Tanzania yapeleka wanajeshi wake mpakani na Msumbiji

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Tanzania yapeleka wanajeshi wake mpakani na Msumbiji

Tanzania imevamiwa na Msumbiji

Haki miliki ya pichaMARCO LONGARIImage captionKikundi cha kigaidi kaskazini mwa msumbiji kimekuwa kikivamia maeneo mbalimbali na kuua watu

Tanzania imepeleka vikosi vyake kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Msumbiji baada ya kuibuka kwa mashambulizi yaliyotekelezwa na wanamgambo kutoka kaskazini mwa Msumbiji, wanamgambo ambao wamekuwapo tangu mwaka 2017.

Hatua ya kupeleka vikosi imechukuliwa kama hatua ya tahadhari baada ya kutokea machafuko katika kitongoji cha Cabo Delgado, gazeti la the Citizen limeripoti, likinukuu maafisa wa serikali.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya sera, ajira, wenye ulemavu, kazi, bunge na vijana Jenista Mhagama amesema vikosi vitapelekwa mkoa wa Mtwara ambao mpaka wan chi hiyo unapakana na mji wa Cabo Delgado.

Alisema mwezi Machi, serikali ilipeleka vikosi katika eneo la Sindano mkoani Mtwara na Chiwindi, wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma kusini mwa Tanzania.

Siku ya Alhamisi, Balozi wa Marakani anayeshughulikia masuala ya Afrika Tibor P Nagy, amesema uasi kaskazini wa Msumbiji unatia hofu.

Amesema ana matumaini Msumbiji itashughulikia hali hii kwa umakini mkubwa.

Kilichotokea Msumbiji
Watu sita wameuwawa na watu wasiojulikana

Image captionWatu sita wameuwawa kusini mwa Tanzania, katika mkoa wa Mtwara,

Mwezi wa Aprili mwaka huu, watu karibu 50 waliuawa katika eneo la Muidumbe. Vyombo vya habari zinasema Umoja wa Mataifa umerekodi matukio 28 ya mauaji katika eneo hilo tangu kuanza kwa mwaka 2020, ambapo watu 400 walipoteza maisha na takribani watu 100,000 waliyahama makazi yao.

Uasi wa wanamgambo nchini Msumbiji umeibuka na kuwa vita vya wazi katika wiki za hivi karibuni, kukiwa na ripoti za mauaji ya watu, kukatwa kichwa na kutekwa kwa miji miwili katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado.

Video iliyochukuliwa mwezi uliopita kwenye simu ya mkononi katika eneo la Muidumbe ilikuwa ushahidi mpya kuwa mzozo katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji sasa umekuwa wazi, katika hali ya kutia wasiwasi.

Video ya pili ilirekodiwa wiki chache zilizotangulia, zikionesha mwili wa mtu , asklari-akiwa amelala kwenye dimbwi la damu.Kisha kamera ikaonesha mwili mwingine, kisha mwingine akiwa kwenye gari ya polisi, kisha mwili wanne ambao uliwekwa hadharani, kisha silaha nyingi katika eneo kama la hifadhi ya silaha za polisi au jeshi.

Wanamgambo wa IS walikiri kutekeleza mfululizo wa mashambulizi ya hivi karibuni nchini Zimbabwe, ambayo 18% ni jamii ya kiislamu na imekuwa ikionekana kusukuma ajenda zao huko kama sehemu ya operesheni ya kuongeza nyayo zake katika sehemu kadhaa za Afrika.
 
Bora wakajenga ukuta mapema kabla mambo hajabadilika huko mbeleni. Hawa wapuuzi hupenda sana kutembelea nyota za raia wasio na hatia ili tu wakidhi matakwa yao ya kishetani.
 
Ndugu zangu wa kazamoyo tunduru wanafahamu hali ilivyo huko kwa sasa.

Nasikia wameshaanza kunyoa ndevu na kuvaa suruali ndefu sio pedo

Ndo raha ya kuwa na jeshi imara wanakuminya kimya kimya
 
Ndugu zangu wa kazamoyo tunduru wanafahamu hali ilivyo huko kwa sasa.

Nasikia wameshaanza kunyoa ndevu na kuvaa suruali ndefu sio pedo
Home boy!Sasa jamaa wanawaunganishia?
 
Hao jamaa "wanalishia mdogo mdogo" huko mpakani, wanaoishi maeneo ya uvuvi wanaelewa kauli hiyo.
 
Back
Top Bottom