Tanzania Yaibuka Kinara wa Uwekezaji EAC Yote. Yasweka Kibindoni Dola Bilioni 1

Tanzania kinara uwekezaji EAC kwa dola bil. 1

TANZANIA imezipiku nchi zote za Afrika Mashariki kwa kupata uwekezaji mkubwa wa Dola bilioni 1.0, kwa mujibu wa taarifa ya uwekezaji ya kidunia iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Biashara Sawia Kimataifa (UNCTAD).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya uwekezaji wa kidunia kwa mwaka 2020, Burundi ilipata uwekezaji wa Dola million sita, Kenya Dola milioni 717, Rwanda Dola milioni 135 na Uganda Dola milioni 823.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dk. Maduhu Kazi, alisema jana kwamba janga la corona imesababisha Tanzania kuvutia mitaji ya viwanda vya dawa za binadamu hususani vifaa vya kujikinga (PPE).

Kuhusu ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji, Dk. Kazi alisema katika kipindi cha mwaka wa 2020/21 miradi ya wawekezaji ya Watanzania pekee iliyosajiliwa ni 66 sawa na asilimia 28 ya miradi yote 235 kwa kipindi hicho.

Pia alisema miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni iliyosajiliwa ni 65 sawa na asilimia 28 ya miradi yote, hivyo katika miradi 235 iliyosajiliwa, asilimia 56 ya miradi hiyo Watanzania wamehusika katika umiliki wake.

Alisema kutokana na maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka 2020/21 kumekuwapo mafanikio makubwa katika eneo la uwekezaji ambayo ni kusajiliwa kwa miradi mipya 235 inayotarajia kuwekeza mtaji wa Dola za Marekani bilioni 3.3 na kuzalisha ajira mpya 36,849.

Idadi hiyo, alisema ni ongezeko la asilimia nane ya miradi iliyosajiliwa mwaka 2019/20 ambapo ilisajiliwa miradi 219 na kwamba miradi miradi 99 iko Dar es Salaam ikifuatiwa na Pwani 34.

Mikoa mingine na idadi ya miradi kwenye mabano ni Mwanza (15), Dodoma (13), Arusha (120, Shinyanga (11), Mara (tisa), Iringa na Tanga (minane) kila mmoja, Morogoro (saba), Geita (minne), Lindi na Ruvuma (mitatu kila mmoja), Kagera (miwili) na mikoa iliyobakia mradi mmoja kila mmoja.

Dk. Kazi alisema sekta ya uzalishaji viwandani yenye miradi 138 ikiongoza kwa uwekezaji.

Alisema kuongezeka kwa miradi ya uwekezaji kumechangiwa na jitihada zilizofanywa na uongozi wa serikali ya awamu ya sita akitoa mfano wa Aprili hadi Juni, mwaka huu ambapoTIC ilisajili miradi 84 ambayo ni ongezeko la asilimia 68 ikilinganishwa na miradi 50 kipindi kama hicho mwaka jana.

Pia alisema ajira na mitaji inayotarajiwa kutokana na miradi ya Aprili hadi Juni ni wastani wa mara sita ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka jana na kwamba kuongezeka kwa miradi, ajira na mitaji hiyo inatokana na maboresho mbalimbali yaliyofanywa na TIC

Mkuu kweli unaweka uzi wa kusifia uwekezaji wa dola Billion moja kwa nchi yenye raslimali nyingi hivi ?

CCM mmeshachoka kuongoza nchi ?
 
Something is better than nothing.
 
Mnajidanganya
 
Back
Top Bottom