Tanzania yaongoza duniani kwa utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia simu

maryedow

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
257
88
1.JPG

Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.

Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng. James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

“Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” alisema.

Kuhusu mkutano huo wa kimataifa ulioshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa ITU, alisema umelenga kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika sehemu ambazo hazifikiwi na huduma hiyo.

“Mkutano huu unasimamiwa na shirika la mawasiliano duniani ITC ambao umelenga kujadili namna ya kutumia mitandao ya simu kupeleka huduma za kifedha katika maeneo yasiyofikiwa na huduma za kifedha hasa ambako hakuna mabenki. Mkutano huu nchi imeamua kuuanda kwa ushirikiano wa TCRA na BOT, ” alisema.

Naye Gavana Mkuu wa BOT Profesa Benno Ndulu alisema hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu takribani watanzania milioni 21.5 nchi nzima wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.

“Hadi kufikia Julai, 2016 watanzania 21.5 milioni wanatumia mitandao ya simu walau mara 1 kwa mwezi idadi hii ni kubwa na kwamba inaonesha sekta hii inakua kwa kasi,” alisema.

Profesa Ndulu alisema kuwa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imesaidia kukuza uchumi wa nchi.

“Malipo ya fedha kwa njia ya simu yanasaidia kupunguza gharama hivyo na kuwa kichochea cha maendeleo, sasa hivi wafanyakazi, wakulima, wanaotumia huduma za bima, wanaonunua bidhaa hulipa kwa Kutumia simu za mkononi hususani kwamba muda ndio muhimu,” alisema.

Aliongeza kuwa “Mitandao ya simu haiathiri huduma za kibenki, na benki wamechangamkia kutumia mitandao kufikia wateja wao, hutumia mawakala kufungulia account, mitandao hii husaidia benki kufikia wateja kote nchini, woga huo umepungua kwa sasa,”

=======
Moderator:

Unaweza kusoma zaidi - Kenya overtaken by Tanzania in mobile money transfer
 
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.

Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng. James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Mkuu wangu Kilaba (najua nawe ni member humu JF), hizi takwimu za Tanzania kuwa kinara zipo katika Public domain?

Tovuti ya BoT ina data za mwaka 2013 (ingawa tupo 2016) na nashindwa kuelewa wapi kama mwananchi nitapata publication hii nione tukiwa tumewapiku Kenya.

Najiuliza, BoT hawana kitengo kinachohusika na mawasiliano kwa Umma? Kinafanya kazi gani?

Hiki ndo hutokea ukitembelea tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania:

Screen Shot 2016-09-20 at 11.05.51.png

Na hapa ndo wameajiri wataalamu wabobezi wa IT!

Lakini, tovuti yenyewe ina data hizi:

Screen Shot 2016-09-20 at 11.11.08.png

“Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” alisema.
Pale mtaalamu anapoongea kisiasa ndo mtu unashindwa kuelewa tunakoelekea! Labda mimi ndo nina uelewa mdogo?!

Kuhusu mkutano huo wa kimataifa ulioshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa ITU, alisema umelenga kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika sehemu ambazo hazifikiwi na huduma hiyo.

Naye Gavana Mkuu wa BOT Profesa Benno Ndulu alisema hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu takribani watanzania milioni 21.5 nchi nzima wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.

“Hadi kufikia Julai, 2016 watanzania 21.5 milioni wanatumia mitandao ya simu walau mara 1 kwa mwezi idadi hii ni kubwa na kwamba inaonesha sekta hii inakua kwa kasi,” alisema.
Prof. wapi taarifa hizi kwa umma wa watanzania? Wapi takwimu? Si mmeikubali OGP? Wekeni vitu public, acheni siasa bana.

Profesa Ndulu alisema kuwa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imesaidia kukuza uchumi wa nchi.
Takwimu tafadhali? Si maneno matupu?

“Malipo ya fedha kwa njia ya simu yanasaidia kupunguza gharama hivyo na kuwa kichochea cha maendeleo, sasa hivi wafanyakazi, wakulima, wanaotumia huduma za bima, wanaonunua bidhaa hulipa kwa Kutumia simu za mkononi hususani kwamba muda ndio muhimu,” alisema.
Yanapunguza gharama zipi? Wananchi wanaridhika na makato mnayowakata ambayo kwa sasa ni maradufu na wala hamkutaka muafaka nao?

BTW, hivi mnajua watanzania wanaibiwa sana na hawajui hata pa kukimbilia? Elimu kwa umma ni muhimu sana. Sikatai kuwa kuna mafanikio ila tunapoyaongelea mafanikio tuziangalie kwa ukaribu changamoto na ziwe addressed!

Aliongeza kuwa “Mitandao ya simu haiathiri huduma za kibenki, na benki wamechangamkia kutumia mitandao kufikia wateja wao, hutumia mawakala kufungulia account, mitandao hii husaidia benki kufikia wateja kote nchini, woga huo umepungua kwa sasa,”
Which means woga ulikuwepo na bado upo lakini 'umepungua'. Hii haina tofauti ya Traditional Media kuogopa ujio wa social media na hata kuzi-discredit kwa nguvu badala ya kuona fursa ndani yake na kuitumia.

Lakini, mnajua kuwa ndo money laundering inafanyika kirahisi? Mnaweza kutuhakikisha kuwa mnaweza kudhibiti utakatishaji fedha kwa mabadiliko haya ya teknolojia?
 
atupe takwimu za kidunia/za kimataifa sio kusema ''ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,”
 
Mida hii nimemtumia taarifa hii jamaa yangu mmoja anayefanya kazi katika mtandao wa kijamii mmoja wa kimataifa huko nje amecheka sana kisha kaniambia pia kwamba Tanzania katika data za kidunia ndiyo nchi ya kwanza kwa wateja wake kuibiwa kupitia huduma hiyo hiyo na ile ya muda wa maongezi.

Kasema ni kutokana na faida ya kijanja janja wanayopata makampuni ya mawasiliano ndiyo maana wanatumia kila njia kupenyeza aina hiyo ya huduma kwa wananchi ili wavune vizuri, na pili ni kutokana na kushindwa kwa mabenki yetu ambayo ndiyo wajibu wake kutoa huduma hiyo kwa gharama ndogo na kwa haraka.
 
atupe takwimu za kidunia/za kimataifa sio kusema ''ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,”

ILA NIKWELI HAYA MA MPESA,TIGO PESA,AIRTEL MONEY YAMESAIDIA SANA KUCHANGAMUSHA UCHUMI NAKUPUNGUZA SHIDA.NCHI NYINGI ZA KIAFRIKA HAWANA LABDA KENYA..KAMA KUNAMTU ANAJUA BASI ATUELEZE NCHI ZINGINE WALIO KAMA SISI NA KENYA
 
Tuseme Ndio nchi ya kwanza ulimwenguni.
Inamaana hana uwakika c ndiyo?
Bado Hana data zinazompa uwakika? Basi angevuta subra tu.
 
Ee mbona Wakenya nao wamedai hivyohivyo majuzi tuu hata imkampelekea muasisi wa Facebook bwana Mark Zuckerberg kufanya ziara kwa wachapa codes wa Nairobi kwa kigezo hicho?
Hawajaona.. wangeona wangesema tumekuwa wa pili. Cooked data
 
Benki za Tanzania zijichunguze zaidi na mifumo yao ya kiimla.

Haiingii akilini mifumo ya simu banking imukopeshe mtu kwa kigezo cha laini tu afu bank wanaleta longolongo kwenye mikopo inayoonyesha mpaka biashara zilipo.
 
alafu bado hamtaki kukatwa kodi sijui mnadhani hayo maendeleo yatadondoka kutoka mbinguni kama mvua
 
Benki za Tanzania zijichunguze zaidi na mifumo yao ya kiimla.

Haiingii akilini mifumo ya simu banking imukopeshe mtu kwa kigezo cha laini tu afu bank wanaleta longolongo kwenye mikopo inayoonyesha mpaka biashara zilipo.
Hill nalo neno ndg ikiwa kwenye mitandao inawezekana kwa bank iwe ngumu.hakika kwenye mabenk Luna ulasimu sana tu
 
Hawajaona.. wangeona wangesema tumekuwa wa pili. Cooked data

Tumeona tukapotezea, back and forth huchosha wakati mwingine. Hii jambo tushajadili sana humu, Tanzanian customers have multiple mobile money accounts unlike Kenyans who only have a single account. In Tanzania, a single person will have an account in Vodacom, Tigo, Ezy Pesa and Aurtel Money while in Kenya somebody only has Safaricom's MPesa with a few customers having both MPesa and Airtel Money. In terms of total number of active accounts mmetushinda but kwa value of transaction tumewawacha mbali sana. Tanzania ina transact $5 billion per year na sisi tupo $40 billion per year.
Pitia kweny huu mjadala Kenya overtaken in mobile money transfer
 
Sasa unaleta taarifa za kupika una hata data!!
Mod na nyie taarifa za upotoshaji muwe mnaziondoa hapa zinafanya jukwaa linakuwa lakitapeli!!
 
Back
Top Bottom