Tanzania yaongoza SADC, Africa Mashariki uzalishaji viwandani

Bei Mbaya

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
2,262
843
kwenye mkutano wa CTI uliofanyika jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na wadau wa viwanda na Waziri wa uwezeshaji Bi. Mary Nagu imetangazwa Tanzania kuongoza kwa kasi ya ukuaji wa uzalishaji wa bidhaa za viwandani mbali na nchi kukabiliwa na tatizo la mgao wa umeme kwa muda mrefu sasa

'utafiti huo unaonyesha kwa kipindi cha mwaka mmoja kufikia sasa ukuaji wa bidhaa viwandani umefikia asilimia nane sawa na Msumbiji. Ni Africa kusini kwa sasa nchi ambayo inazalisha bidhaa nyingi katika eneo la kusini mwa Africa' alisema mwenyekiti CTI Bw. Mosha

aidha waziri wa uwezeshaji Bi. Nagu aliwaeleza waliohudhuria mkutano huo mgao wa umeme utakuwa historia kwa mikakati iliyowekwa na serikali
 
Hii dunia haiishi viroja....Tanzania inaongoza uzalishaji wa bidhaa za viwandani? Bidhaa zipi hizo jamani na viwanda gani hivyo?

Labda vile vya kule kwa ndugu zangu wa Tanga vya kutengeneza tunguli na hirizi
 
Acha porojo zako wewe,,,,,,south afrika unaiweka wapi?????si ipo sadc????
 
mbona uchumi wa nchi nyingi maskini unakuwa kuliko wa ulaya na Amerika
 
Na Kenya jee. Walalahoi watakuwa ndio wameandaa hiyo report alosoma Mama Nagu.
 
Mleta mada, tafadhali fafanua; Tanzania imeongoza kwa ukuaji wa uzalishaji wa bidhaa viwandani au imeongoza kwa uzalishaji wa bidhaa viwandani? Bado haiingii akilini, Ni viwanda vingapi vpya vinaanzishwa Tanzania kila mwaka, ukitoa inavyofungwa kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali! Unaweza kuweka figa hapa! maana naona umeongea juujuu tu; Leta chanzo atleast, maana huenda mimi au wewe tunashindwa kutafsiri ujumbe!
 
Acha porojo zako wewe,,,,,,south afrika unaiweka wapi?????si ipo sadc????

South Africa na nchi nyingi ukanda huu zinazalisha kwa wingi kwa mwaka kulinganisha na Tanzania, lakini growth rate ya uzalishaji yao ipo chini
 
Mleta mada, tafadhali fafanua; Tanzania imeongoza kwa ukuaji wa uzalishaji wa bidhaa viwandani au imeongoza kwa uzalishaji wa bidhaa viwandani? Bado haiingii akilini, Ni viwanda vingapi vpya vinaanzishwa Tanzania kila mwaka, ukitoa inavyofungwa kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali! Unaweza kuweka figa hapa! maana naona umeongea juujuu tu; Leta chanzo atleast, maana huenda mimi au wewe tunashindwa kutafsiri ujumbe!

imeongoza kwa ukuaji wa uzalishaji na sio uzalishaji, soma paragrafu ya kwanza ya thread inavyoeleza
 
Hizi habari wakawapatie magazeti ya udaku yatawaamini, huku wanajisumbua bure

mbona usomaji wao unafanana na wa kwako, mnatawaliwa na hisia

soma, elewa kilichoandikwa kwenye paragrafu ya kwanza hasa sentesi bolded
 
usitudanganye sisi sio bongolala sema tunaongoza kwa importation ya bidhaa
 
Back
Top Bottom