Tanzania yaleta aibu kwenye Boxing (TBF)

senator

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
1,924
66
Leo nilikuwa naangalia taarifa ya habari kwenye sehemu michezo nikashangazwa sana na aibu ambayo Tanzania imetuletea kwenye mchezo wa Ngumi(boxing).
Tanzania kama nchi mwenyeji wa mashindano ya ridhaa ya Mabingwa wa mabingwa wakiwa na nchi wageni Kenya,Uganda na Shelisheli…yaani timu ya Tanzania haikutokea kwenye mashindano ingawa asubuh walikwenda kwenye weighing na bout zikapangwa, ila mchana wakat wa mechi wakaingia mitini.Nimeshangazwa zaidi na Mwenyekiti wa chama cha ngumi za ridhaa Joan Minja anasema hata yeye mwenyewe anashangaa kutokuwaona vijana wake!!Ni kweli timu ilikuwa kwenye maandalizi duni sana na malalamiko yalianza kujitokeza mapema vijana kuwa wanahama hata kwenye hotel zakuishi na kwenda kwenye za bei nafuu pia posho zao zilikuwa utata mtupu.Hata timu ya Uganda ilipofika jana walalamikia mapokezi na hta huduma za malazi.
Binafsi kama mpenzi wa michezo hili limeniudhi sana ni bora wangehairisha mapema kama walikuwa hawajapata wadhamini kuliko kuwasumbua watu wametoka mbali afu mnafanya mambo ya Kipopompoo!!
Uongozi mzima naona haufai kwa maendeleo ya Ngumi nchni.
 
njaa ndugu yangu... sasa hivi watu wote nguvu kwenye kampeni mkuu...
 
Waandaji nadhani watakuwa walipata wadhamini na kutakuwepo na zawadi za washindi ila kwenye michezo ujanja mwingi haswa kwenye hizi boxing kuanzia Yule Mwenyekiti mwenye Kesi (alhaj) na wengineo wote walikuwa wanaendesha chama kimagumashi tu..Nimesikitika sana...
 
Mini nashangazwa sana na aibu ambayo Tanzania imetuletea kwenye michezo Mbalimbali kama Boxing na riadha. Ni Aibu sana kwa nchi yetu ya Tanzania ambayo inawafanya Biashara wakubwa, Ina wapenda michezo wengi wenye uwezo sana inashindwa kushiriki ipasavyo kwenye michuano au mashindano mbalimbali ingawa wakti mwingine hali inakuwa ngumu lakini kwa mtazamo wangu hali hii kwa nchi yetu inatokana na kutokuwajibika ipasavyo kwa waliopewa dhamana ya kuongoza sekta hii ya michezo. Unajua mara kadhaa timu zetu za michezo mbalimbali zinapofanya vibaya wachangiaji wengi hukimbilia kusema tujitoe kwa miaka 5 mpaka 10 eti baada ya hapo tutakuwa katika kiwango muafaka kushiriki. Mimi kwa upande wangu nataka kutofautiana nao kama ifuatavyo
1. Hivi tumewahi kujiuliza vipi maandalizi ya timu zetu za michezo mbalimbali zinavyo andaliwa.
2. Hivi tumewahi kufutatilia jinsi timu nyingi zinavyo andaliwa huwa ni okoteza okoteza zaidi ya uhalisia
3. Hivi tumeshawahi kujiuliza tunavioungozi wa aina gani katika sekta za michezo?
4. Hivi hatuoni jinsi viongozi wengi wanaingia kwenye sekta hizi kuchumia matumbo yao?
5. Hivi hatuoni jinsi viongozi wengi wanaingia kwenye michezo kwa minajili ya kujenga majina yao kisiasa?
 
nimesikia kipindi cha tuongee michezo cha redio one asubuhi ya leo kuhusu sauala hilo, kwa kweli uongozi wa shirikisho unatakiwa ubebe lawama zote na ikiwezekana wajiuzulu wameleta aibu kwa taifa. Hawana hela hata kidogo bado wakatake initiative ya kuandaa hayo mashindano. Kama hawakuwa na hela lakukuwa na sababu ya kuitisha mashindano hayo.

Watanzania tunaogopa sana kusema ukweli, walitakiwa kusema hatuwezi kuhost mashindano hayo straight, na wala sio kubeat around the bush halafu inakuwa aibu.

Longolongo inatucost sana watanzania, left right and centre
 
Wachezaji badala ya kuwekwa kambini wanaambiwa wawe wanakuja asubuhi wakitokea nyumbani wakati mdhamini katoa posho na kila kitu jamaa wakaona isiwe tabu wameamua kuingia zao mitini.
 
