Tanzania yafanikiwa malengo endelevu

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
SERIKALI ya Tanzania imefanya vizuri katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) katika sekta mbalimbali hasa za afya, elimu, viwanda na miundombinu katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi.

Kauli hiyo aliitoa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Adolf Ndunguru jijini hapa jana wakati akifungua mkutano wa wadau kufanya tathmini ya Ripoti ya Utekelezaji Malengo hayo yaliyosainiwa hapa nchini tangu Septemba mwaka 2015 na kuanza kutekelezwa Januari mwaka 2016.

Alisema wadau kutoka sekta binafsi (PS), asasi zisizo za kiraia (CSO), washirika wa maendeleo (DP) na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) na kutoka Zanzibar, wamekutana kufanya tathmini, kutoa maoni na kuiboresha ripoti hiyo kabla ya kuiwasilisha kwenye Umoja wa Mataifa Julai mwaka huu.

Ndunguru alisema tangu Januari, mwaka 2016, serikali imetekeleza malengo hayo kwa kuboresha sekta mbalimbali za umma zikiwemo za elimu kwa kupanua elimu hiyo na kuitoa bure kutoka shule za awali hadi sekondari kidato cha nne.
Pia alisema katika kuboresha sekta ya afya, serikali imeboresha huduma hiyo kwa kujenga miundombinu ya kutolea huduma za afya pamoja kuongeza bajeti ya wizara hiyo kwa ajili ya kuboresha huduma za wananchi. “Serikali katika kuinua uchumi, imefanya vizuri katika kupunguza mfumuko wa bei ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yaliyokusudiwa na Umoja wa Mataifa katika agenda ya 2030,” alisema.
 
Back
Top Bottom