Tanzania yabadilishana sumu kwa dhahabu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yabadilishana sumu kwa dhahabu!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jogi, Feb 2, 2011.

 1. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 13,002
  Likes Received: 5,881
  Trophy Points: 280
  Watanzania wenzangu, mkataba wa uchimbaji dhahabu bhulyankhulu ni vibaya kuuacha uendelee, nimetafiti binafsi na kupata takwimu ambazo napenda wanajamvi mzijue, pengine itafanyika jitihada kwa pamoja tusimamishe wizi huu.
  Kila container la 20ft hupeleka sumu bhulyankhulu na kupakia "gold ore" yenye thamani sawa dolari za marekani milioni tatu na laki tano (usd 3,500,000m), msafara mmoja hujumuisha magari kwa uchache 20, mara nyingine hufika 35 na kupindukia.
  msafara huu hufanywa mara mbili au tatu kwa mwezi. ina maana kwa uchache 20*3*3500000 ni sawa usd 210,000,000, ukizibadili zinakuwa tsh 315,000,000,000. kwa mwezi, inakuwaje tufe njaa.
  thamani ya dolari ni tsh. 1500.
  kwa mwaka bhulyankhulu pekee tunaibiwa shilingi 3,780,000,000,000
  nimeambatanisha jpg baadhi ya magari yaliyosheheni sumu yakielekea bhulyankhulu yakirudi na gold ore (mchanga wa dhahabu)
  naomba kuwasilisha
   

  Attached Files:

 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 12,997
  Likes Received: 1,727
  Trophy Points: 280
  Wameamua kutupa sumu pia!!!???
  Yaani hawatosheki na kuvuna shamba la bibi.
  Wanahakikisha wanatutoa uhai pia.
  Tujipange tuwashughulikie.
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hatua za haraka zinahitajika!!!
   
 4. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hizo sumu ni kwa ajili gani???? Jamani viongozi wetu wanafanya nini???? utafikiri mchezo wa kuigiza???
   
 5. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 695
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkubwa hiyo sumu ni kwa ajili ya kutumia katika shughuli za uchimbaji au ni sumu kutoka nje inakuja kutupwa hapo Bulyankulu??
   
 6. jcb

  jcb JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu hii ni hatari kwa Taifa letu
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 13,002
  Likes Received: 5,881
  Trophy Points: 280
  ni sumu kwa ajili ya uchimbaji wa madini ambayo inatoka nje, kumbuka kuwa athari za sumu hiyo tunabaki nazo sisi, wanachukua dhahabu bure, rejea hesabu zangu, angalia picha pia uone hayo magari yaliyopakiza hiyo sumu.
  wametupangia sisi tumpate asilimia ngapi ya faida kama vile dhahabu hiyo ni yao.
  hatujawahi kuwapangia wenye visima vya mafuta kuwa tutanunua mafuta ghafi kwa bei yetu, wanapanga wao, iweje hatuna jeuri kwenye dhahabu yetu??????
   
 8. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu upo sahihi kabisa.
  Sumu hiyo ni kemikali ijulikanayo kama "CYANIDE". ni sumu hatari sana. tuliona kule geita na kahama mambo yaliyotokea watu walibabuka, mifugo iliathirika na kwa taarifa tu madhara ya sumu hii huwa inakwenda vizazi hadi vizazi. Kemikali hii hutumika kusafishia madini hasa ya dhahabu.

  Mimi hutumia barabara ya morogoro kutoka maeneo ya kibamba kila siku. Huwa nashuhudia kila baada ya wiki 2 fleet ya malori si chini ya 40 au 50 yakitokea bandarini kuelekea bara huku yakiwa na mabango ya kuashiria kuwa yamebeba sumu. "Cyanide" pamoja na "Mercury" ndizo kemikali zitumikazo kusafisha madini ya dhahabu, zinatumika sana na migodi ya hapa tanzania na ni KEMIKALI HATARI SANA KUPITA MAELEZO.

  Wanachukua mali zetu, wanatuachia sumu na mahandaki. Tufanyeje?
   
 9. Antonov 225

  Antonov 225 JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani kwa hii nchi kuwataka wabadilike wao kwa wao ni kwa neema tuu, Kwani watu hawa wamekaa kwenye harufu mbaya kwa mda mrefu na sasa wameizoea(fatigue) kwa hiyo hawafahamu kama kuna kitu kimeoza tena. Hapa labda watu wapige maombi mtu sijui afe ili uchaguzi urudiwe
   
 10. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 871
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Inabidi tuangalie vizuri hizi taarifa maana kama ni kweli tunaweza kuyafuata hayo magari na tukikuta ni kweli... Hii itakuwa ni kashfa kubwa sana kwa nchi hii..
   
Loading...