Tanzania yaanza kupima kiwango cha kukua kwa uchumi kwa 'nafasi'

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
hii nchi bana haiishi vituko.....................

leo nimekipata chengine.

mabwana na kina mama fulani wakiwa kwenye chumba cha mikutani wameibuka na tathmini kwamba uchumi wetu umekua kwani kumbukumbu zinaonesha kuwa miaka chache iliyopita Tanzania ilikuwa nafasi ya 153 miongoni mwa nchi 184, lakini sasa ni ya 152. kwa hiyo jamaa wale wanaojiita wachumi wakajinasibu kwamba uchumi wetu unakua kutokana na mipango na mikakati madhubuti ya kiuchumi ya serekali ya mzee wa msoga. [Source ITV]

ikaniuma sana. japo mimi si mchumi, lakini na umbumbumbu wangu wa uchumi, siamini kama unaweza kupima uchumi wa nchi kwa kutumia nafasi ya namba.


vituko vingine nilivyopata wiki hii:

Membe kudai Tanzania haiungi mkono suala la Kenya kuwasaka na kuwapiga al Shabaab wakati ni juzi kati tu imeripotiwa kuwa Mkuu wake wa kazi akiwa kwenye mizunguko yake huko Australia alikutana na Mkulu wa Kenya na kueleza waziwazi kama anaunga mkono hatua ya Kenya kuishambulia Somalia. [Source JF]

Kituko chengine ni zile porojo za Mohamedi Saidi kuwa uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa kwenye ule mtaa maarufu wa kulangua vipuri vya wizi vya magari....Kariakoo Gerezani. [Source JF]


This is why they say Thursday is the best day of the week.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom