Tanzania yapanda nafasi 4 ya viwango vya soka vya dunia FIFA

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepanda katika list ya viwango vya soka vya dunia FIFA iliyotolewa hii leo Alhamisi Oktoba 25, 2018

Katika viwango hivyo vilivyotolewa na FIFA, Taifa Stars imepanda nafasi nne zaidi hadi kufikia 136 kutoka nafasi ya 140 kwa mwezi uliopita.

Uganda iliyo nafasi ya 79 inaongoza kwa nchi za Afrika Mashabiki ikifuatiwa na nchi ya Kenya iliyo katika nafasi ya 105 huku nchi ya Rwanda ikishika nafasi ya 138 na nchi ya Burundi ipo nafasi ya 142.

Aidha, Ubelgiji imefanikiwa kuiondoa Ufaransa katika nafasi ya kwanza huku Nigeria ikiongoza katika bara la Afrika ikiwa katika nafasi ya 44 ya viwango vya soka vya dunia vya FIFA.

IMG_20181025_152605.jpeg
 
Dah bado tuna safari ndefu mno. Ukifikiria huo mlima kupanda kufikia huko juu..Unapata presha Unakufa
 
Huko chini ya mia huko wala hakuna mshawasha...kushuka na kupanda hakuna tofauti yoyote. Tunawasubiri huku juu ya mia tuanze kuwapa kongole.
 
Hapo juu tayari akina Hazard wamefanikiwa vilivyo kufurusha akina Mbappe
 
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepanda katika list ya viwango vya soka vya dunia FIFA iliyotolewa hii leo Alhamisi Oktoba 25, 2018

Katika viwango hivyo vilivyotolewa na FIFA, Taifa Stars imepanda nafasi nne zaidi hadi kufikia 136 kutoka nafasi ya 140 kwa mwezi uliopita.

Uganda iliyo nafasi ya 79 inaongoza kwa nchi za Afrika Mashabiki ikifuatiwa na nchi ya Kenya iliyo katika nafasi ya 105 huku nchi ya Rwanda ikishika nafasi ya 138 na nchi ya Burundi ipo nafasi ya 142.

Aidha, Ubelgiji imefanikiwa kuiondoa Ufaransa katika nafasi ya kwanza huku Nigeria ikiongoza katika bara la Afrika ikiwa katika nafasi ya 44 ya viwango vya soka vya dunia vya FIFA.

View attachment 910453
Kwenye ndumba bado hatuna mpinzani... Tumejikita kileleni... Tumesimamia ukucha
IMG-20181024-WA0049.jpeg
 
Brazil ni muda sasa wamezoea sehemu yao
Huko chini ya mia huko wala hakuna mshawasha...kushuka na kupanda hakuna tofauti yoyote. Tunawasubiri huku juu ya mia tuanze kuwapa kongole.
IMG_20181025_173916_038.jpeg
 
Back
Top Bottom