Tanzania ya Uwazi na Ukweli!!!

Advisor

Member
Joined
Jan 10, 2008
Messages
40
Points
0

Advisor

Member
Joined Jan 10, 2008
40 0
Tanzania ya Uwazi na Ukweli!!!

Napata shida sana kuelewa kwa nini watanzania tunahangaika sana, kuzua na kubuni mambo ambayo ni haki ya kila mwananchi.
Sijajua kwa nini taarifa za mafisadi zinatolewa kama zawadi za peremende kwa watoto ili kuwahimiza kufanya jambo fulani.
Sijajua kwa nini, kwa mfano, kiongozi atoe taarifa kwa wananchi kwamba kuna watu wamesimamishwa kazi bila kuwataja majina na ikawa sawa tu kwake na kila mtu.
Huyo Gavana mpya alipoteuliwa alisema amefanya mabadiliko makubwa BoT halafu akaona akisema waliobadilishwa atakuwa amewapa watanzania zawadi kubwa sana. Badala yake akaacha tuanze kucheza kamari.
Hivyo vikao vya kamati za uchunguzi kwa nini haviwi televized?
Kwa nini hayo mahojiano yasirushwe na TV ya taifa badala yake TVs zetu zinakuwa muda mwingi zinaonyesha vichekesho vya America?
 

Forum statistics

Threads 1,366,653
Members 521,537
Posts 33,374,571
Top