Tanzania yaongozwa na Katiba ya CCM au Katiba ya nchi? Kikwete aiogopa CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yaongozwa na Katiba ya CCM au Katiba ya nchi? Kikwete aiogopa CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Ni jambo lililonishangaza Kikwete kuitisha kikao cha Chama kwa ajili ya kujadili na kuomba ridhaa yao kufanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri. Kwa hali ilivyo inaelekea hata yaliyotokea kwa akina Jairo na wengineo aliogopa kuchukua hatua kwa kuogopa chama chake.

  Serikali huongozwa na katiba ya nchi si katiba ya Chama, sasa Rais anapoomba ridhaa ya chama kufanya mabadiliko serikalini ina maanisha nchi inaongozwa na katiba ya Chama badala ya Katiba ya nchi?
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kusema kweli hii ni aibu kubwa sana kwa kiongozi wetu kuweka kikao cha chama ktk maamuzi ambayo yako chini ya mamlaka yake. Hata kama wamekaa kikao hiki basi wangeifanya siri ikaonekana kama ushauri tu, lakini sii kusikia ati kikao cha CC kimekubaliana naye kubadilisha baraza la mawaziri mbele ya maamuzi ambayo alitakiwa yeye kama rais wa nchi kuyafanya.

  Ama kweli leo JK ametumia akili za ngong'ota badala ya mbayuwayu kama madai yake siku zote...
   
 3. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Masuala ya serikali yanajadiliwa na chama , na chama kinatoa tamko juu ya nin wameazimia. wakat tamko lilitakiwa kutolewa na pinda au makamu wa rais
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Binafsi ni jambo ambalo limenishangaza baada ya kusikia tangazo hilo na Katibu Mwenezi wa CCM kwamba CCM imekuwa na kikao na Rais kuamua mabadiliko ya Baraza la mawaziri, ni shauri zito linalokanganya.

  Ni katiba gani ambayo Kikwete anaitumia kuongoza nchi? Katiba ya Tanzania haielezi po pote kwamba masuala ya uongozi wa nchi chama fulani kitoe uamuzi wakati kuna katiba na waandamizi serikalini ambao ni jukumu lao kisheria pamoja na usimamizi wa kisheria wa Mwanasheria Mkuu wa serikali.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Badala ya kusikia tamko la Mwanasheria wa serikali kumshauri Raisi masuala ya utawala wa kisheria sasa Rais anashauriwa na Chama na kuweka kando vyombo ambavyo vimeainishwa kikataba kutumika katika kushauri.
   
 6. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Jibu ni ndio na imekuwa hivyo tangia mwaka 1977.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama jibu ni ndiyo kwa nini Rais anaapa kuongoza nchi kwa kadiri ya katiba ya nchi? Kwa nini asiape kufuata katiba ya Chama?
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mchambuzi,
  UInataka kunambia Nyerere alipokuwa akivunja baraza la mawaziri alifanya vikao vya chama na kushauriwa alivunje?.. sidhani mkuu wangu hili itabidi nilifanyie utafiti maana linaondoa maana ya katiba na mamlaka ya rais ikiwa chama ndicho kinaamua, Hivi unataka kunambia hata anapochagua mawaziri huwa kuna kikao cha chama kinachomchagulia mawaziri? maana kama wanaweza kuvunja basi wanaweza pia kumchagulia..
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Haya ni maamuzi ya aibu ambayo Rais yeyote wa Tanzania amewahi yafanya! Hatuna kiongozi hapo Ikulu. Nawaomba Watanzania wote wazalendo tupigane pamoja kurudisha heshima ya nchi hii!
   
 10. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mkandara,
  nimetoa jibu hilo kutokana na experience yangu, atleast kupitia literature mbali mbali juu ya jinsi gani nchi hii imekuwa inangozwa, especially jinsi gani katika kipindi chote cha 1977 hadi miaka ya hivi karibuni, mhimili wa 'Rais' umekuwa unaburuza mihimili mingine ya bunge na mahakama ikibidi. Hii ilichangiwa zaidi na 'CHAMA KUSHIKA HATAMU", ambapo watumishi wote wa serikali na mashirika ya umma ilikuwa ni lazima wawe kwanza ni wanachama hai wa chama cha mapinduzi. Nadhani pia unakumbuka kwamba ilikuwa ni jambola kawaida kukuta matawi ya CCM kwenye ofisi zote zenye shughuli za serikali/umma.

  Pia nikuulize - inakuwaje Maalim Seif na Hamad Rashid iliwezekana kuwafukuza kutoka katika nafasi zao za uongozi ndani ya chama cha mapinduzi - unaibu waziri, waziri kiongozi (hasa ubunge) lakini hivi sasa, chini ya katiba ile ile ya mwaka 1977, hilo limeshindikana na halitawezekana (Kafulila & Hamad Rashid) ? Kwanini ilikuwa rahisi sana kumtoa waziri mkuu Malecela mwaka 1994 kwa katiba ile ile ya 1977 lakini leo hii kumtoa Pinda inakuwa vigumu? Yote ni kwa sababu, kwa maslahi ya chama inawezekana, lakini kwa mujibu wa katiba ya nchi, sio rahisi hivyo.

  Sina uhakika kama Rais huwa anakaa na chama chake kuchagua mawaziri lakini nachojua ni kwamba mawaziri wote huchaguliwa kwa kuangalia maslahi ya chama.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Apr 28, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wakuu mlikuwa mnafikiri dhana ya kuwa "Chama Tawala" maana yake nini?
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280

  ....Ni msanii huyu wa hali juu si ajabu hata hajui mamlaka makubwa aliyokuwa nayo kama Rais wa nchi labda alidhani baada ya shinikizo la Wabunge kuhusu utendaji wa Baraza la Mawaziri alilazimika kupata ridhaa ya kamati kuu ili aweze kufanya mabadiliko ya mawaziri. Mie niliposoma hiyo kwamba aliitisha kikao cha ghafla cha kamati kuu na wamepma ridhaa ya kufanya mabadiliko nikabaki nimepigwa mshangao wa hali ya juu. Je, kamati kuu isingempa ridhaa baraza la mawaziri lingebaki kama lilivyo!?
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unachojadili ni behind the screen. Ni dhahiri Rais anayeongoza atachagua cabinet yake kutoka chama chake, na ridhaa yake tu kuteua cabinet member nje ya chama chake. Hali hiyo haiashirii kwamba katiba ya chama tawala ndiyo inayoongoza nchi, bali cabinet member wa chama ndio wanaoongoza nchi kwa kutumia katiba ya nchi si katiba ya chama.

  Rais pamoja na cabinet yake ya serikali wanaweza kuwa viongozi wa chama, lakini ni viongozi wa serikali inayotawala nchi nzima bila kujali itikadi zao za kichama. Ndio maana utekelezaji wa sera Rais yuko tayari kutekeleza hata sera za wapinzani anapoona inahitajika kufanya hivyo kwa manufaa ya nchi kama ilivyotokea Kikwete kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chadema kutokana na ukweli kwamba ni rais wa wote bila kujali itikadi za kichama.

  Pamoja na historia ya nchi hii kwamba tumetokea kuwa na chama kimoja cha siasa, hii haikuwa na maana kwamba katiba ya chama ndiyo ilikuwa inaongoza nchi licha ya kauli mbiu ya chama kushika hatamu za uongozi, bali chama kilikuwa kinawafua wanachama kuongoza nchi ili wawe na weledi katika utendaji mzuri serikalini. Hii ya kwamba serikali sasa inaitisha kikao cha chama kujadili mabadiliko ya baraza la mawaziri ni jambo jipya na lisilokubalika katika mfumo wa utawala unaofuata sheria na katiba ya nchi.


  Vinginevyo hatuna sababu ya kuwa na katiba ya nchi ila kila chama kinachoshika dola kifuate katiba ya chama chake; Je, nchi itakuwaje?
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Huko ni kutapatapa kwao kuizima hoja ionekane ni ya chama chao sio kwamba imeasisiwa na CDM...ndio maana wanahaha kuibaka hiyo ajenda ya uwajibikaji!!kumbuka alishasema upepo.......(Rais wa matukio)na upepo..
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ina maana kauli ya kusema "ni upepo unaovuma kwa muda" alikuwa bado hajapima speed ya upepo, kwa sasa baada ya kushtukia unabadilika kuwa kimbunga ameshtuka na kuanza kujihami kwa kuitisha kikao cha Chama?

  Kitendo hicho ni dhahiri amedharau mhimili mmojawapo wa serikali ambao ni bunge lenye dhamana ya kufuatilia utendaji wa serikali na kuishauri serikali, na sasa Kikwete anageukia chama ambacho si mhimili wa kuongoza nchi.
   
 16. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hukumsikia alivyosema wakati wa mabadiliko ya mswada wa katiba mpya akibadili wenzake hawatamwelewa, he is weak indeed, hajui kama yeye ni rais.
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo unataka kutuambia rais anaongoza kwa mazoea? hapana, kumbuka mwaka 1977 tulikuwa chini ya chama kimoja kama bado una mawazo hayo basi yamepitwa na wakati.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nimeelewa sababu za kuogopa na kukwepa debate ya kupima presidential candidate katika uchaguzi mkuu uliopita, naamani akipambanishwa kwa hoja za candidates wengine angebwagwa vibaya, anajua udhaifu wake.
   
 19. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hivi mbona tunapenda kuchuja taarifa na kubaki na tunazozipenda? kilichofikishwa kwenye CC ni taarifa ya wabunge wa CCM iliyopendekeza mawaziri wajiuzulu. CC imebariki azimio hilo. simple & clear. hayo ya kuongoza kwa kutumia katiba ya ccm ni tafsiri potofu.
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mkuu feedback hapa umemaliza kila kitu
   
Loading...