Tanzania yaongoza SADC kwa unafuu wa tozo za data

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1553887110501.png


TANZANIA inaongoza kwa kuwa na tozo zenye gharama nafuu kwenye matumizi ya data pamoja na maudhui katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), imeelezwa. Hali hiyo inatokana na uwepo wa Mkongo wa Taifa ambao umesaidia kupunguza gharama za mawasiliano ambapo kwa sasa watumiaji wa data hutozwa Sh 10 kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine.

Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Atashasta Nditiye wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa uliokutanisha Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano (CRASA).

Nditiye alisema katika nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na SADC, Tanzania ndio huduma zake za data zipo chini. “Mkongo wa Taifa ambao upo karibu mikoa yote ndio umesaidia kupunguza gharama na nchi kutoka nje wamekuwa wakija kujifunza namna ya uendeshaji wake,” alisema Nditiye.

Aliongeza kuwa wananchi wanaweza kuwasiliana kwa gharama nafuu na kwamba malipo wanayoyafanya ni kwa ajili ya kuchangia katika uwekezaji uliofanyika. Pia alisema gharama wanazotozwa waendeshaji wa maudhui na blogs zipo chini na kwamba zinaendana na usalama wa Watanzania.

“Gharama tunazotoza ni kwa sababu tunahitaji watu wasivuruge maadili ya Tanzania bali wajifunze matumizi bora ya mawasiliano,” alisisitiza. Naibu Waziri huyo alisema wanashirikiana na jumuiya hiyo katika masuala ya uhalifu wa mtandao, utangazaji wa luninga na redio na kuhakikisha tozo za mawasiliano zinakuwa nafuu ili wananchi wanufaike.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba alisema wamekutana kwa lengo la kupitia changamoto na maendeleo ya mawasiliano katika jumuiya hiyo. Kilaba alisema malengo ya mkutano huo, pamoja na mambo mengine watajadiliana namna ya kuweka uwiano katika tozo na kushughulikia masuala ya mawasiliano kwa ujumla.

“Tunataka kuwa na nchi ya viwanda, hivyo ni lazima mawasiliano ya Tehama yawepo na yawe salama kuanzia miundombinu, mitandao na watumiaji,” alisema Kilaba. Aliongeza kuwa kwa kuhakikisha usalama wa mitandao na watumiaji wanahakikisha kuwa wanawatambua watumiaji wote wa simu kwa kuwasajili. Kilaba alieleza kuwa si rahisi kwa jumuiya hiyo kuwa na kanuni moja ya kudhibiti mawasiliano badala yake wanaweka miongozo ambayo kila nchi wanachama wanapaswa kuifuata.

“Bado kuna changamoto ya elimu kwa watumiaji wa mawasiliano nchini kwani wengi hawajui namna ya kutumia simu zao hivyo hujikuta wakiingia kwenye matumizi mabaya kwa kutuma picha au video zisizofaa bila wenyewe kujua. Hivyo, tunaomba kila mtu ajue matumizi ya simu kabla ya kuanzia kutumia hii itasaidia kupunguza makosa,” alifafanua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom