Tanzania yan'gara kipimajoto cha amani

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Kwa hakika jana ilikuwa siku mbaya sana kwangu. Kilichoninyima raha si kingine bali taarifa zilizotolewa na Amnesty International na Human Rights Watch – Mashirika yanayochunguza na kuratibu hali ya haki za binadamu dunia nzima.

Taarifa zilizotolewa na mashirika haya zimeonyesha kuwa katika miaka 3 iliyopita, kumekuwa na ongezeko kubwa la ukandamizaji wa vyombo vya habari, watetezi wa haki za binadamu na vyama vya upinzani.

Naamini kwamba kila anayeitakia mema nchi yetu na kuipenda lazima atakuwa amefedheshwa na taarifa hizi ambazo zinapaka doa nchi yetu.

Natumaini kwamba mamlaka zinazohusika zitachukua hatua stahiki kurekebisha hali hii. Wakati nikiendelea kuganga mfadhaiko mkubwa niliokuwa nao kutokana na taarifa hizi, nilijikuta nakutana na taarifa nyingine ambayo kwa hakika iliniliwaza sana. Taarifa hii ni ya Kipima Joto cha Amani Duniani -Global Peace Index (GPI). GPI huchapishwa na Taasisi ya Uchumi na Amani (Institute of Economics and Peace - IEP).

Taarifa inaonyesha kuwa hali ya amani duniani imeboreka kwa mara ya kwanza baada ya miaka 5. Katika kipindi hiki na kwa nchi 163 zilizomulikwa na rada ya IEP, amani iliongezeka katika nchi 86 wakati amani ikipungua katika nchi 76. Iceland ndiyo nchi yenye amani kubwa duniani ikufuatiwa na New Zealand, Austria, Portugal na Denmark.

Nchi ambayo amani yake ina mgogoro mkubwa kabisa duniani ni Afghanistan ikifuatiwa na Syria, Sudan ya Kusini, Yemen na Iraq.

Nchi 10 bora kutoka Afrika na nafasi ya nchi husika ikiwa katika mabano ni:
 • Botswana (30
 • Malawi (40)
 • Zambia (48)
 • Tanzania (54)
 • Senegal (58)
 • Liberia (59)
 • Gambia (62)
 • Equatorial Guinea (70)
 • Benin (72)
 • Angola (77)
Tanzania kushika nafasi ya 54 ndiko kulikonipatia faraja na kwa kiasi kikubwa ikatibu majeraha ya taarifa za Amnesty International na Human Rights Watch.

Katika nafasi hii tumefanya vizuri kuliko nchi zote za Afrika Mashariki ambapo nafasi za wenzetu ni kama ifuatavyo: Kenya (119), Uganda (105), Rwanda (79), Burundi (135) na Sudan ya Kusini (161). Hata tumekuwa bora kuliko USA (128) na France (60)

Hali ya amani imegawanywa katika makundi 5. Kundi la kwanza lile linalojumuisha nchi zenye kiwango cha hali ya juu kabisa ya amani.

Hapa kuna nchi 13 zikiwemo Iceland, New Zealand, Austria, Portugal, Denmark, Canada, Singapore, Slovenia, Japan, Jamhuri ya Czech, Switzerland, Ireland na Australia. Kundi la 2 linajumuisha nchi ambazo hali ya amani ni kubwa.

Kuna nchi 62 na Tanzania imo katika kundi hili. Kundi la 3 ni lenye nchi zenye hali ya wastani wa amani linalojumuisha nchi 43 zikiwemo China, Uganda, Rwanda, n.k. Kundi la 4 ni lenye nchi ambazo hali ya amani iko chini.

