Tanzania ya sasa inahitaji kiongozi dikteta na mwenye uzalendo wa kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ya sasa inahitaji kiongozi dikteta na mwenye uzalendo wa kweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, May 24, 2011.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,525
  Likes Received: 1,312
  Trophy Points: 280
  Umaskini wa kutupwa wa Tanzania (pamoja na nchi kujaa raslimali tele) umetokana kwa kiasi kikubwa na mfumo mbovu wa uongozi ambao umejaa ubinafsi, ulafi wa madaraka, ufisadi (corruption), ukosefu wa uzalendo (patriotism) na pia maono (vision). Kwa masikitiko mfumo huu ni mbovu kwenye ngazi zote kuanzia chini kwenye jamii mpaka ngazi ya juu kabisa, yaani, tatizo hili ni systemic na utatuzi wake lazima uwe systemic. Tanzania inahitaji viongozi makini wasio na chembe ya ubinafsi wala ufisadi na ambao ni wazalendo na wenye vision watakaosimamia (with zero tolerance )misingi imara ya sheria na katiba mpya iliyoundwa na watanzania wote kwa manufaa ya raia wote wa Tanzania. Nikiangalia Tanzania ya sasa sijui kama tunao viongozi wenye sifa hizi maana Tanzania ya sasa (baada ya miaka 50) bado imelala na raslimali zake (huku nyingine zikivunwa na wachache). Kwa kifupi, Tanzania bado ni nchi changa yenye kuhitaji kujengwa upya (labda na kizazi kipya!). Kwa sasa sijui! Perhaps (paradoxically!), kwasasa ili nchi iende na iwe kwenye mstari, panahitajika, at least, kiongozi wa nchi (rais) mwenye dictatorship mind na patriotism, ambaye atasimamia (whip by whip and with zero tolerance) misingi ya sheria za nchi na raslimali zake kwa kupambana na ufisadi na ubinafsi kwenye ngazi zote za uongozi huku akifungia macho masuala ya ushikaji ,udini na ukabila katika uongozi kwenye ngazi zote. Tulikuwaga na marehemu Sokoine ambaye angetufaa sana kwa kipindi hiki (keep resting in peace Mh). Sioni kwa karibu type ya kiongozi kama huyu kwa Tanzania ya sasa.

  Lead case examples:

  • China imekuwa inaongozwa na dictatorial regimes (with zero tolerance on corruption matters) and with real patriotism and vision, angalieni walipo wachina kimaendeleo.


  • Ujerumani ipo hapo ilipo kimaendeleo, ubora wa bidhaa na discipline ya hali ya juu kiutendaji kutokana na misingi imara iliyojengwa tangu enzi za dictator Hitler (aliyekuwa na zero tolerance kwenye mzaha wa kujenga nchi pamoja na kwamba ilibidi raia wengi wafe).

  • Urusi iko hapo ilipo (imejengwa) kwasababu ya juhudi ya kina Stalin na Vladmir Lenin ambao waliswaga raia wavivu ipasavyo (na wengi ilibidi wafe) ili kujenga nchi ,tena kipindi kile ilibidi pia wapigane vita vya dunia ambavyo walishinda. Kwa waliopata kuwa na marafiki warusi waulizeni nani alijenga zile metro bora kuliko zote duniani walizo nazo watawaambia.


  Hii na mingine mingi kwingineko ni mifano ya jinsi kiongozi (pamoja na kuwa na itikadi za kidikteta ambazo hazikubaliki) lakini anaweza kujenga nchi yake kwa kusimamia yale anayoona yatawanufaisha wananchi wake. Kwasababu matatizo ya uongozi Tanzania ni systemic, lazima yanawahusisha raia pia, hivyo ili kuondokana na tatizo hili, raia watanzania inabidi nao wabadilike kwa kuwa wazalendo, wenye vision, wafanye kazi, wapinge ubinafsi, ufisadi, udini na ukabila ili waweze kuwakataa viongozi wabovu. Ni kwa mtindo huu tu ambapo Tanzania inaweza kubadilika completely na watu wake kufaidi matunda ya raslimali tulizo jaliwa, no other way round. Kilichobaki kwa Tanzania ya sasa ni individual struggles za mtanzania mmoja mmoja kujitaftia mkate wake kila kukicha (kwa maskini na mwenye nacho), watu wamejikatia tamaa na hawaitegemei serikali yao, it’s a real pathetic situation. Tutafakari……….
   
 2. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  EL anafaa sifa hizo kwa ccm ukiacha ushabiki wa kisiasa
   
 3. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lowassa anafaa kiukweli jamb ni dikteta kimtindo anauwezo wa kuisukuma nchi sehemu moja mpaka nyingine
   
 4. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kuhusu EL sikubaliani na ninyi kwani yule jamaa hana sifa za uongozi. Yule fisadi, hana uzalendo-fikiria kashifa alizonazo yeye na familia yake kuhusu mali ya umma na hata maafiki zake wakuu ni kigezo tosha cha kutoqualify i.e. RA, AC etc.
   
 5. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wapo watu kama Magofuli, mrema, mwakyembe, Dr. Slaa na wengine
   
 6. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  EL hafai ni Mchafu,ananuka ufisadi kila sehemu wapo wachache wanafaa
   
Loading...