilingi bilioni 88.55 zitagharamia mpango wa maendeleo ya sekta ya elimu (ESDP) 2016/17 – 2021/2022 katika sekta tatu ndogo ikiwemo elimu ya msingi, elimu jumuishi, watu wazima na iliyo nje ya mfumo rasmi.

Bilioni 116.40 zitaongeza mchango wa Serikali ya Sweden katika Program ya Elimu kwa matokeo (EPforR) lengo likiwa ni kuwezesha mpango wa maendeleo ya sekta ya elimu 2016/17 – 2021/22 hususan kuwezesha ubora na usawa katika matokeo ya elimu ya msingi na sekondari.

Mkataba uliosainiwa leo unatokana na mfuko ambao unachangiwa na washirika wa maendeleo wengine wakiwemo UNICEF, UNESCO, Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Australia, Canada, Denmark, Ufaransa, Korea, Uholanzi, Norway, Hispania, Uswis, Marekani na Uingereza.
 
Tulivyoingia madarakani tuliahidi kuwa sisi hatutapokea misaada bali tutaanza kutoa misaada.

Hii habari inaweza kuwa sio sisi tuliopokea msaada ni sisi tumewapa Sweden msaada.
 
Tundu huko aliko atakuwa kanuna kinoma. Maana yeye aliwaomba watutenge!
 
Mmeanza kupokea pesa za maadui zetu? Maana siku hizi kuna siasa za majitaka, wapinzani wakiongea na hao hao wazungu wanaotoa misaada wanaambiwa wanashirikiana na maadui zetu! Lakini serikali ikipokea pesa za wazungu wanageuka sio maadui zetu!
Ma CCM hayajitambui kabisa.
 
Back
Top Bottom