Tanzania yapata tunzo ya UN kwa kutoa huduma bora kwa jamii!

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,221
3,166
4.JPG

03.JPG

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, Tuzo ya UN ya mshindi wa pili ya Tanzania katika kutoa huduma bora kwa Jamii (Mkurabita) , wakati Makamu alipofika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Juni 23, 2011 kufunga maadhimisho ya siku ya Utumishi ya Umoja wa Mataifa na Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kuadhimishwa Barani Afrika na kufanyika nchini Tanzania.

Mtazamo:Hivi wanatumia vigezo gani ukichukulia hali halisi ndio hii hapa chini?

wodi.jpg

DSC00161.jpg

DSC00164.jpg

DSC00165.jpg

4.JPG

03.JPG

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, Tuzo ya UN ya mshindi wa pili ya Tanzania katika kutoa huduma bora kwa Jamii (Mkurabita) , wakati Makamu alipofika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Juni 23, 2011 kufunga maadhimisho ya siku ya Utumishi ya Umoja wa Mataifa na Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kuadhimishwa Barani Afrika na kufanyika nchini Tanzania.

Mtazamo:Hivi wanatumia vigezo ukichukulia hali halisi ndio hii hapa chini?

wodi.jpg

DSC00161.jpg

DSC00164.jpg

DSC00165.jpg

Mkuu umeua!
 
4.JPG
03.JPG
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, Tuzo ya UN ya mshindi wa pili ya Tanzania katika kutoa huduma bora kwa Jamii (Mkurabita) , wakati Makamu alipofika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Juni 23, 2011 kufunga maadhimisho ya siku ya Utumishi ya Umoja wa Mataifa na Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla hiyo kuadhimishwa Barani Afrika na kufanyika nchini Tanzania.Mtazamo:Hivi wanatumia vigezo gani ukichukulia hali halisi ndio hii hapa chini?
wodi.jpg
DSC00161.jpg
DSC00164.jpg
DSC00165.jpg
umeuaa,ndio maana hawaipendi JF
 
943947_orig.jpg

Barabara ya Ukonga Mombasa jijini Dar es Saalam.Mikoani hali ndiyo mbaya zaidi.
 
Huu ni utani!!!Kweli UN ina nia nzuri na bongo? Ninaanza kuunga mkono wahifadhina wa Marekani wanaotaka UN ifutwe. Hii ni jumuiya shenzi kabisa!
 
IMG03059-20110516-1052.jpg

IMG03086-20110516-1140.jpg

Barabara ya Dar - Lindi - Mtwara, Katika sehemu ya Marendego-Somanga.
 
Tanzania ilipata tuzo kwenye mambo ya elimu mwaka jana at around the same time matokeo ya kidato cha IV yakionesha kuwa 80% wa watahiniwa walifeli! Rais Kikwete alionekana kwenye vyombo vya habari akinyanyua juu tuzo huku akijuwa fika watoto zaidi ya laki moja na nusu wako mtaani baada ya kufeli.

Sasa, miezi michache baadae Tanzania, tena inapata tuzo ya utata! maternal health ni mgogoro mtupu, upitakani wa maji safi na salama ni kitendawili, huku uhusiano wa raia na vyombo vya usalama (hususan police) ukiwa dhaifu kuliko kipindi chochote. Hiyo tuzi imepatikanaje?

Jibu ni Dr Asha Rose Migiro. Kuna mpango kabambe unaoendelea kati ya huyu mwanamama na wakubwa wa magogoni.Atajidai anatangaza mafanikio ya Tanzania lakini ukweli uko wazi (a) anarudisha fadhila na (b) 2015. Na Ban Ki-moon baada ya kupigiwa upatu na Tanzania amekuwa a man of his word - daima anawakumbuka wale wote waliofanikisha safari yake kwenye kiti cha enzi lakini je anajuwa jina la huu upatu aliojiunga nao?
 
UN kundi la wanywa damu wauaji wakubwa na wanafiki waliopitiliza..i hate this useless group called Un...huduma bora wakati kina mama wanalala wa 4 kitanda kimoja!!!
 
