Je, Tanzania ya Viwanda imeshakamilika?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,840
17,437
Ni muda sasa Rais akihutubia bila kusikia neno "viwanda" kama ilivyokua kawaida yake

Na pia hakuna update yoyote ya viwanda vinavyojengwa

Labda niwaambie kitu tu nchi kuwa ya kiviwanda mnatakiwa muwe na viwanda kama utitiri yaani vya kutosha mfano kwa ukubwa wa Tanzania na watu wake ili kufikia uchumi wa kati tunapaswa tuwe na angalau viwanda laki mbili au laki tatu

Sasa hivi naskia nchi nzima viwanda vikubwa havifiki hata mia sasa hii ndo nini?

Labda niulize zile "ndaru" zilizokua zikurindima humu ndani na vijana wa lumumba wakibebea bango kwamba ni "viwanda" viwanda" yameishia wapi? Sasa hivi kwaya ni "mandege mandege"sasa hayo mapesa ya kununulia mandege si ingetosha kujenga viwanda vikubwa kila mkoa na itoe ajira za watu hata 50000 kwa kila mkoa??

Okay nirudi kwenye swali: Tanzania ya viwanda imeishia wapi???
 
Wakuu heshima kwenu,

Katika Uchaguzi uliopita yaani mwaka 2015, CCM na mgombea wao (John Magufuli) walikuwa wakihubiri kuwa Tanzania ya Magufuli itakuwa ya viwanda.

Baada ya uchaguzi tukaanza kusikia propaganda kutoka kila mahali kuwa viwanda tele vimejengwa mikoa yote, jambo la ajabu ni kuwa viwanda hivi si tu kuwa huwezi kukutana au kumfahamu yeyote aliyeajiriwa katika haya maelfu ya viwanda vipya lakini pia viwanda hivi ni ngumu mno kuviona kwa macho.

Nilidhani kwa kuwa Tanzania ni kubwa ngoja tuone katika uchaguzi huu Mgombea wa CCM kwa kuwa anapita kila mahali atakuwa anatuambia hapa kimejengwa kiwanda hiki, lakini ajabu na kweli Mgombea huyu hasemi chochote mahali popote kuhusu viwanda hivi vipya kwa maelfu yake, badala yake anasema flyover mbili (Tazara na Ubungo) zilizoko Dar es Salaam.

Naomba nitoe rai kwa Mgombea wa CCM, tafadhali huu ni wakati wa kutuonyesha haya maelfu ya viwanda pote unapofika.
 
Mheshimiwa Rais,

Kwa sasa sijasikia ukizungumzia Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya Viwanda, ambayo itatoa ajira kwa vijana kulingana na wingi wa viwanda hivyo, vijana ambao wako mtaani licha ya kuhitimu fani mbalimbali, sasa nilitaka nifahamu ile Tanzania ya Viwanda uliyoinadi 2015 imeshakamilika?

Kama imekamilika unapozunguka katika kampeni waeleze wananchi Tanzania yako ya viwanda uliyoahidi imeshakamilika ili ujizolee kura nyingi, kwa vijana ambao wamepata ajira katika viwanda hivyo ulivyoahidi.
 
Tanzania ya viwanda sio ya kuibeza.

It was and it is a right move to increase value of raw materials available in Tanzania ili kupata finished product kwa sokola ndani na nje ya Tanzania.

The best way, ilitakiwa tuwe na various business models on how do we get there.

BOT ilitakiwa na inatakiwa kui-facilitate TIB Bank ili Watanzania kupitia makampuni yao wakopesheke kuanzisha viwanda. Kuna policies za kujificha nyuma ya pazia kuwa sio lazima kuwa na mtaji kuanzisha kiwanda, huu ni uongo mweupe.

Wakati mmoja namba 1 wakati anazindua Mlinganzila Hosp, alitoa maelekezo Watanzania wanaotaka kuanzisha viwanda vya vifaa tiba wapewe mikopo na NHIF ambao nao walikuwa wanakopesha kwenye majenzi ya nyumba. Kwa namna ilivyo sijui mpaka sasa kuna utaratibu gani wa wazi ili to make the investment projects happen.

Namjua doctor mmoja Mwanza, mpaka sasa hajapata access ya funds. Kama angepata, angewekeza kwenye plant ya vifaa tiba ambayo ingetoa ajira za moja kwa moja kwa watu 45. Products zake zingeuzwa East Africa na SADC. Uzuri wa proposal yake, plant kama hiyo ipo Misri na South Africa pekee. Na sie Tanzania kupitia MSD tuna-import India na China....

Kuna wakati Prof. Kyaharara wa NSSF alikuwa na plan ya kukopesha equipment kwa ajili ya agro-processing. Hii nayo sijui ilishia wapi.

To make a summary, viwanda vingetoa ajira za moja kwa moja. likewise, supporting services sectors kama logistics, legal, banks, insurance, training, consultancy, pension funds zingekuwa. Serikali bado ina dhamana ya ku-facilitate. Ikiacha mambo yatokee by default, investor toka nje hawawezi kuja kuwekeza katika projects ambazo zitakinzana ni nini kinazalishwa katika nchi zao, achilia mbali athari ya capital flight kutokea as a result of generating income in our motherland.

Tujifunze kwa mining industry, hela zao wakiuza, wanaweka kulee ughaibuni. Hii ndiyo hatari ya wakuja. Angewekeza kafulila, Masanja au Chacha potentially, mpunga wao ungebaki kwenye bank zetu. Wangeweza kupanua biashara zao likewise ku-diversify na kutoa ajira zaidi
 
Inaendelea, Ndege mpya inawasili karibu kuipokea kama ukipenda, Tanzania mpya ya viwanda!
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom