Tanzania yakopa Benki ya Dunia tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya Elimu, Barabara na Mawasiliano!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,902
141,845
Benki ya Dunia imeikopesha Tanzania jumla ya tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya sekta za Elimu, Barabara Mawasiliano na uchumi jumuishi.

----
mkopo.jpg

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya shilingi trilioni 2.7 kutoka Benki ya Dunia (WB).

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Warwick ndio Wamesaini mikataba hiyo kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IDA).

Kupitia mkopo huo, miradi itakayotekelezwa ni katika sekta ya Elimu, Barabara, Tehama na Nishati ya umeme, Tanzania Bara na Zanzibar.

Barabara za vijijini zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 693.2, mazingira ya elimu ya juu wa bilioni 982.1 bilioni na digitali bilioni 346.6.

Aidha,huduma za umeme Zanzibar zitanufaika kwa mkopo wa Bilioni 328.1 bilioni ukiwemo mkopo wa Bilioni 346.6 kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi visiwani humo.
 
Daaah, 2.7t inaenda kuingia mtaani, mifukoni mwa kina mkwere, kurudisha zama za "...unajua mi nani....", laki si pesa. Elimu, barabara, sawa.

Zitatolewa mara moja au kwa awamu? Maana ni takribani 10% ya bajeti yote ya nchi
 
Serikali imekopa Sh. 2.7 trilion kutoka benki ya dunia kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara na elimu! Wakati huo huo serikali inatutoza tozo za simu kwa miradi hiyo hiyo.

Chonde chonde serikali usitutwishe mizigo ambayo hatuwezi kuibeba! Tanzania ipo milele na watu wataendelea kuijenga kwa kadri wanavyo ongeza uwezo wa mapato na si kukamuliwa!

Huku kodi, huku tozo, huku kulipa madeni, huku bima ya afya nk, hii sasa imekuwa balaa!
 
Kuna bili za nyumba na mita za umeme, mpaka akili ziwakae sawa maana wavunge wenu mliowachagua ndio wanapitisha hivyo vitu bila ya kupigwa, anyway wapinzani walitucheleweshea maendeleo
 
Haya mambo ni ya ajabu sana, yanafikirisha, ukiwa mkopaji utakuwa mtumwa wa mkopaji, kwa nini kama taifa tusiwe na utaratibu wa kujiendesha wenyewe kwa hela zetu za ndani?

Haya mamikopo ndo yanatupa kiburi ya kutojibana kama taifa badala yake,tunajilipa maposho ya ajabu, wabunge wanajilipa wanavyotaka, misafara ya ajabu ajabu, hapa mzigo anatwishwa mwanannchi wa kawaida, kimsingi CCM imeishiwa sera, hawana jipya tena, laiti uchaguzi ungekuwa mwaka huu walahu pamoja na tume yao ila wasingeambulia kitu!

Sasa hivyi nchi hii imekuwa sio tena wananchi mbali ya kikundi cha CCM bungeni, mwananchi haangaliwi tena, wanajali matumbo yao tu!! Kimsingi huyu mama ajitafakari wananchi wengi wana hasira Naye, sijui hao wapambe kama wanamfikishia taarifa, lakini ni ukweli usiopingika kuwa umaarufu wa mama umeshuka kwa kiwango cha 4g mtaani, na Ccm washukuru watanzania wengi ni wajinga, ila ingekuwa kama ni nchi za wezetu wenye akili , lumumba pangewaka moto!!!
 
Back
Top Bottom