Tanzania yakopa Benki ya Dunia tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya Elimu, Barabara na Mawasiliano!

Benki ya Dunia imeikopesha Tanzania jumla ya tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya sekta za Elimu, Barabara Mawasiliano na uchumi jumuishi.

Source: ITV habari
Bila katiba ya wanyonge hii nchi tutakuja kuuzwa, maana tunanuka madeni........siku mkidemkia kwa mchina mtajua kama hamjui.....
 
Naona kila siku ni habari za kukopa na serikali ikijivuna kwa hilo lakini sijaona taarifa za kulipa madeni
 
Kukopa kusikoambatana na nidhamu ya fedha ni kusaliti vizazi vijavyo!
Haswaaa......hapo utaambiwa zimeagizwa VIIEITE mpya kwa ajili ya wakuu wa mikoa na wilaya, bila kusahau viongozi waandamizi wa chama chakavu, maana wao tuliambiwa na polepole gari wanayotembelea inaanzia kiwango cha VIIEITE......
 
Sikuelewi mkuu.
Una maana gani na hiyo "kuifungua"?
Huwezi elewa ila namaanisha connectivity ya barabara kwenye nchi yetu iko hovyo na msimu wa mvua ndio kabisaa ,tatizo kubwa ni fedha zilikuwa kiduchu.

Inamaana wakiimarisha ufikikaji wa maeneo jita itakuwa kubwa kwenye uchumi na uwekezaji utaongezeka.
 
Huwezi elewa ila namaanisha connectivity ya barabara kwenye nchi yetu iko hovyo na msimu wa mvua ndio kabisaa ,tatizo kubwa ni fedha zilikuwa kiduchu.

Inamaana wakiimarisha ufikikaji wa maeneo jita itakuwa kubwa kwenye uchumi na uwekezaji utaongezeka.
Unasema "Siwezi elewa"?

Katika haya uliyoeleza hapa wewe unadhani ni kipi kigumu sana kueleweka kiasi cha mimi nishindwe kuelewa? Umejuwaje kiasi cha uelewa wangu!
 
Hiyo 2.7T inaenda kupigwa na wajanja wachache tu wanaojiandaa na uchaguzi wa 2025.

Hizi tozo tunazochapwa daily zinaingia fungu lipi?

Nchi ipo set kwenye auto-pilot.
Rubani kaenda zake vacation. How comes kodi za miamala tunaambiwa znajenga barabara na madarasa afu bado wanakopa zngne?
 
Kwaiyo zile harakati za Lema kuzunguka Dunia nzima ili Tanzania isipewe misaada lime buma,si ndio?
 
Benki ya Dunia imeikopesha Tanzania jumla ya tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya sekta za Elimu, Barabara Mawasiliano na uchumi jumuishi.

----
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kutoka Benki ya Dunia (WB).

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Warwick ndio Wamesaini mikataba hiyo kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IDA).

Kupitia mkopo huo, miradi itakayotekelezwa ni katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar.

Barabara za vijijini zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 693.2, mazingira ya elimu ya juu wa bilioni 982.1 bilioni na digitali bilioni 346.6.

Aidha,huduma za umeme Zanzibar zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 328.1 bilioni ukiwemo mkopo wa Bilioni 346.6 kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi visiwani humo.
Kwanini wanakopa kwa ajili ya barabara ili hali wakijua wameweka tozo ya miamala kwa ajili ya ujenzi wa barabara?

Hii nchi ni bora DIASPORA warudi nyumbani wagombee nafasi za juu kuongoza nchi sio bure kuna walakini pahala
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom