Tanzania yaongoza Kikao cha Baraza la Uendeshaji la Umoja wa Posta Duniani

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Kikao cha Baraza la Uendeshaji la Umoja wa Posta Duniani (Universal Postal Union Postal Operations Council) kimeendelea leo tarehe 24 Novemba,2021 jijini Berne,Uswis ambapo Tanzania Imeongoza kikao cha Kamati namba mbili ya Baraza hilo inayohusu Huduma za Posta na Biashara Mtandao (Physical Services and E-Commerce) ikiwa ni mwenyekiti mwenza pamoja na nchi ya Uswis.

Kikao hiki ni cha kwanza kufanyika Makao Makuu ya Umoja wa Posta Duniani jijini Berne,Uswis baada ya Mkutano Mkuu wa 27 wa Umoja huo uliofafanyika jijini Abidjan,Ivory Coast mwezi wa Agosti 2021 ambapo Tanzania ilichaguliwa kuwa mjumbe wa mabaraza yote mawili ya maamuzi ya Umoja wa Posta Duniani yaani Baraza la Utawala na lile ya Uendeshaji (Council of Administration and the Postal Operations Council of Universal Postal Union).

Baada ya Uchaguzi huo ambao Tanzania iliweka historia ya kushinda Mabaraza yote mawili kwa wakati mmoja,ilipewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti mwenza wa kamati namba mbili ya Baraza la Uendeshaji la Umoja huo.

Bwana Constantine John Kasese, Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji wa Shirika la Posta Tanzania ameongoza kikao hicho leo pamoja na mwenyekiti mwenza Bwana Bjorn Arni wa Posta ya Uswis.

Katika kikao hicho Bwana Kasese aliongoza ajenda iliyovutia mjadala mzito ambayo ilihusisha Pendekezo la kushughulikia masuala ya Majanga asilia hasa linalohusisha janga la UVIKO-19 ambalo liliathiri huduma za vifurushi vya Posta.

Vikao vya mabaraza hayo ndiyo yanahusika na kufanya maamuzi ya msingi kwa ajili ya Uendeshaji wa shughuli za Posta duniani ambapo wanachama wake wapatao nchi 192 huguswa na maamuzi yanayofanyika kupitia mfumo huu wa pamoja (Postal office as single village).

Tanzania inashiriki kwenye vikao vya mabaraza hayo ambavyo vimeanza jana tarehe 22 hadi 26 Novemba yatakapohitimisha vikao vyake. Katika vikao hivyo Ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Mhandisi Clarence Ichwekeleza, Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ; wengine ni Constantine Kasese, Kaimu Meneja Mkuu, Uendeshaji Biashara Shirika la Posta Tanzania; Cecilia Mkoba, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Fedha kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dorosela Rugaiyamu Afisa TEHAMA mwandamizi wizarani na Elia P.K.Madulesi, Mkuu wa Mawasiliano na Mambo ya Posta Kimataifa kutoka Shirika la Posta Tanzania.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania.
24 Novemba, 2021.
 
TANZANIA YAONGOZA KIKAO CHA KAMATI NAMBA MBILI YA BARAZA LA UENDESHAJI LA UMOJA WA POSTA DUNIANI (UPU)

Bern, Uswis

IMG-20211125-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom