Tanzania yachajisha Mazishi ya Mandela, siri za kijeshi zaanikwa

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,596
1,071
Kikwete awaambia Mandela aliingia Tanzania kupitia njia za panya Mbeya na hakukaa Hotelini bali nyumbani kwa Nsilo Swai. Nafasi ya Tanzania katika historia ya SA yaanikwa.

Wajane Winne & Graca, Maraisi na waombolezaji wahaha kumtia jicho Mama Vic Nsilo Swai aliye hifadhi viatu vya Mandela miaka 27 kabla ya kumrudishia. Ukumbi walipuka kwa makofi kwa Mama Maria na Vic..

Wafichuliwa siri za kijeshi, viongozi wa ANC walipewa pasi za kusafiria za Tanzania. Wengine walipewa majina ya Kitanzania.

Amtania Thambo Mbeki kwamba yawezekana hajarudishapasspoti kwake.

Makamanda Wakuu wa Kijeshi wasisimuka kukumbushwa Makambi ya Kongwa, Dakawa, Mazimbu na Dabaga.

Ila hakutaja watoto waliochwa na Wasouth nchini.
 

Attachments

  • Tomb 2.jpg
    Tomb 2.jpg
    125 KB · Views: 204
Swai alikuwa Mmoja wa Mawaziri wa kwanza baada ya Uhuru. Huyu mama ndo Mk ?t wa Checheme Kilimanjaro
 
Back
Top Bottom