Hapa kuna nchi 27 zikiwemo USA, Kenya, Afrika Kusini, India, Israel, n.k. Mwisho kabisa ni kundi la 5 ambalo hali yake ya amani iko chini sana. Hapa tunaziona nchi kama Nigeria, Sudan, Libya, Afghanistan, Syria, n.k

Kwa kuhitimisha hebu niseme hivi: katika kushika nafasi ya 54, tumeshuka nafasi 2 ukilinganisha na nafasi tuliyokuwa kwenye GPI ya 2018.

Je tutaendelea kutembea kifua mbele miaka ijayo au tutateremka?
 
Hahaha halafu inapata report mbaya amnesty international na HR watch. Kweli ccm ni chama cha majambazi.
 
Amani ni nini?: ni hali ya raha na salama bila ugomvi.

Utulivu ni nini?: ni hali ya kutoleta matata, hali ya kutulia.

Mimi kwa mtazamo wangu Tanzania tuna utulivu lakini sio amani.
 
Haya yote kwa ajili ya uongozi bora usiokubali kubabaishwa na mabeberu, ukiwaendekeza wanavuruga nchi, wamejaribu kutafuta pakuingilia, mara ebola, mara ugaidi.
 
Hahaha halafu inapata report mbaya amnesty international na HR watch. Kweli ccm ni chama cha majambazi.
Tanzania kuwa ya 4 kati ya nchi 53 Afrika na ya 54 ya nchi 163 ni matokeo mazuri sana. Haya ni matokeo ya utafiti ambao hufanwa kila mwaka. Pia imeeleza utafiti ulivyofanywa (Methodology). Ripoti ya Amnesty Internatuonal (AI) na Human Rights Watch (HRW) ni muhimu na inasitahili kufanyiwa kazi. Hata hivyo ina utafiti hafifu uliojengwa kwenye misingi ya “perceptions, isolated critical incidences and biased”. Ni tofauti na ripoti ya utulivu na amani.
 
Tanzania kuwa ya 4 kati ya nchi 53 Afrika ni matokeo mazuri sana. Haya ni matokeo ya utafiti uliohusisha nchi 163 duniani na hufanyika kila mwaka. Ripoti kamili ya matokeo na imebaibisha utafiti ulivyofanywa (Methodology). Ripoti ya Amnesty Internatuonal (AI) na Human Rights Watch (HRW) ni muhimu na inasitahili kufanyiwa kazi. Hata hivyo ina utafiti hafifu uliojengwa kwenye misingi ya “perceptions, isolated critical incidences and biased”. Ni tofauti na ripoti ya utulivu na amani.
Hii ya utulivu na amani ndio ya uongo, Wananchi hawawezi kukubaliana nayo, au kukubaliana nawewe.
Ukandamizaji ni mkubwa, hivyo sidhani, kama utulivu na amani inapimwa mkiwa mmekandamizwa.
 
Mkuu hapa hawaji nikwambie tu uzi huu wanaukimbia lazima udode,ila usijali.

Pamoja na gharama kubwa walioitumua kuichafua serikali ya awamu ya tano ,wamechemka,wamepenyeza uzushi huu kwa gharama kubwa lakini wameliwa,

Magufuli ni mwamba,mungu ambariki afya njema
Kwa hakika jana ilikuwa siku mbaya sana kwangu. Kilichoninyima raha si kingine bali taarifa zilizotolewa na Amnesty International na Human Rights Watch – Mashirika yanayochunguza na kuratibu hali ya haki za binadamu dunia nzima.

Taarifa zilizotolewa na mashirika haya zimeonyesha kuwa katika miaka 3 iliyopita, kumekuwa na ongezeko kubwa la ukandamizaji wa vyombo vya habari, watetezi wa haki za binadamu na vyama vya upinzani.

Naamini kwamba kila anayeitakia mema nchi yetu na kuipenda lazima atakuwa amefedheshwa na taarifa hizi ambazo zinapaka doa nchi yetu.