Wachezaji badala ya kuwekwa kambini wanaambiwa wawe wanakuja asubuhi wakitokea nyumbani wakati mdhamini katoa posho na kila kitu jamaa wakaona isiwe tabu wameamua kuingia zao mitini.
Kuna mdau kazungumza hapo juu watu wanakimbilia kwenye michezo kuuza majina kisiasa yao pasipo kujali maslahi ya mchezo husika.Kwa kweli Mchezo wa ngumi za ridhaa unataka mtu kujitoa na si kutegemea malipo..nakumbuka zaman enzi zakina Salim seif Nkama( RIP) akiwa mwenyekiti huu mchezo ulikuwa upo kwenye nidhamu nzuri na walijitahidi sana kutafuta sponsors wakuendesha mashindano mbalimbali ya kimataifa na kitaifa pasipo kutegemea kupata fadhila za kisiasa kwenye boxing.Walikuwa wapo kwenye ajira zao so haikuwa kuongoza kama kulilia njaa.Sasa viongozi wote waliopo yaani nashindwa hata kuwasemea mana PR hakuna ,uwezo mdogo wa kuijua michezo so inakuwa vigumu kwenda kuomba hata sponsor kwenye big companies.Aibu hii wamejitakia wenyewe TBF ..maandalizi yalikuwa hafifu vijana wanataka posho na chakula wawezekuwa fit kimazoezi chama kinawapa uso wa mbuzi!...Naona kuna haja ya kupiga chini uongozi mzima na kujipanga upya.Huyu mama Minja sijui kama anajua boxing inavyokwenda hata amateur boxing ya wanawake sidhani kama ipo bongo kwa sasa.Kichefu chefu tu
 
Kuna tatizo kubwa sana kwenye vyama vya michezo, vingine vimejijengea aina fulani ya U-royal family ndani yake, kitu ambacho kimewasababishia kupoteza kabisa mvuto na hata kukosa ushawishi kwa sponsors. Watu wanapitia humo kupeperusha majina yao tu, ubunifu zero scouting capability zao ni blabla tu wanategemea majeshi, badala ya kuizunguka Tanzania kutafuta vipaji wanakaa Dar tu, aibu hii haiwezikwisha mpaka uzalendo wa kweli utakapoingia nchini ukitokea kule ulikopotelea.
 
BMT yaikaanga BFT kashfa ya mabondia
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limesema kwamba kitendo cha mabondia wa Taifa kugoma kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki ya mabingwa wa mabingwa ni kielelezo cha uongozi mbovu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT).

Mabondia wa Tanzania waligoma kushiriki mashindano hayo kwa kile walichoeleza kutolipwa fedha za posho kutokana na ushiriki wao kwenye mashindano hayo na pia kuelezwa waende nyumbani wakale kisha warudi kupigana, wakati wenzao wa nchi nyingine walipewa huduma zinazostahili.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa BMT, Idd Kipingu alisema lengo la mashindano hayo lilikuwa zuri kuwapa mazoezi wachezaji wa Tanzania watakaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini India Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo alisema tatizo lililosababisha mabondia kugomea mashindano hayo ni la kiuongozi, kwani hakukuwa na mchakato mzuri wa maandalizi, ushirikishwaji wa wachezaji, viongozi na mamlaka husika kwa maana ya BMT na Wizara.

Kipingu alisema taarifa alizonazo ni kuwa Katibu wa BMT alikutana na Katibu wa BFT na kumwambia asifanye mashindano hayo kutokana na kuwepo uwezo mdogo wa kuyaandaa.

Alisema bahati BFT haikuzingatia angalizo lililotolewa na Katibu wa BMT na mashindano yaliendelea kufanyika hata kusababisha mabondia wa Tanzania kugomea mashindano hayo.

"Kupuuza angalizo la Baraza na kushindwa kuandaa kikamilifu mashindano haya ni kielelezo cha uongozi mbovu ndani ya shirikisho hilo," alisema Kipingu.

Kuhusiana na suala la wachezaji wa tenisi ambao nao wiki hii waligoma kwa muda kushiriki mashindano ya kimataifa, Kipingu alisema nalo linafanana na mambo ya ngumi.

"Matukio haya yanaashiria kuwa migogoro ya aina hiyo itaendelea kushamiri katika vyama vyetu, suala la uongozi mbovu katika vyama vyetu ni suala mtambuka," alisema na kuongeza kuwa BMT inajipanga kuandaa semina ya uongozi kwa vyama vyote kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Alisema semina hiyo itaeleza mawasiliano yanayohitajika ndani ya chama na nje ya chama na kwamba kwa wakati huu vyama vyote vya michezo vikae pamoja, wachezaji na viongozi ili kuona kwamba aibu haijitokezi tena.

Katika hatua nyingine Serikali imeagiza lazima timu ya taifa netiboli ishiriki mashindano ya kimataifa yatakayofanyika nchini Afrika Kusini mwezi huu.

Akizungumza jana, Kipingu alisema Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) na kile cha Zanzibar (Chaneza) havina budi kukutana na kumaliza tofauti zilizopo ili timu ya Taifa ya netiboli ‘Taifa Queens' ishiriki bila matatizo yoyote.

SOURCE: habari leo
 
Back
Top Bottom