Tanzania yangu nakupenda: Wanasiasa wanaojidai viongozi wanakudhalilisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yangu nakupenda: Wanasiasa wanaojidai viongozi wanakudhalilisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MsandoAlberto, Mar 18, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania,

  Nchi ya babu na bibi zangu. Nakupenda na kukutukuza.

  Ila nasikitika kwamba kumbukumbu nzuri na tamu kuhusu wewe ni wimbo na bendera yako.

  Vingine vyote nimevisahau. Madini, mito, milima, maziwa, misitu, hifadhi, viwanda, watu n.k. Vyote ni mali za wengine. Hakuna hata kimoja ambacho naweza kutembea kifua mbele nakujisifu kwamba ni changu au chetu.

  Kwa muda mrefu sasa wanasiasa wamejidai ni viongozi. Wanachofanya ni siasa na si kuongoza. Wangetuongoza tusingefikia hapa tulipo. Ahadi zao siku zote zilikuwa kulinda mali zako na kutuletea neema. Tuliahidiwa kupigana vita dhidi ya Maradhi, Umasikini na Ujinga siku nyingi sana. Nilikuwa sijazaliwa ila bibi na babu walinihadithia kabla hawajatangulia mbele ya haki. Mpaka leo hii vita haijaanza. Silaha zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili ya vita zimekwisha muda wake na muda na saa yoyote zitalipuka zenyewe. Hata hivyo haitakuwa jambo geni kwani kuna silaha nyingine zilikusanywa kwa ajili ya vita ambayo hatuijui zinalipuka zenyewe na kutuua. Sasa hivi wanao wengine wanaishi kwenye mahema.

  Tanzania, kama tungeanza vita dhidi ya maradhi wanao wengi wasingekimbilia Loliondo kwa Babu. Angalau Babu anatibu kwa imani. Tunapata matumaini lakini kwa bahati mbaya wengine wetu wanakufa wakati wanapata tiba. Wanafika huko kwa shida na tabu kuu. Wengine wamekufa baada ya magari yao kugongana uso kwa uso kwa sababu ya vumbi!! Hata lile tumaini dogo tunalopata muda mwingine linatuharakishia mauti. Babu anatibu magonjwa sugu ila hazuii ajali zitokanazo na uzembe au barabara mbovu.

  Tanzania, kama tungeanza vita dhidi ya umasikini mapema basi wengi wangefika Loliondo kupata tiba ili kufidia kuchelewa kwetu kuanza vita dhidi ya maradhi. maelfu wanalia vijijini. Hawana uwezo wa kufika Loliondo. Tunafanyaje?

  Bado sisi ni masikini wa kutupwa. Hakuna anayetuthamini tena. Siku zote asiye na kitu hathaminiwi. Tukiongea tunaambiwa tunatishia amani na utulivu. Tukitembea tunaambiwa ni wazururaji, wezi, hatuna cha kufanya, wanafiki na maneno mengi ya kejeli na dharau.

  Eti tunaambiwa tunafadhiliwa na nchi fulani kuleta fujo. Hivi, inawezekanaje nikalipwa au kufadhiliwa ili niseme kwamba nina njaa, sina kazi, nchi yangu inauzwa, naibiwa, nadhalilishwa nk? Kwa nini nilipwe ili niijue hali yangu ya ufukara?

  Kama ningekuwa na kiongozi basi maneno hayo yasingesemwa. Kamwe kiongozi hawezi kuacha kazi za umma, akaenda kutumia chombo cha umma kuueleza umma kwamba 'chama fulani kinafadhiliwa na nchi fulani'......Ni kiongozi wa aina gani huyu kama sio mwanasiasa tu? hapo anafanya kazi yake, siasa.

  Tanzania, haya yote yanawezekana kwa sababu wanasiasa wanaamini kwamba kwa kutokuanzisha vita dhidi ya Ujinga basi sisi ni wajinga. hilo ndio kosa lao kubwa ambalo muda si mrefu litatuletea neema. Kwa njia moja au nyingine Mungu amewaruhusu walitende hilo kosa.

  Kwa kukosa kwetu elimu ya darasani (tumeipata ile ya shule na vyuo vya kata) wanadhani watatufanyia siasa milele kwa kisingizio wanatuongoza. tutawafundisha adabu. Sasa hatutaki tena kutumiwa. Kama ni AMANI ni yetu wote. Kama ni UTULIVU ni wetu wote.

  Tanzania, niruhusu nitubu na kukiri kwamba endapo nyoka ataingia ndani kwangu na kujificha kwenye mtungi wa kioo kisha nishindwe kumtoa, kuliko nirudi kulala atoke aning'ate nitauvunja huo mtungi nimuue. Nadhani nitakuwa salama zaidi.