Jamani kumbukeni TZ inawasomi wasioelimika na ni watalaamu wa kwenye makaratasi, yaani mtu akikuandikia report hizo za marejesho kwa wafadhili utakubali lakini utekelezaji ni ziro, ndiyo hayo tunayaona ya mambo ya tuzo, kwani jamaa wanapelekwa kukagua maeneo machache (sample) na wao kutoa zawadi. Ingependeza hizi picha zikatumwa kwa Ban Ki Moon azione ili aambiwe mzee zawadi yako kwa huduma bora kwa TZ ndiyo hizi....!
 
Tanzania ilipata tuzo kwenye mambo ya elimu mwaka jana at around the same time matokeo ya kidato cha IV yakionesha kuwa 80% wa watahiniwa walifeli! Rais Kikwete alionekana kwenye vyombo vya habari akinyanyua juu tuzo huku akijuwa fika watoto zaidi ya laki moja na nusu wako mtaani baada ya kufeli.

Sasa, miezi michache baadae Tanzania, tena inapata tuzo ya utata! maternal health ni mgogoro mtupu, upitakani wa maji safi na salama ni kitendawili, huku uhusiano wa raia na vyombo vya usalama (hususan police) ukiwa dhaifu kuliko kipindi chochote. Hiyo tuzi imepatikanaje?

Jibu ni Dr Asha Rose Migiro. Kuna mpango kabambe unaoendelea kati ya huyu mwanamama na wakubwa wa magogoni.Atajidai anatangaza mafanikio ya Tanzania lakini ukweli uko wazi (a) anarudisha fadhila na (b) 2015. Na Ban Ki-moon baada ya kupigiwa upatu na Tanzania amekuwa a man of his word - daima anawakumbuka wale wote waliofanikisha safari yake kwenye kiti cha enzi lakini je anajuwa jina la huu upatu aliojiunga nao?

Mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia zote.

Ninazifananisha hizi TUZO na zileeeeee PHd za HESHIMA ... yaani za mgao tuu
 
Oh no! kama migiro anafanya hivyo basi anaua nchi! what! TZ na huduma bora wapi na wapi! mana UN wanaweza kufanya research ya ukweli na kuconclude TZ ndio ipate tuzo kweli!!!!! what the heck!!kama unavyosema lazima kuna namna hapo! ila udhalilishaji wakina mama wanalala chini wengine wanapokea tuzo, this country is full of surprises
 
Wakuu hao wanaotoa hizo tuzo sijui wameenda wapi na wapi wakaangalia huduma za jamii wanazozisema
May be wangetuambia wametembelea wapi na wapi wakaona hizo huduma safi za jamii then waje hapa watupe tuzo
Huko Manyara wanawake wajawazito wanapelekwa na machela kituo cha afya ambaco hakina umeme kinatumia kibatari na kina muuguzi mmoja anayehudumia wagonjwa kibao bado tunaziita huduma bora
Huduma bora wakati watoto huko ngorongoro wanakaa chini ya mti ambao unaitwa darasa
Huduma bora wakati asilimia kubwa ya shule za sekoondari zilizoanzishwa hazina vitabu wala madawati wala maabara na sio mbali na mjini
Hapa Arusha kuna shule iko ndani ya manispaa hapa mateves ya sekondari na watoto wanakaa chini hawana madawati na iko ndani ya eneo la jiji
Tuache unafiki jamani may be hao watu au wakaguzi walipelekwa Agakhan wakao wagonjwa walivyolala vizuri na huduma wanazopata wakajua kila hospitali tanzania ndo ilivyo au walipelekwa Shabban Robert Secondary au Mzizima Secondary wakaona kila mwanafunzi anavyokaa kwa starehe na kila huduma anapata wakajua shule zote za tanzania ndo zilivyo
 
ukiona unasifiwa na hao UN ujue ni mjinga wakupindukia ndio maana unaona viongozi wetu ni wajinga, niwapumbavu na vichaa hawanajipya ni kuchekecheka tu, nakulia lia kabla ya kuchukua uamuzi wa nini walifanyie taifa wao na safari tu uzadhani walishaolewa na USA au nchi za magharibi sijui nilini tutapata viongozi wenye akili timamu maana nina mashaka na akili ya viongozi wetu pengine inabidi tuwe tunawapima akili ndio wanangombea maana sikutegemea kuona nchi yenye rasrimali nyingi na za kila aina baado ni maskini tena umaskini unaongezeaka kila kukicha.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom