Tanzania yapendekeza Kiswahili kuwa lugha ya majidiliano katika shughuli za SADC

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Tanzania yapendekeza Kiswahili kutumika kama lugha rasmi itakayotumika kwa ajili ya majadiliano chini ya vikao vilivyo chini ya baraza la mawaziri na kuwa rasmi kwenye utendaji wa SADC.

Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema wakuu wa nchi za Afrika Mashariki waliridhia Februari 27, katika kikao kilichofanyika kwa mtandao, kwamba Kiswahili kitakuwa lugha ya tatu katika shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema katika shughuli za SADC Lugha za kikoloni zimetumika kwa muda mrefu ambapo wakuu wa nchi wamekubaliana lugha zianze kwa mtiririko mzuri kwa kuanza kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri hadi kufikia kuwa lugha rasmi ya kinyaraka.

Balozi Ibuge amesma hayo Machi 8, baada ya kukaa kikao cha Maafisa wakuu Watendaji wa SADC ambapo katika kikao walikuwa na lengo la kupendekeza lugha ya kiswahili kutumika kama lugha ya kinyaraka.
 
Back
Top Bottom