Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,666
- 729,801
Penye kustahili kupongezwa lazima tufanye hizo bila kujali tofauti zetu kisiasa kitamzamo kimaono na hata kisera.
Bila kujali serikali hii imeingiaje madarakani...slogan ya TANZANIA YA VIWANDA imewavutia kama si kuwafurahisha wengi
Kila unapozungumzia Tanzania ya viwanda wananchi wanajenga picha fulani ya kuvutia sana kwenye bongo zao...na hili si kwa wananchi tu bali hata kwa viongozi wote wenye kunia mema na mafanikio kama Taifa.
Mwalimu Nyerere mzee yule mchonga meno alikuwa na maono kama haya lakini kwa mtazamo tofauti kidogo kwamba alitaka tuanze na viwanda vidogo vidogo kuanzia vya pini mpaka viwanda vikubwa kabisa ambavyo umiliki wake ungekuwa ni wa Taifa kwa asilimia mia moja...alifanikiwa maono yake haya kwa asilimia za kukumbukwa.
Mageuzi ya kiuchumi kuingia kwenye soko huria yakatukumba bila maandalizi ya kutosha...tukakwama kwenye tope.
Ndoto hii inafufuka kipindi hiki ikiwa ni ndoto chotara, ndoto ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia wa kile tunachokitaka, uhalisia wa ndoto wa kuwa na chakwetu ambacho si chetu....hiki tulichonacho sio TANZANIA YA VIWANDA VYETU bali ni TANZANIA YA VIWANDA VYA WACHINA.
Mchina ni mjanja sana uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa sana, kwahiyo mahitaji yake ya malighafi yako juu sana.
Slogan ya TANZANIA YA VIWANDA wameipokea kwa mikono miwili, wanajifanya kuja kuwekeza kwa mikataba isiyojulikana sana lakini kwa asilimia 90 faida yote ikirudi kwao na kuwapatia wananchi wake biashara na ajira.
Serikali yetu bado iko usingizini tunamuuzia mchina ardhi kubwa kwa bei ya kutupa, baada ya hapo hata katenda ka milioni kumi anampa mchina mwenzake, malighafi zote kwa asilimia 85 zinatoka China, vyakula mpaka vitu vya starehe nk.
Kwa kuzuga ndani ya mfumo wa kiuongozi wanaweka wazawa wachache kwenye nafasi za chini kishapo lundo la vibarua ndio huwa kubwa sana huku wakijitapa kuwa wameleta neema ya ajira.
Hatujachelewa sana lakini ni wakati wa serikali kugutuka isije kufika mahali tukawa watumwa fulani kiuchumi kwa kumruhusu mgeni afanye vile atakavyo. ..sheria zetu ni dhaifu bado na huyu mchina anatumia udhaifu wake kutuzunguka.
Mkuranga yote mpaka kibiti ni viwanda vya wachina Kibaha mpaka chalinze lugoba na maeneo mengi ya nchi ni wachina tupu (tutegemee spicie mpya ya chotara za kichina miaka ijayo....)
Nitoe tu rai kwamba pamoja na nia yetu njema sana ya kuwa na Tanzania ya viwanda tuwe makini sana tusijejikuta tunakuja kujikuta tuna Tanzania ya viwanda vya wachina.
NIA NJEMA IENDANE NA MIPANGO THABITI MAONO NA TAFAKURI KUU
MUNGU IBARIKI TANZANIA