Tanzania ya viwanda: Je, serikali ya CCM inayo dira sahihi kufikia ndoto hii?

K

karama kaila

Senior Member
Joined
Jan 30, 2015
Messages
122
Likes
16
Points
35
K

karama kaila

Senior Member
Joined Jan 30, 2015
122 16 35
Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais John Pombe Magufuli inaimba ndoto ya Ujenzi wa Viwanda nchini. Hilo ni jambo jema kwa nchi yetu inayopambana ili iendelee kiuchumi na kuondoa umasikini.

Viwanda ni sehemu muhimu ya Ujenzi wa uchumi imara katika ulimwengu huu wa leo. Kwa hivyo, jitihada zozote chanya zenye kuonyesha dhamira ya kuhakikisha nchi yetu inakuwa na viwanda vikubwa, stahimilivu na endelevu kwa uchumi wa nchi, ni jitihada za kuungwa mkono na mtanzania yeyote mzalendo.

Hata hivyo, serikali ya ccm haijatambua unyeti wa jukumu na wajibu wa jambo husika. Hili limedhihirishwa kufuatia msimamo wake wa kisera wa kutojihusisha moja kwa moja katika ujenzi na umiliki wa viwanda. Waziri wa viwanda anasema mara kwa mara kuwa wajibu wa wizara yake (Serikali) ni kutengeneza tu mazingira kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda. Kwamba jukumu la kujenga viwanda ni la sekta binafsi, macho hasa yakitolewa kwa wawekezaji kutoka nje.

Chama cha ACT Wazalendo, kinakosoa msimamo na mtazamo huo. Huo ni msimamo ambao kwa hakika utaichelewesha nchi kufikia malengo ya nchi ya uchumi wa kati mapema, kwa kuwa serikali inajivua jukumu inalopaswa kubeba na kutekeleza kwa nguvu zote.

Tunatambua ya kwamba Sekta binafsi ina mchango mkubwa katika Ujenzi wa viwanda, lakini si ya kuachiwa na kutegemewa jukumu hilo nyeti kwa uchumi wa nchi. Ni lazima Dola (serikali) ibebe jukumu hili sambamba na ushiriki wa sekta binafsi.

HALI ILIVYO SASA

Takwimu zinaonyesha kwamba Tanzania kuna viwanda vipatavyo 49243. Hii ni kwa mujibu wa sensa ya viwanda ya mwaka 2013. Kati ya viwanda hivyo 49243, viwanda vidogo vidogo ni 47921 sawa na 97.3% na viwanda 1322 sawa na 2.7% tu ndio idadi ya viwanda vikubwa.

Nafasi za ajira za moja kwa moja zilizotengenezwa na idadi hiyo ya viwanda ni takribani 264223.

Takwimu pia zinaonyesha kwamba nguvukazi ya umma wa watanzania ni 86% ya watu. Idadi hiyo ni sawa na watu wapatao milioni 38.

Ikiwa nguvukazi ya Tanzania ni watu milioni 38, na idadi ya watu walioajiriwa moja kwa moja viwandani ni 264223 tu ambao ni sawa na 0.7% pekee, ni dhahiri hali inaashiria kuwa mbaya. Nao mchango wa viwanda hivyo katika pato la taifa ni asilimia 7 (7%) tu.

Katika mazingira ya namna hiyo, taifa haliwezi kusubiri wawekezaji waje kulipatia nusra yake inayolikabili kiuchumi. Ni wajibu wa dola kuchukua hatua za makusudi sasa pasipo kuchelewa ili kulikwamua taifa na mkwamo huo.

TUNATOKAJE HAPA TULIPO?

Changamoto kuu zinazochelewesha ujenzi wa viwanda ni pamoja na uhaba wa mitaji, utaalamu na teknolojia.

Malighafi na masoko ya bidhaa sio tatizo hasa kwa kuwa malighafi hapa nchini ipo ya kusaza. Na fursa za masoko zipo za kutosha nchini, katika kanda zetu na kimataifa pia. Teknolojia na utaalamu katika ulimwengu wa leo ni rahisi kupatikana kutoka nchi zilizoendelea.

Kwa mantiki hiyo, changamoto ya msingi kwa mzingira ya nchi yetu ni suala la upatikanaji wa mitaji. Hili ndilo tatizo ambalo serikali ya ccm imekosa ubunifu wa utatuzi wake, mpaka kufikia hatua ya kujivua majukumu yake na kuyatelekeza kwa wanaoitwa 'wawekezaji' kutoka nje. Ikiwa tukiendelea kukubaliana na maoni haya ya serikali kwamba tutajengewa viwanda na wawekezaji kutoka nje, tutasubiri zaidi ya karne nzima pasipo kuona hatua za maana kwa taifa letu kujijenga kwa uchumi wa viwanda.

Chama cha ACT Wazalendo kinapendekeza Sera yake ya Hifadhi ya Jamii itumike kutekeleza lengo la kujenga viwanda. Hifadhi ya jamii kama chombo cha utatuzi wa changamoto za za kijamii, pia yaweza kuwa mwarobaini wa tatizo la viwanda hapa nchini.

Changamoto ya mitaji, inaweza kutatuliwa vizuri kwa uwekaji wa mfumo jumuishi wa hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni suluhisho la upatikanaji wa mitaji ya kuwezesha dola kujenga viwanda, kuwekeza katika kilimo cha kisasa cha biashara pamoja na matatizo mengine ya kijamii kama afya, elimu na bima.

Ili kupata fedha za kuwekeza katika ujenzi wa viwanda, panahitajika mkakati mahsusi wa taifa (wananchi) kuweka akiba. Endapo watu milioni 5 tu kati ya watu milioni 38 idadi ambayo ni nguvukazi ya taifa, watakuwa kwenye Hifadhi ya Jamii kuchangia kima cha chini cha chini kabisa kwa mwezi, akiba ya kiasi cha tsh. 1.8 trillion itapatikana kila mwaka. Kiasi hicho ni sawa na 2.5% ya pato la taifa. Hicho ni kiwango kikubwa kinachoweza kufanikisha Uwekezaji mkubwa kwenye kilimo na viwanda.

Kwa uchumi kama wa Tanzania unaokua kwa wastani wa 7% , ili kuondoa umasikini inahitajika uwekaji akiba wa 35% ya pato la taifa na zaidi. Nchi ya China, kwa mfano, ambayo uchumi wake unakua kwa 10% uwekaji akiba wake ni 50% ya pato la taifa.

Mfumo wa Sera ya Hifadhi ya Jamii ni njia muafaka ya kuweza kufikia lengo la uwekaji akiba nchini, kiasi cha kutosha kufanya Uwekezaji tunaohitaji.

Nchi yetu imeendelea kusafirisha nje mazao bila kuyaongezea thamani na hivyo kupata fedha kidogo kutokana na mazao hayo pamoja na kupoteza ajira kwa mataifa mengine.
Mazao ya Kahawa, Korosho, Tumbaku, Samaki, Pamba, Katani, Maua na mbogamboga yamekuwa ni 'export' kuu za nchi yetu. Kuna haja mkubwa kuchukua hatua za makusudi zenye kuhakikisha kwamba Tanzania haiendelei kusafirisha mazao hayo yakiwa ghafi.

Tunashauri Serikali ianzishe makampuni ya kisekta kwa mazao hayo na mengineyo yanayozalishwa kwa wingi hapa nchini ili pamoja na majukumu mengine, makampuni hayo yawe na Kazi mahsusi ya kuhakikisha yanajenga viwanda vya kusindika mazao na kuuza nje bidhaa zenye thamani.

Wananchi watashiriki katika kuweka mitaji na umiliki kwa kununua hisa katika makampuni hayo ya umma.

