Tanzania yapata ofa ya kuuza mikoa mitatu.tanga, kilimanjaro na arusha

Kuhusu kigamboni nibora tukawa na ushahidi dhahiri badala ya kuendeleza porojo zinazopigwa kila siku mitaani. Kuhusu hili la KIATA itakuwa safi sana hawa matajiri wakija kukodisha na kusimamia uendeshaji mzima wa KIATA kwa mkataba wa win win situation mtawala na mtawaliwa wanufaike. Kodi watakayochukua serikali kutoka kwa hawa matajiri ktk huo mkataba wa ukodishaji inatosha kuleta maendeleo makubwa kwa maeneo mengine ya tanzania wakati huo huo maeneo ya KIATA yakiwa na maendeleo maradufu zaidi ya maeneo mengine tanzania. Isitoshe kuna wabunge wengi wa chadema arusha na kilima kyaro kwahiyo watasimamia ipasavyo utekelezaji wa mkataba
 
hapa kuna hoja ya mhimu sana, ila watu hawajaing'amua tu..kuna vitu vingi ambavyotunahitaji kuvifikiria kwa ajili ya msitakabali wa taifa letu..
 
Kwanza nilionyesha mshangao fulani, kwa kuwa tangu nianze kufanya biashara sijawahi kuulizwa biashara kama hii,. Nikawauliza watanunuaje? wakasema wao wana uwezo wa kuilipa serikali pesa za kutosha kuendesha bajeti ya Tanzania kwa 100% kwa kipindi cha miaka 15.Na wao wataichukua hiyo mikoa na kuimiliki kwa miaka 100
bajeti ya tz kwa mwaka ni $7bn kwa miaka 15 ni 7 x 15 equal to $105bn. hamna mtu mwenye hii hela kwa hiyo kama wewe uliwaamini watakuwa walikuona wewe ni mpu....vu. Na kama umetunga ili kufurahisha baraza................OMG
 
Mkuu umeangalia kwa upeo wa chini zaidi...nani kakuambia wawekezaji hua wanakua na hela cash baba!! Financial institution si zipo? ARUMERU HOTEL imekarabatiwa kwa sh ngapi kutoka kwenye bank za kitanzania?? ....
Sema hii mada tuachane nayo maana haijakaa vizuri
 
Kama tumeshindwa kusimamia uwekezaji kwenye madini. Je,kwenye mikoa mitatu yenye rasilimali nusu ya nchi nzima ndio tutaweza?
I think that info is wrong and misleading. Mikoa yenye utajiri wa maana kwa sasa ni ile yenye prospect ya mafuta na gesi,na pengine Uranium.
 
Haya ni matusi,

hawa wazungu wamekutukana na wewe ukalimbua macho, kama kawaida yetu watu weusi kushangaashangaa wazungu, ulitakiwa uwachallenge kwa njia nyingi badala ya kushangaashangaa
 
bajeti ya tz kwa mwaka ni $7bn kwa miaka 15 ni 7 x 15 equal to $105bn. hamna mtu mwenye hii hela kwa hiyo kama wewe uliwaamini watakuwa walikuona wewe ni mpu....vu. Na kama umetunga ili kufurahisha baraza................OMG

Semilong:

Hapa umetoka nje kibajeti. Serikali ya Tanzania yenyewe haina $105bn. Ilichonacho ni uwezo wa kukusanya revenue ya $7bn kwa mwaka. Kukusanya revenue ya $7bilioni ni kitu kinachowezekana.

Anyway, mada iliyowekwa hapa ilishajaribiwa Tanzania. As a matter of facts Tanganyika iliundwa kwa mfumo huo. Serikali ya Ujerumani chini ya Birsmark haikutaka kuwa na makoloni. Birsmark aliona kuwa makoloni yalikuwa yana gharama kubwa kuyaendesha na faida ndogo in return.

Lakini kutokana na uingereza kuendelea kupanua empire yake, baadhi ya wajerumani walihamua kuanzisha makundi yalioitwa German Colonial Association na Baadaye German Colonial Societies.

