Tanzania yalipwa dola 8,000,000/= kwa kumng'oa Nduli Idd Amini Dada

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,784
12,227
Serikali ya Uganda imeilipa Serikali ya Tanzania $ 8m kwa kufanikisha kuuangusha utawala wa dikteta Nduli Idd Amini Dada wa Uganda na hivyo kumwezesha Rais Museveni kuingia madarakani. Mwaka 1979 majeshi shupavu ya Tanzania (JWTZ) yaliyapatia majeshi ya Uganda kipigo kitakatifu na kusababisha Nduli Idd Amini Dada kuikimbia nchi!

Source: Radio One - Kumepambazuka!

Je mapato kama haya yanabarikiwa na Bunge letu tukufu ili kuingizwa katika matumizi?
 
sasa habari ya kumepambazuka unapost njaa zinauma....... BTW watajua wenyewe walipwe wasilipwe.. it makes no difference....... zile za TAMISEMI kwani zimerudi ?
 
sasa habari ya kumepambazuka unapost njaa zinauma....... BTW watajua wenyewe walipwe wasilipwe.. it makes no difference....... zile za TAMISEMI kwani zimerudi ?
Kama Bunge linahoji Sh. 800,000,000/= zilizopelekwa Mbarali bila idhini yake bila shaka lina kila sababu kujua kama fedha hizi ziliwekwa katika mapato ambayo serikali inatarajia kupata mwaka huu wa fedha!

Vinginevyo zinaweza kupigwa tiki taka na kuingizwa katika mifuko ya mafisadi au viongozi wetu wakishirikiana na watumishi wasio waaminifu wakajipasia wenyewe!
 
Serikali ya Uganda
imeilipa Serikali ya Tanzania $ 8m kwa kufanikisha kuuangusha utawala wa
dikteta Nduli Idd Amini Dada wa Uganda na hivyo kumwezesha Rais
Museveni kuingia madarakani
. Mwaka 1979 majeshi shupavu ya Tanzania
(JWTZ) yaliyapatia majeshi ya Uganda kipigo kitakatifu na kusababisha
Nduli Idd Amini Dada kuikimbia nchi!

Source: Radio One - Kumepambazuka!

Je mapato kama haya yanabarikiwa na Bunge letu tukufu ili kuingizwa
katika matumizi?

Utakuwa kizazi cha Lulu weye!
Una uhakika Mseven ameingia madarakani baada ya Idd Amin Dadaa kupinduliwa na Majeshi ya Tanzania?
 
Kama ni kweli basi hizi pesa zilitakiwa ziende moja kwa moja kujenga mabweni hasa ya wasichana katika shule za kata nchini, lakini kwa uchu basi zitaingizwa serikalini ili tuzigawane kupitia posho zetu za vikao.
 
...Mwaka 1979 majeshi shupavu ya Tanzania (JWTZ) yaliyapatia majeshi ya Uganda kipigo kitakatifu na kusababisha Nduli Idd Amini Dada kuikimbia nchi!
Utakuwa kizazi cha Lulu weye!
Una uhakika Mseven ameingia madarakani baada ya Idd Amin Dadaa kupinduliwa na Majeshi ya Tanzania?
Sijaona alipoandika 1979 Mseveni aliingia madarakani. Unaweza ukawa kizazi cha zamani lakini ukawa unashindwa kuelewa hata sentensi zilizo dhahiri, na kizazi cha Lulu wakawa na akili kuliko cha akina Naibu waziri wa elimu
 
Kama ni kweli basi hizi pesa zilitakiwa ziende moja kwa moja kujenga mabweni hasa ya wasichana katika shule za kata nchini, lakini kwa uchu basi zitaingizwa serikalini ili tuzigawane kupitia posho zetu za vikao.

Hata mimi nafkiria inaweza ikawa hivyo, hawa viongozi hata hawaaminiki.
 
Dola huwa zinatumia alama ya "$" na si "/=". Hii ya pili inatumika kwa shilingi
Asante kwa kunielimisha! Hata hivyo lengo langu ilikuwa kuonyesha "bila senti" yaani 800,000.00
 
Hee! , Nilidhani kwamba tulimpiga Amin kwa sababu alivamia Nchi yetu, Na kwamba Tumempiga kwa sababu ya usalama wa nchi yetu, Kumbe tulimpiga ili tulipwe!. ya kwamba tulikodiwa!. kama mamluki!
 
Kama Bunge linahoji Sh. 800,000,000/= zilizopelekwa Mbarali bila idhini yake bila shaka lina kila sababu kujua kama fedha hizi ziliwekwa katika mapato ambayo serikali inatarajia kupata mwaka huu wa fedha!

Vinginevyo zinaweza kupigwa tiki taka na kuingizwa katika mifuko ya mafisadi au viongozi wetu wakishirikiana na watumishi wasio waaminifu wakajipasia wenyewe!

mkuu hili bunge lako la ndio mzeee usitarajie lifanye lolote!
 
Nashauri fedha hizo zitumike kuwaboreshea maisha wapiganaji wetu mashujaa wanaoteseka mitaani baada ya kustaaf...
 
Hee! , Nilidhani kwamba tulimpiga Amin kwa sababu alivamia Nchi yetu, Na kwamba Tumempiga kwa sababu ya usalama wa nchi yetu, Kumbe tulimpiga ili tulipwe!. ya kwamba tulikodiwa!. kama mamluki!
​Hakuna cha bure siku hizi!! Sasa hivi tunazingojea za Kabila wa DR Congo!
 
Back
Top Bottom