Faida kuu zinazotokana na hatua hizo, ni pamoja na upatikanaji wa soko la uhakika kwa mazao ya wakulima wetu, upatikanaji wa nafasi nyingi za ajira, pamoja na ukuzaji wa kipato cha wananchi na nchi kwa ujumla.

HITIMISHO

Sekta ya viwanda INA nafasi ya kuchangia kiwango kikubwa zaidi katika pato la taifa tofauti na hii 7% ya sasa. Tunasisitiza, mapinduzi ya viwanda yatafanikishwa na watanzania wenyewe kwa msaada wa Serikali yao.

Wawekezaji kutoka nje pekee, hawawezi kuwa msaada wa kutegemewa kwa ujenzi wa maendeleo ya viwanda nchini mwetu. Tumewategemea wao kwa zaidi ya miaka 30 sasa tangu nchi yetu ifungulie milango ya sekta binafsi, lakini matunda yake si ya kujivunia kama Taifa- hayajai kiganjani. Hatuna budi kubadilisha Sera na mtazamo na hivyo kuchukua hatua za kiuwajibikaji kwa ajili ya hatima njema ya uchumi wa nchi yetu.

Imetolewa na Idara ya Uenezi

ACT Wazalendo
 
samora10

samora10

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2010
Messages
7,352
Likes
2,615
Points
280
samora10

samora10

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2010
7,352 2,615 280
Tanzania ya viwanda huku ukipiga vita sekta binafsi na mabenki ni ndoto.. Hakuna wawekezaji wenye cash ya kufungua kiwanda
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
45,240
Likes
13,760
Points
280
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
45,240 13,760 280
Serikali ya viwanda ni zaidi ya kuongea majukwaani.

Wakae na sekta binafsi kutatua shida wanazokumbana nazo kwenye shughuli zao za kila siku.

Pia wakajifunze nchi walizoendelea kwa kuwekeza kwenye viwanda walitumia njia gani kufanikiwa kwenye hilo.

Five years of doing nothing.
 
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Messages
22,249
Likes
48,268
Points
280
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2016
22,249 48,268 280
Tangu lini Kuku akazaa?
 
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Messages
8,553
Likes
6,660
Points
280
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2011
8,553 6,660 280
serikali ya viwanda kwa umeme huu wa kuungunga na bado wa bei kubwa itakuwa ndoto, labda vile viwanda vya gongo tu.
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,914
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,914 2,483 280
hata sasa tanzania tayari ni nchi ya viwanda. Inasadikiwa kuwa na viwanda zaidi ya laki 5 vikiwemo vya kusaga mahindi, kufatua matofali na gereji.
 
Mtemi mpambalioto

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
1,549
Likes
2,386
Points
280
Mtemi mpambalioto

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
1,549 2,386 280
niseme tu ukweli kuwa viwanda havijengwi siku moja pengine hata mwaka mmoja!

mwanzoni wananchi waliaminishwa kuwa serikali ndo itajenga viwanda lakin baadae mambo yalibadilika tukaambiwa wawekezaji ndo watakuja kujenga viwanda!

wazungu na wachna wanatucheka sana kwa kuwa hatujui tunatoka wap tunaelekea wapi!

mwijage kamuangusha rais kwa kuwa hakuja na mpango wa kweli wa kujenga viwanda! huwezi kutuambia kuna kiwanda cha matrekta kinajengwa wakat hakuna hata malighafi moja ya trekta inayotengenezwa nchini, Hiyo ni ASSEMBLY kwa maana hata goroli au taa ya trekta inatengenezwa nje huko! na kiwanda kitaishia kuleta ajira ya watu 50 tu
hv mfano kwa kuwatumia hata SUMA JKT tungeanza na kujenga kiwanda kama cha SAMAKI, tukanunua meli zetu hata mbili kubwa za maana zenye crane ya kukamata samaki wakubwa kabisa! kwanza kiwanda kingekuwa pure and 100% tanzanian!

kiwanda hchohcho cha samaki kingetoa BYPRODUCTS ambazo tungetengeneza hata chakula cha kuku, mafuta ya samaki na mbolea ya asili pia! hapohapo tungetengeneza ajira kibao ukianzia baharini ajira, kiwandani ajira, wasambazaji ajira, wauzaji ajira, yan mji ajira ajira ajira! huo ni mfano tu wa kiwanda kimoja ambacho hata gharama yake ingekuwa ndogo na soko lake la uhakika wa 100% hata kama tungeuzia jesh tu kiwanda kingepata mabilioni kila kukicha!

halafu tungekuwa tunauziana samaki hata elfu 4 kwa kilo

swali langu kwa mwijage je hata kiwanda hcho cha mfano kinahtaji uwekezaji kutoka nje au waziri na wewe upo kwenye mpango wa kumuangusha raisi wetu!???

swali la pili, je kwa kutumia mfano huo wa kiwanda cha samaki je ingeshndikana kujenga viwanda vingi vya kutumia malighafi zetu wenyewe ambavyo ving vingetokana na mazao ambayo yangewapa ajira kubwa watanzania? jaman mwijage hata kiwanda cha karatasi ambacho miti ipo iringa? hujaona hlo mpaka ulete kiwanda cha ku ASSEMBLE mavitu yaliyokwisha tengenezwa nje? hapa panatia shaka !

najua wapo watakaonizodoa na kusema sina maana lakin ukweli utabakia ukweli, huwezi kushndana na wazungu eti kutengeneza magari wakati wao walishajiimarisha kwa miaka zaid ya 200!

I wish ningekuwa mie ndo waziri wa viwanda! haki ya mungu leo hii tayari ningeshajenga viwanda na ela ya magufuli ningekuwa nimesharudisha na faida kibao mpaka sasa rais angekuwa anafurahia matunda ya kuhubiri viwanda huko na huko wakat wa kampeni! napata uchungu wa kutaman hata kukata kichwa cha mtu kumuweka alama tu ajue alikosea!

lazima kufanya uthubutu sio kutegemea wawekezaji hadi kiwanda cha kugharimu bilioni 5 unaleta mwekezaji ni aibu!mwijage ana maneno mengi sana mdomoni mpaka anakera! umemdanganya raisi eti kuna viwanda elfu 52 khaaaa! yan hata mtu akiwa na cherehani mbili za kushona nguo basi imekuwa kiwanda khaaaa:confused::(:rolleyes:

tupishe bwana mwijage muda unaenda na unaweka kiwingu sie tunataka viwanda vya watanzania sio wahindi na wachna!

uwezo tunao na nia tunayo tukiamua tutatoka hapa tulipo
 
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Messages
28,692
Likes
19,482
Points
280
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2011
28,692 19,482 280
Katika hili nakuunga mkono....ni kweli ana maneni mengi.Mtu ambaye mpaja sasa ameitwkeleza huu sera ya viwanda kimatendo ni Eng Evarist Ndikiro mkuu wa mkoa Pwani....nadhani huyu anaweza kuwa mbadala ...hana maneno mengi huyu....ni vitendo tu
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
35,783
Likes
24,216
Points
280
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
35,783 24,216 280
Viwanda msitegeme kuanzishwa na serikali hii!
Ni blah blah tu.....
LEO nilikuwa mingoi,bagamoyo kuna Jamaa nmeenda mtembelea Yuko ktk mchakato wa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mabati...
Watu wanafanya mambo kimya kimyaaa siyo kwa maneno....

Ova
 
T

Tanzania Njema Yaja

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Messages
3,057
Likes
2,120
Points
280
T

Tanzania Njema Yaja

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2015
3,057 2,120 280
Kapewa 8% ya bajeti yake ... wote wasanii tu
 
Msukuma_De_Great

Msukuma_De_Great

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2016
Messages
1,159
Likes
941
Points
280
Age
29
Msukuma_De_Great

Msukuma_De_Great

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2016
1,159 941 280
Kiukwel mwijage mtamtwisha zigo la lawama bure.. nchi haina dira ya wap tunaelekea ndo sababu ya haya yote hata mh alikua hajui na ajajiandaa kuwa mkulu na ilo wazo la viwanda alilichukulia kama ukataji wa michembe kule tabora.... mie napinga mwijage uku ni kuonewa kwan pia it seems mkulu anataka kila kitu afanye yeye sasa mawaziri wanakosa kujiamini ilo wazo likifeli sie hatumjui mwijage ila mkuluna pia asitafutwe mtu wa kufa nae kwa ili
 
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Messages
8,942
Likes
14,537
Points
280
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2015
8,942 14,537 280
viwanda chini ya huyu ndugu tunafeli, ukweli mchungu...
 
Lyamber

Lyamber

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2012
Messages
7,235
Likes
8,729
Points
280
Lyamber

Lyamber

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2012
7,235 8,729 280
Shida ya viwanda ipo kwenyr kodi nani aanzishe mradi utakao kua unaishia kulipa kodi tuu, hakutakua hata na kiwanda kipya katika awamu hii...
 
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
13,115
Likes
648
Points
280
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
13,115 648 280
Kwani Mwalimu alijengaje?
 
Wong Fei

Wong Fei

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2016
Messages
3,757
Likes
4,146
Points
280
Wong Fei

Wong Fei

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2016
3,757 4,146 280
Hiv bado kuna watanzania wana hii mambo ya ndoto za viwanda? Ishafeli siku nying sana hii mambo.
Wapo busy na faru Fausta na kuwateka watu. Viwanda vi..wonder?
 
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Messages
28,692
Likes
19,482
Points
280
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2011
28,692 19,482 280
So far nimeona jitihada zake za kuandaa makobngamano ya wafanyabiashara...seriously anatakiwa akaze buti.......hebu mcheki muhongo kwenye REA halafu mcheki mawasiliano na uchukuzi....nenda kwenye elimu...hata afya pamoja na kukkosa fedha ameweza kusimama....
 
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Messages
28,692
Likes
19,482
Points
280
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2011
28,692 19,482 280
Hiv bado kuna watanzania wana hii mambo ya ndoto za viwanda? Ishafeli siku nying sana hii mambo.
Wapo busy na faru Fausta na kuwateka watu. Viwanda vi..wonder?
Punguza kucopy mawazo ya wajjane na masuria ka mangee...jadili hoja kwa kina,
 
A

artch2311

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2016
Messages
609
Likes
277
Points
80
Age
42
A

artch2311

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2016
609 277 80
niseme tu ukweli kuwa viwanda havijengwi siku moja pengine hata mwaka mmoja!

mwanzoni wananchi waliaminishwa kuwa serikali ndo itajenga viwanda lakin baadae mambo yalibadilika tukaambiwa wawekezaji ndo watakuja kujenga viwanda!

wazungu na wachna wanatucheka sana kwa kuwa hatujui tunatoka wap tunaelekea wapi!

mwijage kamuangusha rais kwa kuwa hakuja na mpango wa kweli wa kujenga viwanda! huwezi kutuambia kuna kiwanda cha matrekta kinajengwa wakat hakuna hata malighafi moja ya trekta inayotengenezwa nchini, Hiyo ni ASSEMBLY kwa maana hata goroli au taa ya trekta inatengenezwa nje huko! na kiwanda kitaishia kuleta ajira ya watu 50 tu
hv mfano kwa kuwatumia hata SUMA JKT tungeanza na kujenga kiwanda kama cha SAMAKI, tukanunua meli zetu hata mbili kubwa za maana zenye crane ya kukamata samaki wakubwa kabisa! kwanza kiwanda kingekuwa pure and 100% tanzanian!

kiwanda hchohcho cha samaki kingetoa BYPRODUCTS ambazo tungetengeneza hata chakula cha kuku, mafuta ya samaki na mbolea ya asili pia! hapohapo tungetengeneza ajira kibao ukianzia baharini ajira, kiwandani ajira, wasambazaji ajira, wauzaji ajira, yan mji ajira ajira ajira! huo ni mfano tu wa kiwanda kimoja ambacho hata gharama yake ingekuwa ndogo na soko lake la uhakika wa 100% hata kama tungeuzia jesh tu kiwanda kingepata mabilioni kila kukicha!

halafu tungekuwa tunauziana samaki hata elfu 4 kwa kilo

swali langu kwa mwijage je hata kiwanda hcho cha mfano kinahtaji uwekezaji kutoka nje au waziri na wewe upo kwenye mpango wa kumuangusha raisi wetu!???

swali la pili, je kwa kutumia mfano huo wa kiwanda cha samaki je ingeshndikana kujenga viwanda vingi vya kutumia malighafi zetu wenyewe ambavyo ving vingetokana na mazao ambayo yangewapa ajira kubwa watanzania? jaman mwijage hata kiwanda cha karatasi ambacho miti ipo iringa? hujaona hlo mpaka ulete kiwanda cha ku ASSEMBLE mavitu yaliyokwisha tengenezwa nje? hapa panatia shaka !

najua wapo watakaonizodoa na kusema sina maana lakin ukweli utabakia ukweli, huwezi kushndana na wazungu eti kutengeneza magari wakati wao walishajiimarisha kwa miaka zaid ya 200!

I wish ningekuwa mie ndo waziri wa viwanda! haki ya mungu leo hii tayari ningeshajenga viwanda na ela ya magufuli ningekuwa nimesharudisha na faida kibao mpaka sasa rais angekuwa anafurahia matunda ya kuhubiri viwanda huko na huko wakat wa kampeni! napata uchungu wa kutaman hata kukata kichwa cha mtu kumuweka alama tu ajue alikosea!

lazima kufanya uthubutu sio kutegemea wawekezaji hadi kiwanda cha kugharimu bilioni 5 unaleta mwekezaji ni aibu!mwijage ana maneno mengi sana mdomoni mpaka anakera! umemdanganya raisi eti kuna viwanda elfu 52 khaaaa! yan hata mtu akiwa na cherehani mbili za kushona nguo basi imekuwa kiwanda khaaaa:confused::(:rolleyes:

tupishe bwana mwijage muda unaenda na unaweka kiwingu sie tunataka viwanda vya watanzania sio wahindi na wachna!

uwezo tunao na nia tunayo tukiamua tutatoka hapa tulipo
Pole Ndugu
Yaelekea hujui Hata Sera ya Viwanda,
Hujui kama sisi sio wajamaa tena
Hujui kama kisera Viwanda vinajengwa na sekta binafsi.
Kwamba serikali sasa haifanyi biashara au kuzalisha bidhaa Bali inakusanya kodi tu.
Kwamba Hata maeneo machache ambayo bado wanashikilia hisa ujue bado wanafanya hivyo kuwqanda watanzania wake kununua baadae.
Mwijage alikuwa sahihi aliposema kazi yake no kupiga debe baada ya kujenga mazingira ya uwekezaji.

I wish you kudu know beta
 
Mtemi mpambalioto

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
1,549
Likes
2,386
Points
280
Mtemi mpambalioto

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
1,549 2,386 280
Pole Ndugu
Yaelekea hujui Hata Sera ya Viwanda,
Hujui kama sisi sio wajamaa tena
Hujui kama kisera Viwanda vinajengwa na sekta binafsi.
Kwamba serikali sasa haifanyi biashara au kuzalisha bidhaa Bali inakusanya kodi tu.
Kwamba Hata maeneo machache ambayo bado wanashikilia hisa ujue bado wanafanya hivyo kuwqanda watanzania wake kununua baadae.
Mwijage alikuwa sahihi aliposema kazi yake no kupiga debe baada ya kujenga mazingira ya uwekezaji.

I wish you kudu know beta
wewe ndo huelewi kenge
 
Forum statistics

Threads 1,273,057
Members 490,259
Posts 30,469,138