Tanzania yapata Mkopo wa Sh. Trilioni 3.3 toka Standard Chartered Bank kwa ajili ujenzi reli ya SGR

Tunapoelekea sio pazuri. Mikopo ni mingi mno na bado hali za kiuchumi za wananchi ni ngumu.

Kama hatutaimarisha na kuweka mazingira ya uchumi wetu kukua basi madhara ya mikopo hii inaweza kuonekana na kuwepo hata miongo mitano ijayo
Na sehemu kubwa ya mikopo hiyo inatumika kununua wapinzani na kufadhili vikosi vya kigaidi vya Wasiojulikana.
 
Tutasonkolwa mpaka tukome! Hasa tukirejelea kale ka kauli ka kuwa donor country
 
Wewe usijitekenye. Hakuna nchi duniani isiyokopa, tuondolee kelele zako hapa

Sent using Jamii Forums mobile app

Uzuri sasa hivi ule uongo kuwa tunajenga miradi kwa pesa zetu za ndani umefutika rasmi, na kile tunachosema kuwa hali ya makusanyo ni duni kinaendelea kuwa wazi zaidi. Deni la taifa kwa muda mfupi limekuwa kubwa ili kusaka sifa za kisiasa, huku uwezo halisi wa kulipa hayo madeni ukizidi kuwa mdogo.
 
Haya mambo ya kukopakopa wakati tunatumia matrilioni kununua ndege cash yatakuja kugharimu huko baadaye, sioni uchumi unaokua kuweza kulipa hayo madeni makubwa. Wakishaingia wale akina moody na standard&poor kutu-downgrade tutarudi kuwaimbia mabeberu kale ka-wimbo ka kuomba kusamehewa madeni....watch it.
 
..kwanini tuliwasamehe barrick deni la usd 191 billion?
Labda kwa sababu deni lilikuwa feki?

Itaonekana sasa wakati kontena za makinikia kwenye bandari zinauzwa.
Wanakemia wa serikali walidai wakati ule zina dhahabu mara ngapi (ilikuwa mara 10, 20?) kuliko walivyosema Barrick.

Kama hii ni kweli, basi kampuni mpya (50% za serikali) itapata pesa nyingiiiiii sana.
Kama wimbi hili la pesa halionekani, basi makadiriko yalikuwa feki pamoja na bilioni za USD.
Tutaona
 
Tatizo siyo kukopa ila wanakopea mradi wa kipuuzi usio na tija.
 
Back
Top Bottom