Natumaini kwamba mamlaka zinazohusika zitachukua hatua stahiki kurekebisha hali hii. Wakati nikiendelea kuganga mfadhaiko mkubwa niliokuwa nao kutokana na taarifa hizi, nilijikuta nakutana na taarifa nyingine ambayo kwa hakika iliniliwaza sana. Taarifa hii ni ya Kipima Joto cha Amani Duniani -Global Peace Index (GPI). GPI huchapishwa na Taasisi ya Uchumi na Amani (Institute of Economics and Peace - IEP).

Taarifa inaonyesha kuwa hali ya amani duniani imeboreka kwa mara ya kwanza baada ya miaka 5. Katika kipindi hiki na kwa nchi 163 zilizomulikwa na rada ya IEP, amani iliongezeka katika nchi 86 wakati amani ikipungua katika nchi 76. Iceland ndiyo nchi yenye amani kubwa duniani ikufuatiwa na New Zealand, Austria, Portugal na Denmark.

Nchi ambayo amani yake ina mgogoro mkubwa kabisa duniani ni Afghanistan ikifuatiwa na Syria, Sudan ya Kusini, Yemen na Iraq.

Nchi 10 bora kutoka Afrika na nafasi ya nchi husika ikiwa katika mabano ni:
 • Botswana (30
 • Malawi (40)
 • Zambia (48)
 • Tanzania (54)
 • Senegal (58)
 • Liberia (59)
 • Gambia (62)
 • Equatorial Guinea (70)
 • Benin (72)
 • Angola (77)
Tanzania kushika nafasi ya 54 ndiko kulikonipatia faraja na kwa kiasi kikubwa ikatibu majeraha ya taarifa za Amnesty International na Human Rights Watch.

Katika nafasi hii tumefanya vizuri kuliko nchi zote za Afrika Mashariki ambapo nafasi za wenzetu ni kama ifuatavyo: Kenya (119), Uganda (105), Rwanda (79), Burundi (135) na Sudan ya Kusini (161). Hata tumekuwa bora kuliko USA (128) na France (60)

Hali ya amani imegawanywa katika makundi 5. Kundi la kwanza lile linalojumuisha nchi zenye kiwango cha hali ya juu kabisa ya amani.

Hapa kuna nchi 13 zikiwemo Iceland, New Zealand, Austria, Portugal, Denmark, Canada, Singapore, Slovenia, Japan, Jamhuri ya Czech, Switzerland, Ireland na Australia. Kundi la 2 linajumuisha nchi ambazo hali ya amani ni kubwa.

Kuna nchi 62 na Tanzania imo katika kundi hili. Kundi la 3 ni lenye nchi zenye hali ya wastani wa amani linalojumuisha nchi 43 zikiwemo China, Uganda, Rwanda, n.k. Kundi la 4 ni lenye nchi ambazo hali ya amani iko chini.

Hapa kuna nchi 27 zikiwemo USA, Kenya, Afrika Kusini, India, Israel, n.k. Mwisho kabisa ni kundi la 5 ambalo hali yake ya amani iko chini sana. Hapa tunaziona nchi kama Nigeria, Sudan, Libya, Afghanistan, Syria, n.k

Kwa kuhitimisha hebu niseme hivi: katika kushika nafasi ya 54, tumeshuka nafasi 2 ukilinganisha na nafasi tuliyokuwa kwenye GPI ya 2018.

Je tutaendelea kutembea kifua mbele miaka ijayo au tutateremka?
 
Haya yote kwa ajili ya uongozi bora usiokubali kubabaishwa na mabeberu, ukiwaendekeza wanavuruga nchi, wamejaribu kutafuta pakuingilia, mara ebola, mara ugaidi.

Ripoti ya Amnesty International ni ukweli mtupu.
 
Naomba niongee Kama muwakilishi wa chama changu Cha democrasia kutoka ufipani "TANZANIA HATUNA AMANI WALA UTULIVU BALI TUNA VITA KALI SANA"

#Team kupinga
#Team CDM..
Nawasilisha wakuu.
 
Back
Top Bottom