Tanzania yapata ofa ya kuuza mikoa mitatu.tanga, kilimanjaro na arusha

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,866
2,000
Kama kawaida yangu, mimi ni mjasiriamali, na biashara yangu ni kuuza chocho au kusaidia kuuza chochote ili mradi mnunuzi na mnunuaji wanaridhika na maslahi ya hiyo biashara.

Katika pilika zangu za weekend, nilikutana na mabwana fulani ktk mgahawa mmoja maarufu hapa New zealand. Ktk mazungumzo yetu wao walijitambulisha kwangu, wao ni mawakala wa Tajiri mmoja anaeitwa LORD CARRINGTON na shughuli zao kubwa ni kununua raslimali popote zilipo duniani.

Niliwaambia mimi natoka Tanzania, wakasema wanaijua vizuri sana na kila kitu kilichopo na tena wakanifahamisha kuwa siyo Tanzania tu, wanaijua Africa yote na vilivyomo. Mimi nikawauliza, Je kwa Tanzanian wao wanataka kununu nini?. Wao wakaniambia, Kama itawezekana wangependa kuuziwa mikoa mitatu ya Tanzania bara, TANGA, KILIMANJARO NA ARUSHA.

Kwanza nilionyesha mshangao fulani, kwa kuwa tangu nianze kufanya biashara sijawahi kuulizwa biashara kama hii,. Nikawauliza watanunuaje? wakasema wao wana uwezo wa kuilipa serikali pesa za kutosha kuendesha bajeti ya Tanzania kwa 100% kwa kipindi cha miaka 15.Na wao wataichukua hiyo mikoa na kuimiliki kwa miaka 100

Mimi kwangu niliona ni biashara nzuri, lakini wasi wasi wangu ikawa ni kujua kama watanunua je ina maana raia wanaoishi ktk mikoa hiyo watafukuzwa au itakuwa namna gani?

Wao wakanijibu, kila raia atabaki kuwa ni mmiliki wa mali zake kwa 100% Ila wao watakachofanya ni kuunda serikali yao mpya ktk mikoa hiyo,na kuwekeza ktk mikoa hiyo na kuwasaidia mitaji ya kuwekeza raia wanaoishi ktk mikoa hiyo ili waweze kukusanya vizuri mapato yao.

La mwisho waliloniambia ni kuhusu sheria za uhamiaji, Kwamba ni lazima kwa mtu au taifa lolote watalazimika kuwa na VIZA za kuingi ktk mikoa hiyo, na pia baada ya miaka 100 watairudisha mikoa hiyo mikononi mwa serikali ya Tanzania

Mimi kabla ya kuwajibu ikabidi niwaombe muda kidogo ili niwasiliane na wadau na tujadili kama kuna faida au hasara halafu mtaliwakilisha kwa JK na serikali yake nao waone kama linafaa. LAKINI KWA UPANDE WANGU NIMEKUBALIANA NAO KWA 100% MAANA KWA KIPINDI CHA MIAKA 15 HATUTAKUWA TENA OMBA OMBA KWA WAZUNGU, NA ISITOSHE KUMBE NI KAMA WANAKODI TU HIYO MIKOA NA SIYO KUINUNUA KABISA.

MWISHO NAOMBA WANA JF TULIJADILI HILI KIBIASHARA ZAIDI NA SIYO KISIASA
 

jyfranca

JF-Expert Member
Oct 3, 2010
297
0
kama huna cha kuchangia bora kanywe gongo. Habari zako pumba tupu na wala hujui kutengeneza habari, hata mjinga anajua umetunga, pumbavu nenda shule
 

Gsana

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
4,383
1,500
Mr Major,iyo ni dili zuri ila naisi inapendeza zaidi ktk fikra kuliko vitendo. Guess umeuza mikoa iyo kumbe wanataka jenga vinu vya nyuklia!au wanawekeza magaidi akina Bin laden!au wanakuja na kilimo cha bangi! Au wanataka kulifanya jalala ili wenye taka duniani walete hapo? Always subject matter of the contract matters than its consideration. Proposal pekee jk anawezasaini kama ungepata watu wa kujenga capital city zanzibar kama ilivo kgamboni ingeleta maana zaidi. Unajua by 2035 Kigamboni is designed to be the most luxurious city in whole Africa! Plan starts by 2011 kwa kujenga kwanza daraja la kigambon,ktuo cha gari kasi kivukon. N.k.
 

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,202
0
what happens wakishanunua alafu wakaongeza kodi za ajabu ajabu ambazo wazawa wote wakashindwa kuzilipa..... ???
 

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,175
1,195
Nafikiri waPM RA au EL najua watakusaidia sana. Kila kitu kinawezekana and it begins with you!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 

Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,586
2,000
Nimekupata mkuu vizuri sana, hakika kiyo mikoa mitatu tu inatosha kuendesha na kuinua uchumi wa nchi hii bila kutegemea mikoa mingine. Kwa mfano, rasilimali kama Mlima Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro, Mbuga za Wanyama huko Serengeti, na Bandari iliyosahaulika ya Tanga na ardhi nzuri kule Lushoto na Pangani pamoja na Vivutio vingi vya utalii.

Hakika hata kama ni mawazo yako ya kufikirika kwa mtu makini ni changamoto ya kutosha.

Kwenu Watawala wetu, najua kwa mtizamo wenu mdogo mtaona huyu jamaa karopoka.
 

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,805
1,225
Wanajua kuwa Loliondo tuliuza kwa waarabu kwa hio msiiweke kwenye plan zenu. Hata hivyo wamechelewa tushauzwa siku nyingi na alie tununua ni m-USA kupitia kwa mkaburu, wakaanza na mabenki na unajua ukisha kontrol fedha ni kila kitu.
 

Keynes

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
533
225
Hii mikoa ni hatari sana kujadiliwa humu tunaomba MODE uondoe hii threads.
Kuna jamaa tulikua naye mahala fulani tunapiga umbea AKASEMA kulingana na unyonyaji wa serikali na UFISADI yeye anataka aende umoja wa mataifa akadai uhuru wa nchi ya KIATA!! Nikamuuliza hii nchi ya KIATA iko wapi? Alijibu hii ni kilimanjaro arusha na tanga...hakuishia hapo kaanza kutaja sababu.
1. Alianza na dolla...Tuna chuo kikubwa cha polisi moshi na kambi kubwa ya jeshi monduli
2. Utalii....mbuga zote kubwa za wanyama zipo arusha, mlima kilimanjaro
3. rasilimali...madini yote ikiwemo tanzanite yanapatikana mikoa ya arusha na tanga
4. usafiri...akasema ana kiwanja cha ndege cha kimataifa cha kilimanjaro pamoja na bandari ya tanga
5. elimu ..akasema ana vyou vikuu vya kutosha na mashule ya kutosha ni kiasi cha kuboresha tu
6. huduma za jamii kama vile maji na afya...alisema kule wana hospitali za kutosha kama vile kcmc na maji kule siyo tatizo kule ndo yanapotokea
7. Nishati..alisema analo bwawa la nyumba ya mungu linatosha
HUYU JAMAA ALIELEZA UPUUZI MWINGI SANA HATA MENGINE SIKUMBUKI NA ALINIOGOPESHA SANA.
Mwishowe alisema kama atafanikiwa kwa muda wa miaka 5 KIATA itakua kama HONG KONG AU SINGAPORE.
 

De Javu

JF-Expert Member
May 5, 2010
265
0
Nadhani hapa watu wanakurupuka bila ya kujua undani wa hii hoja, yawezekana kabisa kukodisha eneo kama ilivyokua Hongkong toka China au Macao, tatizo lipo kwa hao watakaoingia mikataba na hao wajasirimali. Tatizo la Tanzania ni viongozi wanaongia mikataba wakiwa hawajui nini wanafanya zaidi ya kukimbilia chajuu chao. Mifano ya wazi ni kama Tanesco na Richmond, Dawasco na NBC etc. Kweli kutawaliwa kubaya, lakini angalia Afrika ya kusini au hata Zimbabwe zilizopata uhuru baada ya Tanzania, ziko wapi ki miundo mbinu ukilinganisha na Tz iliyojitawala miaka yote hiyo ?
 

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,690
2,000
Hivi hii inawezekana, mimi ndio kwanza naisikia biashara ya namna hii!!
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,694
2,000
Badala ya kumshambulia Major ambaye ni mtoa habari jadilini hoja. Ndio maana watu uleta hoja hapa ili zinyambuliwe. Tuwe great thinkers kweli.
 

Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
4,460
2,000
Hivi hii inawezekana, mimi ndio kwanza naisikia biashara ya namna hii!!

Mkombe biashara hiyo ipo tangu zamani tu, mfano eneo la Guantanamo Bay ambapo kuna kambi ya kijeshi ya Marekani pamoja na ile jela maaruf kwa kashfa za haki za kibinadamu ni eneo la Cuba lakini walilikodisha kwa Marekani miaka mingi sana iliyopita kabla ya akina Castro...

Pia Alaska iliuzwa na Urusi kwa Marekani miaka mingi sana iliyopita...
 

Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,150
2,000
Kama tumeshindwa kusimamia uwekezaji kwenye madini. Je,kwenye mikoa mitatu yenye rasilimali nusu ya nchi nzima ndio tutaweza?
 

Njilembera

JF-Expert Member
May 10, 2008
1,495
2,000
Nimepinda hii hoja HATA kama ni ya kufikirika! Mantiki iko pale unapoangalia Tanzania, nchi pekee Africa iliyobahatika kuzungukwa na maji kila upande. Hata bila ya kufikiria HUO UKANDA WA Tanga Killy na Arusha, ungeliweza kufikiria Mbeya Sumbawanga na Njombe/Iringa. Yaani kanda mmoja ina utajiri wa ajabu wa kuweza kulisha taifa kwa miaka nenda rudi. Sembuse kanda zote! Ukweli uchumi tumeruhusu ukakaliwa na wasiofikiria kibiashara hata kidogo. Wao wakipata katripu ka Ulaya wakanunuliwa suti wakawekwa hotelini na mamsepu mzungu wanafikiri ndio maana ya kuwa viongozi na wanaona fahaari kufanikiwa. Na watakaporuhusiwa kushikana na mkono na viongozi wa kimarekani picha zinazopigwa huhifadhiwa miaka nenda rudi kama vile zitalipa kuwa nazo.

Nimependa hii hoja maaana inatekenya akili, nipeni kasehemu ka nchi yenu tu, nikodisheni wala msiwe na shida wakazi hawatakuwa na shida, lakini kwa kutumia ustadi wa kibiashara hio pesa ya kuikodi tutairudisha na tutafaidika kwa kiwango chetu. Bongo tumelala! Tuamke!

Nimependa pia hoja ya mchangiaji hapo juu ingawaje anasema alijawa na hofu kwa waliokuwa wanafikiria kujitangazia jamhuri yao wenyewe. Kweli kuna watu wanataka kwenda mbele lakini Dar inawavuta kamba. Wafanye nini kama sio kukata hio kamba. Inatisha lakini kuna wakati unafika na kuwaza kweli mimi na baba huyu niendelee naye tu, nife mnyonge au nijitoe nimkache, halafu na yeye ataona umuhimu. Hili linchi akipewa mtu mwaadilifu, hakuna nchi Africa itakayotukaribia kuanzia raslimali, biashara na hata michezo. Mungu Ibariki Tanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom