Tanzania ya Viwanda na Umeme wa Mgao Makao Makuu ya nchi Dodoma

Lobapula

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
2,388
1,582
Tumekua tukihubiri kuhusu uwepo wa Tanzania ya viwanda na Tanzania kufika kuwa nchi yenye uchumi wa kati kufikia 2025 lengo hili halitafanikiwa kwani tangu wiki hii imeanza kumekuwepo na mgao wa umeme katika mkoa wa Dodoma ambao na makao makuu ya nchi toka Jumatatu hakuna umeme wa uhakika maeneo ya mjini jumatatu kulikua hakuna umeme kabisa,jumanne maeneo ya ipagala na kisasa na chaduru kulikuwa hakuna umeme kabisa,siiku ya jumatano maeneo ya mjini pia mpaka Iringa road kulikua hakuna umeme kabisa mchana kutwa jana pia maeneo ya uzunguni kulikuwa hakuna umeme kuanzia saa nne mpaka saa nne usiku leo pia mjini hakuna umeme toka asbuhi mpaka muda huu.

Ssasa tunajiuliza hivyo viwanda vitaendeshwa na nn kama nchi haina umeme wa uhakika? Kuna wajasiliamali wanaotegemea umeme katika stationaries kuna viwanda vidogo vya kusindika zabibu na kutengeneza wine wote hawa wanahitaji umeme wa uhakika lakn mpaka sasa tunaona nchi au Serikali imeshindwa kulisimamia au kutekeleza hilo swali linakuja je Tanzania ya uchumi wa kati kufikia 2025 itawezekana?

Wasalaam ni mimi Mkonongo
 
Back
Top Bottom