#COVID19 Tanzania yapokea dozi 500,000 za Sinopharm kutoka Serikali ya China

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali imepokea Dozi 500,000 za Chanjo aina ya Sinopharm kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima amesema mwamko wa Chanjo ni mkubwa na wananchi wanaendelea kujitokeza.

Amesema, "Chanjo za Johnson & Johnson zimeisha tangu 19 Oktoba. Sasa tunaendelea kutoa Chanjo 1,065,600 za Sinopharm na kwa takwimu za hadi kufikia Oktoba 31 jumla ya Watanzania waliopata Chanjo hiyo ni 88,546".

=======

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Profesa Abel Makubi amewataka Watanzania waliopata chanjo ya Sinopharm kuhakikisha wanapata dozi mbili kama inavyoelekezwa.

Profesa Makubi ameyasema hayo leo wakati serikali ya Tanzania ikipokea msaada wa chanjo kutoka serikali ya China.

Chanjo hizo dozi 500,000 zimepokelewa leo Novemba 2, 2021 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA).

Profesa Makubi amesema,” Sinopharm ni lazima uchanje mara mbili. Hakikisha unapata dozi zote mbili ili uweze kupata kinga inayotakiwa,”

“Ikitokea umepata dozi moja na umesafiri usiwe na wasiwasi chanjo utaweza kuipata katika mkoa wowote taarifa zako zitachukuliwa.”
Kwa upande wake Waziri wa Afya Dk Dorothy Gwajima ametangaza kuwa hadi kufikia Oktoba 31 Watanzania 88,546 wamepata chanjo ya Sinopharm.

“Chanjo ya Johnson Jonhson iliisha tangu Oktoba 19, sasa tunatoa chanjo ya Sinopharm ambayo hadi jana watu 88,546 wameshapata chanjo hiyo sawa na asilimia 8.3 ya chanjo zilizoletwa,” amesema.

Dk Gwajima amesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kuchanja huku akibainisha mikoa 10 iliyofanya vizuri kwenye utoaji wa chanjo hiyo.

Mikoa hiyo ni pamoja na Ruvuma, Mbeya, Mtwara, Kagera, Dodoma, Arusha, Dar, Mwanza, Mara, Songwe na Pwani.

“Tutaanza kutoa takwimu za mikoa katika utoaji chanjo ili kutoa changamoto kwa mikoa ambayo iko chini,” amesema Dk Gwajima.

Chanzo: Mwananchi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom