Tanzania yapata msaada wa $900m za kilimo kutoka G8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yapata msaada wa $900m za kilimo kutoka G8

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saranda, Aug 1, 2012.

 1. S

  Saranda Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni miongoni mwa nchi teule tatu zilizobahatika kupata msaada wa kilimo katika mpango African food security. Sasa njaa itakwisha na mipango ikienda vizuri tutakuwa na uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa hadi kuweza kuuza chakula nje ya nchi.

  Kwa hili Dr. kikwete amefanya kazi vizuri na anastahili pongezi.
   
 2. L

  LIWALONALIWE Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kupongeza ni muhimu ila mimi sidhani kama kuna haja kwani hii miaka mitatu iliyobaki kwa huyu Dr.wetu mambo atakayo yafanya watu watabaki midomo wazi.Nasema hivi kwasabau kuan watu hapa ahata ukifanya mazuri vipi wao ni kuponda tu sasa ni matendo kwenda mbele.
  Kama kuna mtu ni ksafiri kwa kazi zake za kijikimu utaona nchi nzima matrekta ya kilimo kwanza yamejaa.sasa na hizi pesa ndio itamaliza kabisa.
   
 3. L

  LIWALONALIWE Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 29, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Liwalonaliwe
   
 4. m

  mnduoeye Senior Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni fedha nyingi sana zinaletwa na wafadhili lakini zinaishia mifukoni mwa watu wachache. tusimpongeze kwa kuleta fedha asimamie matumizi yawafikie walengwa yaani wakulima na kkuanzisha miradi ya umwagiliji ndio tumpongeze.Hakuna maandalizi yeyote kwa miaka nenda miaka rudi ya kilimo cha umwagiliaji wakati tuna mabonde mengi waaongelea kila budget lakini imekuwa kwenye makabrsha maofisini bila utekelezaji.Mabilioni ya Kikwete tuliandika miradi mizuri ya kilimo lakini waliopewa hata hatutaki kukumbuka na hazijarudishwa na hazitarudishwa tulie tu ndugu yangu .
   
 5. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Hela za kutafuna hizo! Wacha zije uone kama kutakuwa na kilimo au muongezeko wa magorofa!
   
 6. igwana123

  igwana123 Senior Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwa hilo jamani tuwe unauwezo wa kuchanganua masuara ya inchi. Penye mazuri tupongeze kwa zati. Tanzania imepata msaada huo wa kilimo, pongezi Rais kwa hiro asie liona hilo sasa hana macho!
   
 7. sister

  sister JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,026
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  fadha si tatizo..........tatizo ni kwamba hayo malengo yaliyowekwa kwa ajili ya hizo fedha yatatimizwa.
   
 8. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kupata fedha na kuinua hali ya kilimo nchini ni mambo mawili tofauti
   
 9. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubliana na wewe tatizo letu kuu ni namna ya kutumia pesa. hatuna nidhamu kwenye matumizi. Kwahiyo hata kama ni kweli tumepata msaada huo kwa ajili ya kilimo usishangae zikapelekwa kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya IPTL ambako mikono yote ya watawala wajasiria mali inafika.
   
 10. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  nadhani baadhi yetu tunafikiri kuwa kuna maofisa wa serikali watakuwa na vifurushi vya hizo pesa wakipita mashambani/vijijini wanawagawia wakulima, kumbe hizo power tiller zilizopo hapo Lugalo watakwambia ndio sehemu ya hizo pesa pamoja na malipo ya hizo pembejeo zinazosemekana kuwa fake. Tusubirini na tutaona

   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tusifurahie sana hela za Wamarekani maana wana nia tata sana. Misaada ya Bush kupitia account ya MCC (USD 700M) ndiyo hiyo hiyo sehemu yake ilitumika kuleta Symbion. Hizi za Kilimo Kwanza sijui zitaleta nini?
   
 12. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Saranda,

  Tatizo nchi hii si fedha, ni mfumo na watu wake. Mfumo umesababisha tusahau kuwa akili yaweza kuleta maarifa! Hizo fedha wajnja wachache watazichungulia na kuzitangizia!!

  We are doomed!!!!
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Misaada mingapi imefika hapa nchini kwetu na kwa uhalisia imefanya nini
  Kwanza wajiulize zile pesa za EPA walizosema zinaenda kweney kilimo kwanza zimetumikaje na nani waliofaidi hizo pesa
  kabla ya kushangilia msaada mwingine
  Tunashangilia msaada wakati kila kitu tunacho cha kuweza kuzalisha zaidi ya huo msaada
  Hatupaswi hata kushangilia ila tunapaswa tusikitike maana hao waliotupa huo msaada wamepata na kuvuna zaidi ya hizo hapa kwetu
   
 14. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  katika hizo $900m.. $500m watagawana wanasiasa na wafanyabiashara. $250m watapewa watu wa nje na hawata fanya lolote [ wazungu na wachina] $100m zitapotea wizarani. $50m ndo watajaribu kuifanyia kazi. shida sio kupewa hizo fedha. shida ipo kwenye usimamizi mzuri wa hizo fedha..
   
 15. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Misaada kila siku na sioni mabadiliko, wajanja watazigawana tu hizo, waendelee kujenga mahekali na kuanzisha vituo vya mafuta. (Lake Oil)
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Siungi mkono sababu nimesomeshwa na kilimo, toka miaka ya themanini hakuna improvement yoyote ile serikali imefanya, wakulima zana ni zile zile, jembe la mkono, hizo pesa wajanja watazitafuna zote
   
 17. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,053
  Likes Received: 3,964
  Trophy Points: 280
  suorce wapi mzee ya hii habari yako?
   
 18. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Msongamano wa magari ya kifahari utaingezeka maradufu. Wsiokuwa kwenye mkondo wa pesa hio, kaeni chonjo.
   
 19. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  imepata msaada huo waje wachukue vizuri gesi na mengineyo kibao yaliyoko nchii hii ya ma chowderheads
   
 20. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  JK ana nia thabiti ya kuendeleza kilimo na mambo mengine - we sema kuna viongozi wenzake wako hell bent ku-undermine effort ZAKE ili aonekane ni wanting! Hii haina ukweli wowote.

  Mimi kwa maoni yangu JK anapaswa kufanya radical changes katika wizara ya kilimo, bila kufanya hivyo hizo funds will end up not serving any useful purpose! Zitaishia GOD knows where?

  Nilisha sema humu kwamba matatizo ya Wizara ya Kilimo hayana tofauti na Wizara ya Nishati na Madini specifically TANESCO, tukitaka TAIFA letu libadilike katika nyanja za kilimo, uongozi mzima wa SECTOR hii unapaswa kubadilishwa kama walivyo fanya TANESCO-mwenye kuona umwambii atazame! Borrow a leaf from Prof. and Patriotic MASWI, team hii ndio itakuwa PANADOL ya endemic ufisadi wa TANESCO.
   
Loading...