  Nisipofanya hivyo sitalala kwa amani, na sitakuwa salama. Mwenzake atamfuata na wataweka makazi huku wakizaliana kwa imani kwamba sitathubutu kuuvunja mtungi wangu wa kioo. Wataendelea kufurahia ulaini wa kioo pamoja na joto la ndani mwangu na muda wote watakuwa kazi yao ni kujamiiana ili waongezeke huku mimi nikiendelea kukaa macho na wasiwasi tele kuhusu uhai wangu. Sitavumilia. Sivumilii tena.

  Tumewachoka wanasiasa. Sasa tunataka tupate viongozi. Tunataka kuikomboa nchi yetu kutoka mikononi mwao. Hatutaki ahadi zao tena. Ni za muda mrefu na zitalipuka na kuleta madhara zaidi tukiwaendekeza.

  Na vile vitoto vya nyoka vinavyojidai kuandamana eti kupongeza hotuba baada ya kuona kwamba hakuna maendeleo ya kupongeza tutaviteketeza pamoja na mtungi. Vinakimbilia kujificha ndani ya mtungi pamoja na mijoka mikubwa. Wote hawatasalimika. Vioo vya mtungi na marungu yetu vitawawahusu.

  Tanzania, nakupenda. Ila kama Mungu atakupenda zaidi ahadi zake zitimizwe.
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Kwanza nikupe pole.
  Inaonekana ulinifahamu vyema katika ule ushauri kule ulipoaga.

  MsandoAlberto umenifanya nicheke ingawaje uliyoyaandika yanasikitisha.

  Lakini ni vizuri "Utubu" na sote tutubu kwa sababu tumeisahau nchi ya babu na bibi zetu.

  Si unafahamu nchi ya babu na bibi zetu haikuitwa Tanzania?

  Kwa hiyo sisi tunaipenda nchi nyengine kabisa. Nchi ya kufikirika.

  Ukiwauliza wazanzibari watakupa jibu zuri tu. Waulize Tanzania kuna nchi ngapi?
  Watakwambia rudi kwenye mkataba wa Muungano utazitambua.

  kwa hiyo ,kweli tutubu kwani tusipotubu tunaelekea pabaya. Miaka 47 sasa imepita na ugumu unazidi sio kwamba unapungua.

  Safari yetu ni refu lakini kaza buti. Ukiweza kugundua "kiini macho" hichi basi ndio mwanzo wa safari.
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, babu na bibi zetu walikuwa na Tanganyika.

  Unakumbuka somo la Geografia na Historia? Siasa? Gone are the days when a thought of our country gave us so much inner satisfaction. Siku wimbo wa Taifa ulipowekewa neno CHADEMA nilishindwa kwa dakika kadhaa kujua cha kufanya. Ilikuwa ni kwenye viwanja vya NMC Arusha siku ya kuwaaga marehemu waliouwawa na polisi.

  Mpaka leo natafakari sana. Nikikaa na watoto wangu nawajaribu kuwaambia tuimbe wimbo wa taifa. Wanang'ata maneno. Shuleni wanafundishwa nyimbo za kizungu na za kwenye birthday!

  Kwa sasa mimi mwenyewe sipati nafasi ya kuimba wimbo wa taifa. Mwaka mzima unaweza kuisha sijausikia wala kuuimba. Taratibu mapenzi kwa nchi yetu yametoweka, uzalendo umeisha. Ubinafsi ndio umechukua nafasi.

  Ni lazima hatua zichukuliwe kurudisha heshima ya nchi yetu. Tuheshimu wimbo na bendera yetu. Wanasiasa watuheshimu sisi wananchi. Tupate Viongozi.
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Msando post yako imetangulia mbele yangu......

  Nimewaza sana leo, lakini hata jana na juzi...Hii nchi iko wapi na ni wapi tunakoenda?? Hakika mbele ni giza totoro na sio kwamba tulipo nuru ipo, la hasha ni giza nene, naam kiza kinene sana

  Watoto wetu leo watakuwaje kesho? unawaangalia wanapotoka shuleni na kurudi nyumbani na unapozungumza na mtoto wa kidato cha 4 hafikii yule wa darasa la 7 enzi zile za karibu kidogo ambazo hakika mambo ya kitaalamu walipewa nafasi wataalam kuendesha...

  Unajiuliza watoto hawa watafanya nini kwa nchi yao? wana lipi la kujivuna na kuitetea nchi yao? Unapojiuliza sana unahisi moyo wako unatoa machozi hata kama hayatoki kwenye macho....

  Hapa ndipo ninapoiona post yako.....HAKIKA TANZANIA INATUDAI DENI KUBWA SANA WATANZANIA, hatuwezi kukwepa ukweli huu
   
 5. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  NewDawnTz,

  Inatia uchungu na sononeko sana kuifikiria Tanzania yetu ya leo. Wapo wengi ambao wanaona kila kitu ni sawa, na kama si sawa basi kitakuwa sawa huko mbeleni.

  Tumesahau vitu ambavyo ni basics. Tumejiingiza kwenye kuweka priorities za mambo makubwa na kusahau uwezo wetu. Tunataka computer kila shule wakati hakuna mlo kila nyumba.

  Lazima tufanye mjadala wa kulinusuru taifa letu. Huu ni lazima.
   
 6. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Amakweli wewe na watanganyika wenzako mwehu? Mzarau kwao mtumwa, kati ya babu yako na bibi yako na tanzania yupi alokuja mwanzo? Jee tanganyika imewakosea nini mpaka ikawa hamuipendi wala kuitaja muna ngagania tanzania ambayo muungano uko hatariri kuvunjika na wzanzibar kuwa na zanzibar yao, jee nyiyi mutabaki na tanzania muipendayo na kuzarau tanganyika mulio ipigania uhuru?.
   
 7. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Namsubiri AbdulHafif na yeye aje aseme lake.
   
 8. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka taratibu. Tutashindwa kuvumiliana.


   
 9. W

  Willygs21 New Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magufuli ni Kiongozi wa Mfano jamani!hayumo kabisaaa ktk kundi la wanasiasa uliowasema.But Politicians we need changes indeed LAA SIVYOOO 2015 Tuctafutane
   
 10. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaka Omary,

  Salam. Kwa nini tushindwe kuvumiliana?
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  mkuu si uliaga?

  au nilikuwa ninaota?
   
 12. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kamanda si nilisema mpaka vitambulisho vya utaifa vitoke, nipate hati ya kumiliki kiamba kule kijijini na kituo cha afya kikamilike na mpimaji wa maabara amalize kusoma? Pia nasubiri wanao wamalize elimu ya kata wakifaulu ndio niondoke. Hayo yakitokea ndio safari mkuu.
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Maradhi, umaskini na ujinga...
  Huyo mdudu wa mwisho ndio chanzo cha yote hayo.
  Ni ujinga kuwa na resources zote hizo na bado hufaidiki nazo.
  Ni ujinga kumpa mtu sh mia mbili halafu b'dae ukamwombe sh 50 (kwa nini ulimpa?).
  Ni ujinga kuruhusu akili yako kidogo uliyonayo itawaliwe na watu.
  Ni ujinga kutafuta tiba wakati hujajua ugonjwa.
  Kwanini uwe mjinga?
  Kweli ipo siku tutaona aibu kujitambulisha kuwa sisi ni watanzania, maana uozo wa wajinga wachache unaharibu jamii nzima.
   
 14. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Husninyo,

  Ulichoandika hapa mtu anaweza kupigana. Nimecheka kwa huzuni. Nakubalina nawe 100% ni ujinga. Eti unampa mtu 200 halafu unamuomba sh 50! Kweli ni upunguani. Hii nimekubali. Nimekugongea ka-thanks.
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Maradhi, umaskini na ujinga...
  Huyo mdudu wa mwisho ndio chanzo cha yote hayo.
  Ni ujinga kuwa na resources zote hizo na bado hufaidiki nazo.
  Ni ujinga kumpa mtu sh mia mbili halafu b'dae ukamwombe sh 50 (kwa nini ulimpa?).
  Ni ujinga kuruhusu akili yako kidogo uliyonayo itawaliwe na watu.
  Ni ujinga kutafuta tiba wakati hujajua ugonjwa.
  Kwanini uwe mjinga?
  Kweli ipo siku tutaona aibu kujitambulisha kuwa sisi ni watanzania, maana uozo wa wajinga wachache unaharibu jamii nzima.
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  siku zote nimekuwa nikiwaambia natamani sana Tanganyika ya Mwalimu Nyerere coz Tanzania niifahamuyo mimi si sehemu salama, ipo hovyo na haijal wananchi. Nataman Tanganyika ile ambayo wananchi wote tulikuwa sawa, licha ya umasikini wetu watu walijituma na waliishi kwa furaha huku wakiwa na Matumaini. Mwalimu Nyerere utakumbukwa Daima!
   
Loading...