Tanzania yangu na funika kombe mwanaharamu apite……….


bakuza

bakuza

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Messages
493
Likes
10
Points
35
bakuza

bakuza

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2010
493 10 35
Ndani ya rasimu hii tumeingiziwa serikali tatu yaani Ya Tanganyika,Zanzibar na ya Muungano,na mpaka sasa Zanzibar wanayo katiba yao kwa sasa tunahangaikia ya katiba ya Muungano ambayo itakamilika Mungu akijaalia mwaka 2014 na Uchaguzi mkuu ni 2015.Je uchaguzi utafanyika bila Katiba ya Tanganyika?Na kama tukianza maandalizi ya katiba ya Tanganyika hiyo miezi kadhaa itatosha kuikamilisha?

Na je nini kilitakiwa kuanza kati ya katiba ya Muungano na katiba za nchi zinazoungana? Tumeingiziwa Serikali tatu makusudi ku buy time ili uchaguzi upite..Haiingii akilini kuwa Wasomi wetu wote ndani ya Tume hawakuyaona haya… Kwa uelewa wa kawaida tu ni kuwa hata katiba ya Zanzibar lazima ifanyiwe marekebisho ili kuendana na katiba ya Muungano endapo Muundo wa muungano unabadilika.

Watanzania ondoeni matumaini ya kupata suruhisho la kikatiba mwaka 2014 kwa kuitegemea rasimu hii yenye baadhi ya mambo mazuri ya kutupumbaza ili mambo yaendelee kama wapangavyo,wanasiasa wanaangalia faida yao kisiasa na si taifa na watu wake.
Kuna mapungufu Mengi ndani ya rasmu hii yatupasa tupitie kwa utulivu na tutajifunza mengi.

Muda utaamua...
 
Bobwe

Bobwe

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2013
Messages
1,241
Likes
10
Points
0
Age
39
Bobwe

Bobwe

JF-Expert Member
Joined May 21, 2013
1,241 10 0
Kuanzia leo tanganyika pataitwa tanganyika bara.
 

Forum statistics

Threads 1,273,280
Members 490,351
Posts 30,476,446