Hizi Societies bila kupata msaada wa serikali ya ujerumani waliweza kuanzisha na ku-sponsor German East Africa Company. Hivyo mkoloni wa kwanza wa Tanganyika ilikuwa ni kampuni ya kijerumani na sio serikali ya ujerumani. Hivyo uwezekano wa kampuni kutawala nchi upo.

Pamoja na hayo kampuni lolote linafanya kazi kwa interests za stakeholder and shareholder wa kampuni hiyo. Interests zao ni profits. Hivyo basi hata kama profits itabidi kupatikana kwa ku-enslave watu wa mikoa hiyo, makampuni yatakuwa tayari kufanya hivyo.

Kwa mfano, German East Africa Company ilifanya mabadiliko makubwa lakini watu walikuwa watumwa ndani ya nchi yao wenyewe. Kampuni la matairi la Firestone lili-control Liberia hili kupata ulimbo wa kutengeneza matairi. Matokeo yake indigenous Liberians wakawa watumwa ndani ya nchi yao na kuleta vita vya kiraia vya 1990s.

King Leopold of Belgium alianzisha kampuni yake ambayo ilitawala Congo Free State ( DRC). Na matokeo yake aliwafanya watu watumwa ndani ya nchi yao na kupoteza maisha ya watu zaidi ya milioni 10 kwa ajiri ya kupata faida.

Pamoja na kupenda kwangu capitalism, uhuru siku zote unakuja kwanza. Kuuza nchi ni kupoteza uhuru wako. Ni afadhari ufe masikini kuliko mtumwa ndani ya nchi yako.
 
Kama kawaida yangu, mimi ni mjasiriamali, na biashara yangu ni kuuza chocho au kusaidia kuuza chochote ili mradi mnunuzi na mnunuaji wanaridhika na maslahi ya hiyo biashara.

Katika pilika zangu za weekend, nilikutana na mabwana fulani ktk mgahawa mmoja maarufu hapa New zealand. Ktk mazungumzo yetu wao walijitambulisha kwangu, wao ni mawakala wa Tajiri mmoja anaeitwa LORD CARRINGTON na shughuli zao kubwa ni kununua raslimali popote zilipo duniani.

Niliwaambia mimi natoka Tanzania, wakasema wanaijua vizuri sana na kila kitu kilichopo na tena wakanifahamisha kuwa siyo Tanzania tu, wanaijua Africa yote na vilivyomo. Mimi nikawauliza, Je kwa Tanzanian wao wanataka kununu nini?. Wao wakaniambia, Kama itawezekana wangependa kuuziwa mikoa mitatu ya Tanzania bara, TANGA, KILIMANJARO NA ARUSHA.

Kwanza nilionyesha mshangao fulani, kwa kuwa tangu nianze kufanya biashara sijawahi kuulizwa biashara kama hii,. Nikawauliza watanunuaje? wakasema wao wana uwezo wa kuilipa serikali pesa za kutosha kuendesha bajeti ya Tanzania kwa 100% kwa kipindi cha miaka 15.Na wao wataichukua hiyo mikoa na kuimiliki kwa miaka 100

Mimi kwangu niliona ni biashara nzuri, lakini wasi wasi wangu ikawa ni kujua kama watanunua je ina maana raia wanaoishi ktk mikoa hiyo watafukuzwa au itakuwa namna gani?

Wao wakanijibu, kila raia atabaki kuwa ni mmiliki wa mali zake kwa 100% Ila wao watakachofanya ni kuunda serikali yao mpya ktk mikoa hiyo,na kuwekeza ktk mikoa hiyo na kuwasaidia mitaji ya kuwekeza raia wanaoishi ktk mikoa hiyo ili waweze kukusanya vizuri mapato yao.

La mwisho waliloniambia ni kuhusu sheria za uhamiaji, Kwamba ni lazima kwa mtu au taifa lolote watalazimika kuwa na VIZA za kuingi ktk mikoa hiyo, na pia baada ya miaka 100 watairudisha mikoa hiyo mikononi mwa serikali ya Tanzania

Mimi kabla ya kuwajibu ikabidi niwaombe muda kidogo ili niwasiliane na wadau na tujadili kama kuna faida au hasara halafu mtaliwakilisha kwa JK na serikali yake nao waone kama linafaa. LAKINI KWA UPANDE WANGU NIMEKUBALIANA NAO KWA 100% MAANA KWA KIPINDI CHA MIAKA 15 HATUTAKUWA TENA OMBA OMBA KWA WAZUNGU, NA ISITOSHE KUMBE NI KAMA WANAKODI TU HIYO MIKOA NA SIYO KUINUNUA KABISA.

