RingaRinga
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 1,041
- 510
Je Watanzania wenzangu maoni na mitizamo inayoandikwa mitandaoni ndio mtizamo halisi wa Watanzania wote juu ya serikali yetu?
Zile methali zetu za 'miluzi mingi humpoteza mbwa' nadhani itaendelea kutuathiri kwa kipindi kirefu sana!
Wakati fulani tunashindwa hata kushtuka kuwa tunatumiwa na magenge yanayopambana na serikali kuiondoa kwenye agenda zake muhimu.
Tumekoswa uzalendo wa kuwatetea viongozi wetu na kuwakosoa kizalendo pale wanapokosea na kusahau mara moja jitihada kubwa na uthubutu wa hatari waliojivika kulitoa taifa hili kule lilikonasa.
Kuna jambo limeibuka la watu kutekwa na kupotea, limekuwa kama maigizo au series ambalo mimi naweza kusema linaweza kuwa linafanywa na yeyote kati ya hawa wafuatao:-
- Serikalikali yenyewe ( upstairs wakiwa wanajua kila kitu)
- Wapinzani wa serikali wakiwa ndani ya serikali ili kuipaka matope serikali.
-Wapinzani wa serikali nje ya serikali, na
-Wahalifu wengine wasio na uhusiano au wakiwa na uhusiano na makundi niliyoyataja hapo juu.
Mojawapo ya kundi lolote kati ya haya linaweza kuendesha tamithiliya za namna hii kwa malengo linayoyajua lenyewe
Si haki kuwashambulia viongozi wa serikali tu bila kuyashuku makundi mengine ambayo ni hatari zaidi hasa katika namna ambayo yanatambua kuwa hatuyawazii km yanaweza kuwa yanaendesha kampeni hatari kama hizi. Viongozi wetu ni binadamu pia, watakata tamaa kisha kesho yetu iwe mbaya zaidi. Mambo mengine tusiyo na uhakika nayo tuziachie mamlaka na Mungu mwenyewe.
Vyombo vyetu vya habari vimekuwa bize kusoma tabia za Watanzania kujua viwauzie habari za namna gani bila kujali vinajenga au vinabomoa ili mradi vimeuza.
Punde tutafaulu kuiangusha serikali yetu wenyewe na wanasiasa watakaofata watageuza siasa kama biashara kichaa ambayo hawana haja ya kujitoa mhanga kwa maswala nyeti yanayorudisha nyuma ustawi wa taifa letu.
Kisha tutarudi kulekule ambako
Hatutasikia tena gari zimekamatwa bandarini ktk makontena,
Hatutasikia tena habari za makontena elfu kadhaa yamebainika kupita bandarini bila kulipiwa ushuru,
Habari za udhibiti wa wafanyakazi hewa,
Udhibiti wa safari zisizo na tija,
Kufutwa kwa posho za vikao na zinginezo maeneo ya kazi
Kurejeshwa kwa nidham maeneo ya kazi
Vita dhidi ya madawa ya kulevya ambayo kwa watanzania wazalendo tusingesita kutoa ushirikiano wala tusingeona style iliyotumiwa ya kukusanya watuhumiwa wote kuwa ni udhalilishaji bali ni njia ya kuwasafisha wanaotuhumiwa bure na kuwadhibitisha wanaohusika.
Badala yake tumeamua kuwa bendera....
Wito wangu kwa viongoz wa serikali, mstoke katika ajenda zenu kwa ajili ya Tanzania njema ya kesho, hata Yesu alipata shida znazofanana na hizo.
Kipimo cha idadi ya Watanzania walionyuma yenu mtakiona 2020, MSITISHIKE na kampeni za wauza unga, mafisadi na wenzao waliojificha ktk uanasiasa, uandishi na usanii