Tanzania yaimarisha usimamizi/udhibiti wa matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
296
681
Wataalamu wa Nguvu za Atomiki kutoka nchi 46 za Afrika wamekutana Arusha kujadili utekelezaji miradi ya matumizi salama ya Sayansi na Teknolojia ya nyuklia katika nchi zao

Ni Mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 46 wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki ( IAEA )

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema wamekutana kuweka mikakati ya matumizi sahihi ya Atomiki

Nchi za Afrika zimepata manufaa makubwa katika matumizi ya Atomiki hususani Tanzania ambayo imepata Tsh bilioni 9 zinazotekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ununuzi wa vifaa tiba vya kuchunguza Saratani katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam na Bugando jijini Mwanza

Aidha, wanaendelea kupata mafunzo mbalimbali ya jinsi ya kudhibiti mionzi isilete madhara

Pamoja na hayo Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imefanikiwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekenolojia Mheshimiwa William Ole Nasha wakati wa ufunguzi wa mkutano huo

1552398235987.png
 
Back
Top Bottom