MWISHO NAOMBA WANA JF TULIJADILI HILI KIBIASHARA ZAIDI NA SIYO KISIASA
Hii hoja ni ya msingi na ina mengi ya kuchambua,kujiuliza n kutafakari. Machache n kama ifuatavyo: 1. Mtoa hoja lazma anatoka ktk mikoa hyo n perspection yake n kuwa KIATA is a selective region ambao anaamn kuwa ina watu wenye hadhi,uelewa,elimu,mwamko mkubwa sana so maeneo mengine yanachangia kudumaa kwao! 2. Yule chief mangungo na Karl Peters walianza na kasehemu kidogo tu lkn hatimaye Tanganyika yte ikawa koloni la Germany! 3. Mtohoja amejenga taswira kwamba raslimali zlizopo KIATA pekee zina uwezo wa kuchange livelihood ya jamii y watz,vp raslmali za nchi nzima zikashindwa kuchange maisha y watz? Challenge to tz' leader! 4. Anatoa taswira kwmba wakti umefika kwa tz kuongozwa ki-zones! 5. Viongozi wa tz n after-maslah kiasi kwamba wanaweza kuuza hta watu wao ili kukamilsha wishes zao! 6. Serikali haina uwezo wa kusmamia raslmali zake kwa maslah ya watu wake kiasi kwmba mtoa hoja anawaonea huruma sn wtz hata anatamani viongozi wawe "wazungu" ili wasmamie raslmali zilizopo kwa uadilifu ili watu wawe na gd life! 7. Tanzania iko ktk 'excited state' kiasi ambacho kila mtz ana view yake y namna y kuitoa ktk hali hyo! Dah!yako mengi bt now I bcam tired! Viva mtoa hoja-wapeni bana hyo KIATA ila angalieni wastamani morogoro then mkaja kosa maji+umeme japo kwa huo mgawo!
 
Mtoa mada na hao watu wako akili zenu zilienda likizo. Tuacheni na umaskini wetu na nchi yetu. Sheria gani ulimwenguni inaruhusu biashara iliyo zaidi ya haramu kama hiyo.
 
Kuhusu kigamboni nibora tukawa na ushahidi dhahiri badala ya kuendeleza porojo zinazopigwa kila siku mitaani. Kuhusu hili la KIATA itakuwa safi sana hawa matajiri wakija kukodisha na kusimamia uendeshaji mzima wa KIATA kwa mkataba wa win win situation mtawala na mtawaliwa wanufaike. Kodi watakayochukua serikali kutoka kwa hawa matajiri ktk huo mkataba wa ukodishaji inatosha kuleta maendeleo makubwa kwa maeneo mengine ya tanzania wakati huo huo maeneo ya KIATA yakiwa na maendeleo maradufu zaidi ya maeneo mengine tanzania. Isitoshe kuna wabunge wengi wa chadema arusha na kilima kyaro kwahiyo watasimamia ipasavyo utekelezaji wa mkataba

Mkuu,hta view ya Kigamboni namna itakavyokuwa imeshatoka na binafsi meshaiona! Very attractive view ever seen in Africa. Plz hlo uskaidi!
 
Tanzania yenyewe ilishauzwa kitambo, na mmiliki halali hatumjui mpaka leo.

Eti anataka kununua Hiyo mikoa. Hiyo mikoa iuzwe mara ngapi?
 
Mimi ninacho ona hapa ni watawala wetu kufundishwa namna mikoa hiyo inavyoweza kutufanya tuondokane na umaskin wa kutupwa unao tusumbua na kumfanay JK awe kiguu na njia kwenda kuhemea vibaba Ulaya.

