Tanzania yapata mkopo kuendeleza miradi ikiwemo reli ya SGR

comrade wetu

JF-Expert Member
Nov 5, 2018
964
605
6354f62776992aa5e508cb5bd424ee1e


Benki ya Biashara na Maendeleo imetoa mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1 (sawa na shilingi Trilioni 2.778) hapa nchini na hivi sasa inakamilisha taratibu za kutoa mikopo mingine yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 500 (sawa na shilingi Trilioni 1 na Bilioni 389) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa wakati Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo (Trade and Development Bank – TDB), Admassu Tadese.

Rais Magufuli amemshukuru Bw. Tadese kwa mchango mkubwa unaotolewa na TDB kwa maendeleo ya Tanzania tena bila masharti nafuu na amemuomba Bw. Tadese kuongeza mikopo zaidi itakayosaidia utekelezaji wa miradi muhimu na yenye manufaa ya muda mrefu kama vile ujenzi wa reli, mradi wa kuzalisha megawati 359 za umeme katika mto Ruhuji Mkoani Njombe na miradi ya ujenzi wa miundombinu muhimu.

Kwa upande wake Bw. Tadese amesema TDB imekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango na ameelezea kufurahishwa na mazungumzo yake na Rais Magufuli ambapo ameahidi kuwa benki hiyo itazingatia ombi la kuongeza fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Tanzania ukiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railway-SGR) katika kipande cha kuanzia Dodoma kuelekea Kanda ya Ziwa na kanda ya Magharibi ambako itaunganisha na nchi jirani zisizokuwa na bahari.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James.

Swahilinews
 
.Mbona mnatuchanganya?bosi wenu anahubili mnajenga kwa pesa zenu za ndani na hamhitaji2 msaada kutoka kwa MABEBELU,mala leo mnasema mkopo tena kutoka Kwa walewale mnaowaita Mbuzi dume aliyekomaa🦄,sasa tuwaeleweje?au mnala umeyumba
 
Mabeberu hawatuachii, kulikoni?

Na Dege letu waliachie basi sio wanatupa kwa mkono huu na kuchukua kwa mkono ule.
 
Mbuzi dume huyu hapa
.Mbona mnatuchanganya?bosi wenu anahubili mnajenga kwa pesa zenu za ndani na hamhitaji2 msaada kutoka kwa MABEBELU,mala leo mnasema mkopo tena kutoka Kwa walewale mnaowaita Mbuzi dume aliyekomaa,sasa tuwaeleweje?au mnala umeyumba
tapatalk_1574414219590.jpeg
 
Kudadeeeeki yamekua haya yakukopa tena??? si tunajenga kwa kodi zetu???
 
Wameanzakujileta wenyewe kutoa pesa baada ya kuonajpm anaweza , nabado watazileta sana maana wamesubiri kukwama wanaona kazi inaendetea tu hongera jpm
 
Mikopo ya mashariti nafuu ni muhimu kutoka nje inaleta ahueni kwa vyanzo vya ndani.
 
Afu akisimama kuhutubia wajinga anawqambia kwa feza sio fedha za ndani.
Sisi ni matajiriiii
Tumechezewa aana
 
Pesa Zipo!!
Tembeeni Kifua Mbele Tupo Kwenye Light Track
Wanaotumiwa Na Mabeberu Hawatapenda Haya
 
Huu usanii wa karne. Deni la nchi limeongezeka kwa sababu gani kama mlikuwa hamkopi? Au ndo chanzo cha kumuondoa CAG ili muendeleze uongo juu yetu make upikwaji wa data tuutegemee kwa sana tu. Hainatofauti na Baba anayejinasibu kwa watoto wake kuwa sasa hivi tuna maendeleo huku nyumbani unapikwa uji badala ya chakula. Sasa hapo definition ya maendeleo wakati watu wanakunywa uji wanalaa ndo nini? Endeleeni na ngonjera zenu sisi waelewa tunaendelea kuhesabu siku tutakuja kuelewana tu.
 
unajitoa ufahamu au.fedha yetu ya ndani nikutoka dar mpka makotopora 743 km ambayo reli imeshaanza kujengwa na sasa imeshafika 75%.hawakusema reli yote tutajenga wenyewe hapana.saiz wale waliokataa kutupa mkopo pale mwanzo ndio wameanza kujitokeza baada ya kuona tumeanza wenyewe.mikopo duniani kote ni biashara km biashara nyingine nakupa 100 utanilipa 150 kwa hiyo mtu hawezi kuwekeza au kutoa mkopo ambapo anamashaka km mradi wenyewe utautekeleza na kuleta faida?
 
Back
Top Bottom