Tanzania yapewa tuzo ya ushindi dhidi ya maleria

Chakunyuma

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
810
152
Imepewa tuzo hiyo kutokana na juhudi zilizotukuka zizofanikisha ushindi dhidi ya maleria. Tuzo hiyo imetolewa Addis Ababa na kupokelewa na mh rais. Source tbc1
My take
je ni kweli tumeshinda vita dhidi ya maleria kwa kugawa vyandarua huku vyanzo vya kuzaliana vikiendelea kuwepo jirani ya makazi yetu? Nadhani hatustahili hii tuzo.
 
Na sijaelewa hizo juhudi zilizotukuka ni zipi? Maana yake mtangazaji alikazia sana hili japo hakueleza hizo juhudi ni zipi nikawa najiuliza kwa nini serikali inapenda sifa zisizo za kweli?
 
Je ni kweli vifo vinavyotokana na maleria vimepungua baada ya juhudi zilizotukuka kufanyika? Na je hizo juhudi zilianza lini?
 
Huo ni upuuzi ktk nchi zinazotokomeza malaria tanzania haipo,sera yetu ni kutuliza malaria kwa vyandarua,sio kuua mazalia ya mbu
 
Ni kweli mkuu Bongolala ndio maana nikajiuliza kabla ya kutoa tuzo walikuja kujionea au walibase judgement yao kwenye ripoti walizopewa?
 
Back
Top Bottom