Tanzania yadaiwa kujitoa kwenye Mahakama ya Afrika. Amnesty International na UN walaani hatua hiyo. Serikali yatoa ufafanuzi

Legacy yote aliyoiweka baba wa taifa hili mwal. Nyerer imepoteza na jiwe kwa kipindi cha miaka 4 tu ya UTAWALA WAKE, )maana huyu jamaa sio kiongozi).. R,I,P mwalimu Nyerer. Ila wajue tu hata ALLY Bashiri aliisumbua sana mahakama ya ICC lakini leo yuko jela ya nchi yake mwenyewe, hakuna ubaya usio lipwa kwa ubaya.

RIP Kingunge. Ulitahadharisha vema wakakuona umeanza kuzeeka vibaya na kupoteza mental acuity! Mpaka dakika ya mwisho uliamini chama chako kimefanya makosa. I wish you were alive to witness how damn right you were.
 
Nilidhani Kabudi ni wa msaada kwa taifa kumbe ni kweli ni kutoka jalalani tu

Kwani hana msaada? Unadhani nani anashauri maamuzi ya kijasiri kama haya? Uchaguzi wa Zanzibar 2015 ulipofutwa tuliutangazia ulimwengu kuwa sasa sisi tunakula nyama ya binadamu. Since then, no going back; ni kula nyama ya binadamu kwa kwenda mbele. Waliofuta uchaguzi ule walijiamisha walikuwa wanaisadia nchi! Kumbe walikuwa wanapanda mbegu mbaya sana; ya kula nyama ya Binadamu!
 
Nikiri waz na mm ni mmoja wao wa watu waliokuwa wakiona mahiga ana akil sanaa.

Heb nambie kwan katika hil anahusikaje mzee??

Kwa muda mrefu nimekuwa nikiamini hii nchi yetu sasa inaongozwa na kitchen cabinet; kuna maamuzi makubwa sana yanafanyika bila mashauriano ya kutosha ndani ya vyombo rasmi. Mfano mmoja ni ile barua ya Wizara ya Mambo ya Ndani kutaka makanisa kufuta zile nyaraka zao za Kwaresma na Pasaka bila Waziri wala Katibu Mkuu wa wizara kujua! Ni nani alitoa hayo maelekezo ya kuandikwa barua hiyo?
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiamini hii nchi yetu sasa inaongozwa na kitchen cabinet; kuna maamuzi makubwa sana yanafanyika bila mashauriano ya kutosha ndani ya vyombo rasmi. Mfano mmoja ni ile barua ya Wizara ya Mambo ya Ndani kutaka makanisa kufuta zile nyaraka zao za Kwaresma na Pasaka bila Waziri wala Katibu Mkuu wa wizara kujua! Ni nani alitoa hayo maelekezo ya kuandikwa barua hiyo?
Completelly disorganized..
 
Mahiga alisifiwa sana ooh mzee yule anaonekana ana busara sana sijui nini,haya sasa kazi kazi.

Watu wa chama kile wote wanafanana wanavyofikiria,wanavyotenda etc
Dr. Mahiga anapangiwa tu.

Bora hata ajiuzulu.

Anavyozidi kuwa na utawala huu, ndivyo anazidi kuchafuka nao.
 
Mahiga: Hatujajitoa Mahakama ya Afrika

Monday December 2 2019


BY Asna Kaniki, Mwananchi akaniki@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Serikali haijajitoa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR) bali imeiomba kubadilisha itifaki.

Alisema uamuzi wa kujitoa utakuja baada ya ombi la kubadilisha itifaki hiyo yenye utata katika shughuli za kimahakama kushindikana.

Alisema Serikali imeiandikia barua mahakama hiyo yenye makao makuu yake jijini Arusha kuondoa itifaki hiyo ambayo inapingana na sheria ya Tanzania na kusisitiza kuwa kwa sasa haijajitoa bali inasubiri marekebisho hayo.

“Tunachosubiri kwa sasa ni marekebisho hayo ila ikishindikana basi tutajitoa. Kwa sasa bado hatujajitoa kama inavyosemekana,” alisema.

Miongoni mwa shughuli za mahakama hiyo ni kusikiliza kesi zinazofunguliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali au wananchi dhidi ya Serikali.

Mpaka sasa nchi tisa kati ya 30 zilizoridhia itifaki hiyo zimesaini kuwapa uhuru huo wananchi wake kudai haki zao mahakamani pindi Serikali inapowatendea kinyume. Zilizosaini Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Gambia, Ghana, Mali, Malawi, Tanzania na Tunisia.

Zilizoridhia ni Algeria, Burundi, Cameroon, Chad, Comoros, Kongo, Gabon, Kenya, Libya, Lesotho, Msumbiji, Mauritania, Mauritius, Nigeria, Niger, Rwanda, Jamuhuri ya Kidemokrasia Sahrawi, Afrika Kusini, Senegal, Togo na Uganda.

Miongoni mwa kesi za Tanzania ambazo zimewahi kuamriwa kwenye mahakama hiyo ni ya mwanamuzi maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Johnson Nguza au Papii Kocha.

Babu Seya na wanaye walihukumiwa kufungwa maisha na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004. Walikata rufaa Mahakama Kuu wakashindwa, Mahakama ya Rufani ikawaachia huru watoto wawili lakini Babu Seya mwenyewe na Papii Kocha wakaendelea kutumikia adhabu hiyo.

Mwaka 2015 walikimbilia katika mahakama hiyo na Machi 23, 2018 ikakubali kukiukwa kwa baadhi ya haki zao hivyo kuamuru waachiwe ingawa walishapata msamaha wa Rais.

Kwenye maelezo yake Dk Mahiga hakueleza kipengele chenye utata katika itifaki hiyo bali alitaka aulizwe Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Ukiwa muoga kiasi hicho huwezi kuendelea mkuu. Ndiyo maana duniani kote wasomi kama wewe hawezi kuwa matajiri. Wasomi wanaamini theory sana angalia duniani kote matajiri siyo wasomi hata hapa nchini wakina Azam siyo wasomi hawaamini kwenye theory. Mara nyingi ukiwaza theory sana hutafaulu kwa lolote.
Top ten ya Matajiri Duniani hakuna hata mwenye Diploma wote wanaanzia Bachelor degree's mpaka PhD....
 
Nimesoma updates hapo juu, nimezidi kusikitika. Sijui nini kimetupata.

Pamoja na ubadhirifu wakati wa Mkapa na Kikwete, tulikuwa tunaelekea pazuri, legal and economic reforms angalau zilikuwa zinatia moyo.

Wenzetu wa Afrika walituamini,tulikuwa mediators,negotiators wa migogoro mbalimbali especially kwenye eneo gumu la Great Lakes.

ICTR kwa Rwanda ilikuwa Arusha na hata hii mahakama ya Afrika ya haki za binadamu iko pia Arusha! Yaani sisi sasa hivi tumekuwa watu wakusemwa na Amnesty International!

Hukiondoa hatari ya mtu mmoja mmoja kupoteza haki zake za kibinadamu lakini kama nchi tunapoteza our diplomatic clout. Tutasimama kumtetea nani kwenye bara hili kama ndani tunafanyiana hivi. Hatuna moral authority, very sickening.
 
Naanza kuwaza sasa kwa nini Pengo anataka tuangalie upande wa Pili wa Hitler na Musolin!
Hayupo sawa yule mzee, aidha ni mgonjwa,uzee au duress. Huwezi kumsifu Hitler au hata Mussolini. Mamilioni ya watu wasio na hatia walikufa kwa sababu ya hawa watu. Kama hauwezi ku condemn ubaya na ukatili, bora kukaa kimya.
 
Hivi sheria iliyotungwa mwwka huu kuhusu NGO ndiyo inayoitwa kukinzana na sheria za Tanzania? Je, kipi kilianza?

Sheria ya NGO ilifuata ile ya mahakama ya Afrika, Kwa nini walitunga sheria kinzani na protocol waliokubali awali?

Katika hilo kilichotungwa baadaye siyo batili?

Alexander The Great,
 
Unaambiwa ukiingia mule akiri unaacha mlangoni?
Mahiga alisifiwa sana ooh mzee yule anaonekana ana busara sana sijui nini,haya sasa kazi kazi.

Watu wa chama kile wote wanafanana wanavyofikiria,wanavyotenda etc
 
Kibanga Ampiga Mkoloni,

Kwa hiyo wewe ndio mwerevu lakini upo unaganga njaa hapa JF? Deni la taifa ukiangalia figures the BOT limekuwa linakuwa kwenye muelekeo ule ule kwa muda mrefu sana ukiachilia mwaka 1908/9. Ukitaka kufahamu mapato ya Serikali yapo wazi pamoja na matumizi. Wewe ni wale wale. Magufuli yupo kazini i.e. Chuma kiko Ikulu na kazi zinaendelea, Maendeleo ya Tanzania kwanza mengine baadaye.
 
Sheria nyingi zimetungwa 2015-2019 zinakwenda kinyume na protocol za United Nations na African Union, mfano sheria ya Uhuru wa Habari, Uwazi Wa Mwenendo/Matumizi Ya Serikali, Haki ya kupinga/kuandamana kwa amani (Ipo haki hii kikatiba na katika sheria za kazi) Watoto Wanaojazwa Mimba Haki ya Kurudi kusoma n.k

Zipo sheria nyingi zimetungwa zinakinzana na protocol za United Nations na African Union, kama vile Tanzania tumeanzisha Union Ya Kitaifa yetu pekee duniani.

Ila kuna wapumbavu hawaelewi haya, wanajua kuunga juhudi tu.
 
RIP Kingunge. Ulitahadharisha vema wakakuona umeanza kuzeeka vibaya na kupoteza mental acuity! Mpaka dakika ya mwisho uliamini chama chako kimefanya makosa. I wish you were alive to witness how damn right you were.

Unamwongelea Kingunge yupi? Watu wengine kaeni kimya, Kingunge ambaye alikuwa anatumia pesa za walipa kodi kujinufaisha yeye mwenyewe binafsi na familia yake? Pole sana. Viongozi waliopita wote wanajulikana mazuri na mabaya yao wapo wachache sana na wanajulikana, Nyerere mojawapo hakujilimbikizia mali. JK no, BWM no, Alhaji Mwinyi sina uhakika sana, Msuya no, Mramba no, Sokoine yes, we can list all of them. Acheni kuwapamba wasiopambika.
 
Back
Top Bottom