Kwa kutumia mikoa hii 3 nchi inaweza kupiga hatua kubwa ya kiuchumi, Hapo hatuja jumuisha bonde la mto rufiji,, mbalizi na ihefu ambayo yakitumika vizuri tunaweza hata kulisha Africa mashariki na kati na sisi tunakabaki na chakula cha kutosha na tukasitisha kuagiza Mchele kutoka Japani na India.

Hao wanaosema wanataka kununu hiyo mikoa kwa ajili ya kufanya biashara wanatutoa tongo tongo ili tufumbuke macho.
 
Mimi nimeipenda, baada tu ya uchaguzi nilitamani kanda ya kaskazini ingekua nchi nyingine na sio Tz. Huyu jamaa amefikiria sana hii mikoa acha tu rasilimali pia ina wasomi na wachapa kazi. wazalishaji wapo ni kuwajengea mazingiza ambayo viongozi wetu wameshindwa kuyajenga. Mungu Ikumbuke Tz
 
Haya ni matusi,

hawa wazungu wamekutukana na wewe ukalimbua macho, kama kawaida yetu watu weusi kushangaashangaa wazungu, ulitakiwa uwachallenge kwa njia nyingi badala ya kushangaashangaa

Ok, kama mitizamo yetu wote ni kama wa kwako, Basi tutachelewa sana, Mimi nafikiri ungejaribu kufikiri na kichwa japo kidogo kabla ya kuchangia hoja, sasa ninakuuliza swali, je kwa sasa Tanzania inanufaika vipi na mikoa hiyo? je pato la mikoa hiyo ktk serikali ni % ngapi?. Je? kama kweli anakuja mwekezaji ambaye anataka kutulipa pesa ya kuendesha serikali pamoja na miradi yake ya maendeleo kwa miaka 15. tutakuwa tumepata faida au hasara?
 
Hii hoja ya Major sio ya kufikilika bali he is sending a message ambayo watu wanaweza kufikiria!! Kama wafanyabiashara wanaweza kuendesha bajeti ya nchi kwa muda wote huo kwa kumiliki mikoa mitatu tu ; je nyie serikali ya wachakachuaji mbona mnashindwa kuendesha nchi na kuwa ombaomba kila leo huku mna rasilimali ya mikoa ishirini na moja? Hiyo ndio changamoto ya hoja ya Major!
 
Kama kawaida yangu, mimi ni mjasiriamali, na biashara yangu ni kuuza chocho au kusaidia kuuza chochote ili mradi mnunuzi na mnunuaji wanaridhika na maslahi ya hiyo biashara.

Katika pilika zangu za weekend, nilikutana na mabwana fulani ktk mgahawa mmoja maarufu hapa New zealand. Ktk mazungumzo yetu wao walijitambulisha kwangu, wao ni mawakala wa Tajiri mmoja anaeitwa LORD CARRINGTON na shughuli zao kubwa ni kununua raslimali popote zilipo duniani.

Niliwaambia mimi natoka Tanzania, wakasema wanaijua vizuri sana na kila kitu kilichopo na tena wakanifahamisha kuwa siyo Tanzania tu, wanaijua Africa yote na vilivyomo. Mimi nikawauliza, Je kwa Tanzanian wao wanataka kununu nini?. Wao wakaniambia, Kama itawezekana wangependa kuuziwa mikoa mitatu ya Tanzania bara, TANGA, KILIMANJARO NA ARUSHA.

Kwanza nilionyesha mshangao fulani, kwa kuwa tangu nianze kufanya biashara sijawahi kuulizwa biashara kama hii,. Nikawauliza watanunuaje? wakasema wao wana uwezo wa kuilipa serikali pesa za kutosha kuendesha bajeti ya Tanzania kwa 100% kwa kipindi cha miaka 15.Na wao wataichukua hiyo mikoa na kuimiliki kwa miaka 100

Mimi kwangu niliona ni biashara nzuri, lakini wasi wasi wangu ikawa ni kujua kama watanunua je ina maana raia wanaoishi ktk mikoa hiyo watafukuzwa au itakuwa namna gani?

Wao wakanijibu, kila raia atabaki kuwa ni mmiliki wa mali zake kwa 100% Ila wao watakachofanya ni kuunda serikali yao mpya ktk mikoa hiyo,na kuwekeza ktk mikoa hiyo na kuwasaidia mitaji ya kuwekeza raia wanaoishi ktk mikoa hiyo ili waweze kukusanya vizuri mapato yao.

La mwisho waliloniambia ni kuhusu sheria za uhamiaji, Kwamba ni lazima kwa mtu au taifa lolote watalazimika kuwa na VIZA za kuingi ktk mikoa hiyo, na pia baada ya miaka 100 watairudisha mikoa hiyo mikononi mwa serikali ya Tanzania

Mimi kabla ya kuwajibu ikabidi niwaombe muda kidogo ili niwasiliane na wadau na tujadili kama kuna faida au hasara halafu mtaliwakilisha kwa JK na serikali yake nao waone kama linafaa. LAKINI KWA UPANDE WANGU NIMEKUBALIANA NAO KWA 100% MAANA KWA KIPINDI CHA MIAKA 15 HATUTAKUWA TENA OMBA OMBA KWA WAZUNGU, NA ISITOSHE KUMBE NI KAMA WANAKODI TU HIYO MIKOA NA SIYO KUINUNUA KABISA.

MWISHO NAOMBA WANA JF TULIJADILI HILI KIBIASHARA ZAIDI NA SIYO KISIASA

Haya mambo ni kama yakufikirika hivi.Lakini hata kama ingekuwa kweli. ni mafisadi tu, tena wale wa kutisha, wanaoweza hata kufikiri tu jambo la kipuuzi namna hiyo!This to me is out of discussion and unthinkable.
 
Hii hoja ya Major sio ya kufikilika bali he is sending a message ambayo watu wanaweza kufikiria!! Kama wafanyabiashara wanaweza kuendesha bajeti ya nchi kwa muda wote huo kwa kumiliki mikoa mitatu tu ; je nyie serikali ya wachakachuaji mbona mnashindwa kuendesha nchi na kuwa ombaomba kila leo huku mna rasilimali ya mikoa ishirini na moja? Hiyo ndio changamoto ya hoja ya Major!

Nashukuru sana, kwa kutambua. na pia mimi naona ni bora wawauzie kwa sababu wala sioni kama kuna mpango wowote wa kuiendeleza mikoa hiyo, badala yake naona kama kuna kusudi maalum la serikali kiuwa kabisa. Ebu fikiri Tanga ya zamani na Tanga ya leo!!! tizama bandari ambayo wakati wa mkapa zilikuwa zinatia nanga meli mpaka 20 kwa mwezi,lakini leo inasimama meli moja baada ya miezi mitatu.Tizama reli ya Tanga leo. Angalia viwanda lukuki vilivyokua Tanga, na mambo mengi ambayo kwa mfanyabiashara kama mimi yananitia uchungu.

Tuje Kilimanjaro, ni Aibu, serikali ilibinafsisha viwanda vyote kwa watu wanaowajua wao, matokeo yake leo, kwa makusudi wakafunga viwanda na kugeuza maeneo yale kuwa magodown. Leo hii kilimanjaro hakuna ajira yoyote. na Arusha ni hivyo hivyo. SASA SI BORA WAWAUZIE WATU AMBAO TAYARI WALISHAJUA MAANA YA HII MIKOA?!!
 
Ok, kama mitizamo yetu wote ni kama wa kwako, Basi tutachelewa sana, Mimi nafikiri ungejaribu kufikiri na kichwa japo kidogo kabla ya kuchangia hoja, sasa ninakuuliza swali, je kwa sasa Tanzania inanufaika vipi na mikoa hiyo? je pato la mikoa hiyo ktk serikali ni % ngapi?.

Tuko na resource nying kwenye hiyo miko,pamoja na utaalam mdogo wa technologia, tutaweza kufaidika zaidi in long run chini ya utawala wetu wenyewe waafrika

Je? kama kweli anakuja mwekezaji ambaye anataka kutulipa pesa ya kuendesha serikali pamoja na miradi yake ya maendeleo kwa miaka 15. tutakuwa tumepata faida au hasara?

