Tanzania ya viwanda inataanza baada ya haya kukamilika

Wawekezaji ugopa sana itikadi za kijamaa na nature ya kiongozi ana itikadi zipi.Uchumi wa viwanda uchumi wa kati ni slogan sawa na Kilimo kwanza,big result now,nk kama zilizopita za kuchangamsha jukwaa.
 
Nahisi WATANZANIA WENGI hawajielewi na kama wanajielwa basi hawaelewi wanachokiandika au wanachokisema kutoka na Project zinazoendelea Nchini kwao..


Pia nahisi bado hamjanielewa why nimesema hivyo, ngoja niwafafanulie kitu labda mtanielewa.


• Unapotaka kuita wawekezaji basi lazma uhakikishe una miundombinu thabiti ya kutosha, Swali ni.. Miundombinu ipi inayotakiwa.

Well, jibu ni hili..

Miundombinu muhimu ni network ya USAFIRI na UMEME.

Why hivi viwili, ni kwasababu.. Kiwanja chochote kitahitaji zaidi Usafiri bora wa Mizigo yako ili kupeleka bandarini au sehemu husika za Nchi, lets say kiwanda kimeagiza Malighafi kutoka nchi za nje, Je mizigo yao itafika vipi Viwandani mwao ikiwa serikali haijaimaridha/Kuboresha miundombinu yake ya usafiri..

Yaani unakuta, Hakuna barabara nzuri za kiwango cha lami maana Viwanda vinasafirisha Tani kwa Tani za mizigo hivyo kama barabara ni mbaya zitaharibika kwa haraka na kukosa barabara kabisa, Au unakuta hakuna barabara kabisa au barabara zipo ila zinachangamoto nyingi kama folone za Tazara na Ubungo kwa magari ya mizigo pale Jijini Dar Es Salaam.

KUMBUKA;
Mizigo haisafiri kwa Malori tuu na wawekezaji wengi hupendelea kusafirisha bidhaa zao kupitia huduma ya Treni maana ndio huduma yenye USALAMA & BEI NAFUU zaidi kuliko usafiri mwingine.

Pia, kuna baadhi ya bidhaa zitahitaji kusafirishwa kwa njia ya ANGA.

SWALI NI;
Je, mna Viwanja vya ndege vya kisasa vitakavyoweza kupokea ndege kubwa na Abiria na Mizigo?

JIBU NI;
Tulikuwa hatuna ndo maana Raisi Magufuli akaanza na haya kwanza kwa kupanua Viwanja vya ndege Vilivyopo na kufikia angalau Standard nzuri kama sio ya Kimataifa.

PIA NIKUKUMBUSHE TU;
Nchi yetu ipo kando ya bahari hivyo tunahitaji Bandari maana Viwanda tunavyotegemea kuvianzisha vitahitaji zaidi uwepo wa BANDARI KUBWA ZA KISASA ili kufanikisha usafirishaji wa Bidhaa zake kwenda nje au upokeaji wa malighafi ili kufikisha kwenye viwanda vyake ndio maana Raisi Magufuli akaamua kutenga kiasi cha pesa na kuzitanua Bandari zetu zote ili wawekezaji wawe na kila sababu ya kuja kuwekeza katika Nchi yetu.

NA HII NDO SABABU AMEWEKEZA PIA KWENYE BARABARA;
Kwa maana bidhaa zinahitaji kufika sehemu mbalimbali haswa kwa muda maalum uliopangwa, ili kuwezesha hili Raisi Magufuli akaamua Kutanua Barabara Ya Morogoro Road kuanzia Kimara mpk Kibaha, na kuongeza kwa Kuweka Flyover/Interchange kwenye makutano ya Ubungo ili kupunguza au kutokomeza kabisa Suala la Foleni mahali pale sambamba na kuweka Flyover ya Tazara kurahisisha upitaji wa Magari ya mizigo itokayo Bandari Ya Dar Es Salaam kule kurasini yanayoshika njia kuelekea Ubungo na hatimae kutoka nje ya Mji.

• itakapofika 2023 na kuanza kupeta tuu na Lami kuingia Jiji la Dar Es Salaam mkitoka vijijini/Mikoani kwenu ndo mtakapoanza kuuona umuhimu wa hizo barabara na Flyover mnazozilaani na kuzipinga kila siku, Maana naamini mtakuwa mnatumia Dakika chache kufika majumbani kwenu kutokea Kituo kipya cha Mabasi kinachojengwa na Raisi Magufuli pale Mbezi Luis na kutokaa kwenye foleni mtakapofika ubungo maana Flyover itakuwa imeshakamilika.

MWISHO;
Mbali na mahitaji ya kawaida ya Umeme kwa Wananchi, VIWANDA VINAHITAJI UMEME MWINGI NA WA UHAKIKA ili kuendesha shughuli zake, so ili kuhakikisha Sera yake ya kushawishi WAWEKEZAJI KUWEKEZA VIWANDA nchini Tanzania, Raisi Magufuli akaamua kuhakikisha Umeme unapatikana kwa Wingi na kwa kuhakikisha hilo akaamua kuwekeza Pesa nyingine Nyingi ili kujengwa kwa Mradi Wa Umeme ule wa "Stiegler's Gorge Hydroelectric Power Station"

Pia nasubiri kwa hamu sana kukamilika kwa mradi huu then nione mtasemaje pale Bei ya Umeme itakapokuwa imepungua na kuongeza urahisi wa Maisha kwa watanzania.. Mfano wakakapokuwa wanauziwa Unit 100 kwa Tshs 10,000/= tofauti na Unit 28 wanazouziwa hivi sasa

• HAYA YAKISHAKAMILIKA TARAJIA KUONA VIWANDA VIKIJENGWA KAMA UTITIRI NCHINI KWETU.



Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni takataka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom