Tanzania yakumbwa na uhaba wa chakula

Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
16
Dira ya dunia BBC ya tarehe 23/Jan/2008 imetangaza kuwa bahadhi ya maeneo ya mikoa ya kusini yana upungufu wa chakula hasa mahindi. Kama kawaida wananchi wanachemsha mizizi ya porini.

Akiojiwa waziri wa Kilimo, uhakika wa chakula na ushirika-- Mh. Stephen wassira amekanusha kuwepo na uhaba wa chakula source yake ikiwa ni mikoani. Lakini mwandishi Abdalla MAjura alizidi kumbana na baadaye kwa mbali ndo akakubali upungufu wa MAHINDI.

Ikumbukwe huyu waziri kubisha ni tabia yake kwani hata CCM walipozomewa kule MBEYA alikataa kabisa kuwa hawajazomewa hadi pale vyanzo mbalimbali vya habari vilipoamua kuweka mambo bayana.

Hivi ni kweli tatizo la njaa au ukosefu wa chakula limetushinda kulipatia ufumbuzi hadi tutegemee misaada?
 
Hapa ndo nakubaliana na JOHN BWIRE wa Raiamwema kwenye toleo no. 013 kwenye makala yake hii hapa;

KWA miezi kadhaa sasa, Watanzania wa rika mbalimbali, wamekuwa wakijihusisha na udaku. Na udaku huu sasa umeshamirishwa na yanayoendelea ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Basi, kila mtu amekuwa ni chanzo kizuri cha habari kuhusiana na wizi ndani ya BoT. Kila mtu anataka kujua kwa kina nini hasa kilichotokea ndani ya BoT. Si kwamba hiyo si halali ya raia, la hasha. Kila raia wa nchi hii, ana hisa sawa na mwingine. Na kwa hiyo yanayojiri BoT ni halali yakafahamika, na umma ukaridhika na hatua zitakazochukuliwa.

Tangu Juni mwaka jana BoT ni mada moto, na pamoja nayo, ni mgodi wa Buzwagi na kampuni ya kufua umeme ya Richmond. Kwa ujumla sasa tunakaribia robo tatu ya mwaka nchi ikizungumza habari za ufisadi na mafisadi. Basi mtu akilala ni ufisadi, na akiamka ni mafisadi!

Nchi nzima imetekwa na vuguvugu la ufisadi na mafisadi. Ni kana kwamba hatuna shughuli nyingine ya muhimu ya kufanya. Na hiki ni kilema chetu cha siku zote. Ndiyo. Ni kwenda na Mdundiko. Na kwa kawaida, kama mzazi hakuwa makini, basi Mdundiko humchukulia wana. Akaja kuwapata baada ya siku kadhaa kupita. Atashukuru Mungu kama watakuwa bado wanapumua!

Ni nani anayeweza kusema kwamba tangu baada ya Bajeti ya mwaka jana tumezungumza kwa kina, kuhusu mada nyingine, kwa mfano, kama kilimo? Ama kuwa sahihi zaidi, kuhusu chakula?
Hakika hatutakula BoT, wala Buzwagi wala Richmond. Na sasa majira ndiyo hayo yanapita huku tukishindana wenyewe kwa wenyewe kukwepa wajibu wetu katika mambo ambayo kimsingi tulitakiwa tuyafanye.

Sisi tunasema, mwisho wa siku, pamoja na mambo mengine, tutahitaji kula. Lakini kama tutaendelea na mzaha huu wa kutekwa na jambo moja tu na tukasahau vitu vingine vya msingi, basi tunakaribisha hatari.

Huu ni wito kwa wote, kwamba sasa tugeuzie fikra zetu kwenye uhai. Hazina zetu za vyakula si nzuri kiasi hicho. Tayari baadhi ya sehemu nchini zinaashiria kukumbwa na uhaba wa chakula, lakini kwa ujumla mambo yetu mengi hayaendi kwa hakika, laiti kama tungechukua muda kidogo tukatafakari nje ya mada hizi za kupita!
 
inashangaza kwani wanaoteseka ni watanzania masikini ambo ndi wapiga kura na wanaowaweka madarakani na enjoy neema! na mara wanawasahau wateseke kwa njaa!
Dira ya dunia BBC ya tarehe 23/Jan/2008 imetangaza kuwa bahadhi ya maeneo ya mikoa ya kusini yana upungufu wa chakula hasa mahindi. Kama kawaida wananchi wanachemsha mizizi ya porini.

Akiojiwa waziri wa Kilimo, uhakika wa chakula na ushirika-- Mh. Stephen wassira amekanusha kuwepo na uhaba wa chakula source yake ikiwa ni mikoani. Lakini mwandishi Abdalla MAjura alizidi kumbana na baadaye kwa mbali ndo akakubali upungufu wa MAHINDI.

Ikumbukwe huyu waziri kubisha ni tabia yake kwani hata CCM walipozomewa kule MBEYA alikataa kabisa kuwa hawajazomewa hadi pale vyanzo mbalimbali vya habari vilipoamua kuweka mambo bayana.

Hivi ni kweli tatizo la njaa au ukosefu wa chakula limetushinda kulipatia ufumbuzi hadi tutegemee misaada?
 
Uhhhhhhhhh! Aliyeshiba kawaida hamkumbuki mwenye njaa! Kwa kweli siku ya hukumu ya mwenyezimungu tutakimbiana!wanadamu tutakuwa na hali mbaya!
 
sitashangaa wataanza kupitisha kile kikopo cha kuombea ka' cha mzee Matonya..!! Halafu tutachangiwa hadi bilioni 40!!
 
Hivi zile pesa walizochangisha wakati ule wa ukame ziliisha zote? kwani na wafanyakazi wa serikali walikatwa kwenye mishahara bila utashi
 
bahadhi ya maeneo ya mikoa ya kusini yana upungufu wa chakula hasa mahindi. Kama kawaida wananchi wanachemsha mizizi ya porini.

Kama kusini wanamaanisha Lindi na Mtwara! naomba nichangie kama ifuatavyo!
Zamani zile kipindi cha masika ilikuwa ni kawaida kutokana na ubovu wa barabara!
ukiachilia karanga, korosho, nyanya chungu na mihogo, vingine vyote vinatoka nje.
Hawa jamaa si wakulima aka wavivu! Na kula mizizi ni jadi yao! kuna mizizi fulani ni common sana mtwara (jina nimelisahau), sijui kama ndio alikuwa anamaanisha hiyo au?
 
Back
Top Bottom