Tanzania yaingia hofu ya kukosa misaada sio kujipima na muungano wake

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
EU. KATIKA BAJETI YA MWAKA HUU, EU ILIPANGA KUIPA TANZANIA SH. TRILIONI 1.56, WAKATI UINGEREZA ILIPANGA KUTOA MSAADA WA SH. BILIONI 622. – TANZANIA YAINGIA HOFU YA KUKOSA MISAADA SIO KUJIPIMIA NA MUUNGANO WAKE – MUHAMMAD YUSSUF

Katika Gazeti la Nipashe toleo la Jumaane tarehe 27Juni 2016
kulichapishwa makala yanye kicha cha habari “Serikali yaingia hofu Uingereza kujitoa EU”. Pamoja na mambo mengine, Mwandishi wa makala hiyo, Sanula Athanas, ameandika kuwa “SERIKALI imesema kujitoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya (EU) huenda kukawa na athari kwa Tanzania kutokana na mchango mkubwa wa nchi hiyo katika misaada inayotolewa na umoja huo nchini”.
Akizungumza na Nipashe jana kuhusu athari za uamuzi huo kwa Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Servacius Likwelile, alisema nchi huenda ikaathirika kimisaada na uwekezaji kutokana na uamuzi huo.

“Ni kweli kuna hofu ya athari zitakazotokana na uamuzi huo. Dunia nzima inalizungumzia suala hilo, lakini sisi bado hatujajua kitatokea nini maana Uingereza bado haijatoka (rasmi) kwenye Umoja wa Ulaya. Hofu iliyopo ni ikiwa uchumi wa Uingereza utashuka kwa maana hisa na thamani ya fedha yao kushuka katika soko la dunia, Tanzania tutaathirika kwa maana ya misaada inayotoka EU kwa sababu Uingereza anachangia.”

Hata hivyo, mtendaji huyo wa serikali alisema athari za uamuzi huo zitatokea kwa Tanzania ikiwa uongozi mpya wa Uingereza utaona hakuna haja ya kuwekeza na kutoa misaada kwenye miradi iliyokuwa ikichangia wakati nchi hiyo ikiwa EU. Katika bajeti ya mwaka huu, EU ilipanga kuipa Tanzania Sh. trilioni 1.56, wakati Uingereza ilipanga kutoa msaada wa Sh. bilioni 622. Kwa mujibu wa Waziri wa
 
Back
Top Bottom