Ili mimi naliona kama tusi au dharau, hakuna mtu anaweza uza utu wake kwa sababu ya maendeleo, tutakuwa tunajitawala au tunatawaliwa? hili ndilo alilo kataa Mugabe Zinbabwe land for zinbwabweans, na ndicho alicho kataa Nyerere.

Naamini maendeleo wa tanzania na afrika yataletwa na waafrika wenyewe, tusisahau kuwa, part ya matatizo tanzania na frika chanzo chake ni wao wazungu.

tunakesi nyingi WTO kuusiana na level play field ya biashara, lakini jamaaa wako wazungu hawataki kubadilika

Kumbuka hao wazungu are fighting to keep their interest around the world, wakikuona unaaza kuendelea wao wanapambana na wewe

Kumbuka BARICK Gold, walipo ona bunge letu limepitisha sheria za kufaidika na dhahabu zetu, walitutishia amani mpaka leo hatuwezi kupitisha mambo yetu ktokana na ubabe wao
 
Haya mambo ni kama yakufikirika hivi.Lakini hata kama ingekuwa kweli. ni mafisadi tu, tena wale wa kutisha, wanaoweza hata kufikiri tu jambo la kipuuzi namna hiyo!This to me is out of discussion and unthinkable.

Ok, wewe inaonekana ni mmoja wa wale watu wavivu wa kufikiri, just why you think that is unthinkable. na hata watawa wa tanzania wanajua kuna watu mazezeta kama wewe, ndiyo maana huwa hawana wasi wasi, na mambo ya hovyo wanayofanya. Sasa wewe nakuuliza swali moja dogo kabisa. " Tanzania ilianza kuzalisha gesi yake ya asilia tangu mwaka 1995, huu ni utajiri mkubwa kabisa kama vile ilivyo utajiri wa mafuta ktk nchi nyingi duniani, hii gesi inaweza kutumika vizuri kwa 100% ktk magari yote yanayotumia petrol nchi nzima na hii itaokoa pesa nyingi sana ya kigeni inayotumika kununulia hayo mafuta, na kama inatumika kikamilifu pia shilingi yetu inaweza kupanda thamani kwa zaidi ya 36%

Maajabu ya Tanzania yenye viongozi wenye akili za SAMAKI eti hilo wamelifumbia macho kana kwamba hiyo gesi pia inatoka Uarabuni. SABABU Kubwa ni maslahi wanayopata viongozi wawili watatu tu ktk hayo mafuta yanayoagizwa kutoka nje, TAARIFA za kitaalamu, zinaonyesha kwamba ikiwa mwenye gari atatumia gesi asilia ataokoa mpaka 70% ya garama ya uendeshaji wa gari lake, hii ni kama neema kwa Watanzania

TAARIFA za kweli, Bwanamdogo W Ngeleja alipotembelea maonyesho ya biashara sabasaba ya mwaka 2007, aliingia ktk banda la Watanzania ambao wao wanafunga "CNG KIT" KTK haya magari ya petrol, ambapo unaweza kutumia gesi yetu au wakati huo huo unaweza kuamua ukatumia petrol, Jamaa aliwaahidi, Ni lazima magari yote ya serikali yaanze kutumia hii ges ili serikali ionyeshe mfano wa kuikubali bidhaa yake.

HABARI za kuaminika ni Kwamba bwanamdogo, ngeleja kweli alijitutumua na kuwasilisha hoja yake serikalini, Serikali ilikubaliana naye kwa 100% lakini MADEREVA wa hayo magari ya Serikali walikataa hiyo hoja, SABABU, eti hawaiamini hiyo gesi, LAKINI SABABU YA MADEREVA KUIKATAA NI KWAMBA WANGESHINDWA KUUZA MAFUTA WANAYOIBA KTK HAYO MAGARI YA SERIKALI. NA VILE VILE HAWANGEWEZA KUIBA GESI, "TAFAKARI" HIYO NDIYO TANZANIA YETU, Kwa hiyo mpaka leo gesi ipo ya kutosha kabisa lakini hatutaki kuitumia kwa ajili ya ushauri wa madereva wa serikali ambao wengi elimu yao ni ya darasa la nne la RAIS MWINYI, I SAY, THAT IS REAL SHAME ON US
 
Back
Top Bottom