Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

tumuombe mwenyezi Mungu ampe hekima na busara mama yetu atuongoza kwa haki..

Mama akichukua mazuri ya JK na mazuri ya JPM akatuongoza basi nchi itapiga hatua haraka.. JK alikuwa na akili na mtazamo wa dunia ya sasa inavyotaka kufikia kwenye maendeleo, JPM alikuwa ni msimamizi na muangalizi mzuri kwenye rasimali na utendaji.. Mama akichukua vyote akavitumia kama silaha tutakwenda mbele...

Tatizo la CCM ni makundi, haya makundi ndio yanaweza kuwa kikwazo kwa mama, makundi yameota mizizi mpaka taasisi nyeti na kila kukicha yanaibuka makundi mapya..Ni wakati sasa wa viongozi wa haya makundi kuweka maslahi ya Taifa mbele na kuachana na minyukano yao...
Paragraph ya mwisho ni nzito sana
 
Ukiyaangalia haya mambo kwa jicho la pili, ni kama wale waliokuwa wakipigania Magufuli kuongezewa muda, wameshinda. Sababu Magufuli ataendelea kutawala beyond 2025 ila sasa akiwa ndani ya Mama Samia Suluhu.
 
yeah Ilani na ajenda ni ile ile... mengine uliyosema ni kweli. Unless kuna Ilani nyingine itapitishwa...
Elimu haina mwisho. Jaribu kujisomea zaidi maana inaonekana unaandika makala kwa kutumia experiences zaidi badala ya uhalisia na facts. . Dynamism kwa binadamu matters! Historia ya maraisi wa nchi hii inaonesha mara nyingi hakuna raisi anayezingatia sana focus/mtazamo wa mtangulizi wake.

Tambua kwamba Mhe Raisi Samia na Hayati JPM ni watu wawili tofauti sana kimtazamo katika masuala ya uongozi. Kitu kingine unatakiwa kujua ni kwamba Mhe Samia Suluhu Hassan ni Raisi wa JMT, hivyo halazimishwi kutumia mbuni za mtangulizi wake katika uongozi wake.
 
Ni imani kamba Mh Samia kafanya tofauti na mzee wa chato?

Mimi naona kwa macho yangu na ninasikia kwa masikio yangu kwamba rais wa sasa yupo vyema sana katika kuongoza wananchi wake zaidi ya milioni 60 tofauti na jamaa mkatili na mpenda sifa aliyepita wewe unanijibu eti ni imani!

Hivi unasoma na kuelewa kweli?
Ndugu utamuonea bure Mzee Mwanakijiji kachanganyikiwa kweli maskini hajui hata anachoandika.
Ni wakati sasa watu watoe sifa na utukufu kwa Mungu kuliko kumsifu binadamu aliyeumbwa na Mungu.

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
ina wauma Sana eehh Mtalia na kusaga meno mwaka huu

Nikweli Tanzania ya Samia ni ya magufuli yule yule ndio maana Jana kwa mara ya Kwanza tangu serikali hii ya awamu ya 5 iingie madarakani tumeona mkuu wa mamlaka ya bandari amesimamishwa kaI kwa tuhuma za ufisadi

Takukuru nao wameambiwa waache kujihusisha na kesi zisizo wahusu

Pia Raisi wa nchi kaagiza haraka Sana kesi zisizo na kichwa Wala miguu walizo bambikiwa watu kuwa ni za uhujumu uchumi na uchochezi zifutwe haraka Sana zilikuwa zina haribu taswira ya nchi

Hapo vipi bado una teseka !?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Wale ndugu zetu waliombea, waliongojea, na hata waliosubiria Magufuli afariki akiwa madarakani leo wanataka tuendelee kuamini kuwa chaguo lao limeingia madarakani sasa. Ndugu zetu hawa ndio wale huko nyuma na si mara moja wamekuwa wakisubiria kwa hamu "kitu" kitokee ili "mama" aingie madarakani. Tunawakumbuka hawa jinsi walivyosubiria kwa hamu wakati ule huku wakiposti picha za Makamu wa Rais kuwa ni suala la muda tu. Kama nitakavyoonesha katika makala yangu ya wiki hii (Gazeti la Raia Mwema) kwa baadhi ya watu kifo cha Magufuli hakikuja kwa mshtuko kivile; watu waliombea kisije kutokea lakini uwezekano wake ulikuwa mkubwa zaidi kuliko watu wengi walivyokuwa wanafikiria. Kwamba, sasa Rais Magufuli amefariki dunia basi ujio wa Mama Samia kwa ndugu zetu ni kama sala, dua, na maombi yao yamejibiwa. Katika kushangilia na kufurahia kwao ndugu zetu sasa wamekaa 'mkao wa kula' wakitegemea kuwa ndoto zao zote za Tanzania ya Samia zitatimia kwani haitokuwa ya Magufuli tena!

Yule mbaya wao, yule adui yao, yule kiongozi ambao hawakumtaka hayupo tena na sasa ameingia waliokuwa wamemtaka. Ndugu zetu hawa kwa uzuri au kwa ubaya sasa wamefikia mahali ya kutoa maelekezo, maombi, manuio, na hata matamanio yao chini ya Samia. Wanamuambia afanye nini kwanza, wanataka amtumbue nani kwanza, wanataka aanzie wapi kwanza ili waweze kuamini kuwa yuko nao. Wengine kwa wazi kabisa wanasema - tena siyo kusema wanamtaka aachane na 'mambo' ya Magufuli na akifanya hivyo basi wanaahidi kumuunga mkono na kuwa naye pamoja. Kwamba, hawatamnanga kama walivyomfanyia Magufuli na kuwa watampima Samia kwa jinsi gani anaenda mbali na siasa, mwelekeo, malengo na ajenda ya Magufuli. Ndugu zetu wanataka Samia awe "Rais" wao.

Wameacha kujipanga na uchaguzi, hawataki tena kutengeneza ajenda yao itakayowashindia uchaguzi, na hawataki kupambana kisiasa kushindana na CCM nyuma ya Samia. Wanataka kutengeneza "mgombea" wao na kudandia ajenda mpya ya Samia. Kwa kweli, inabidi tuwarudishe kwenye mstari wao ili wajipanga na kupambana na hali zao. Ajenda ya Samia bado ni ya Magufuli! Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, hana ajenda yake tofauti na ya Magufuli. Samia hajauza ajenda yake katika uchaguzi wowote na hajapigiwa kura ya peke yake nje ya Magufuli. Kwa maneno mengine ni kuwa - na yeye mwenyewe ameshaelezea wakati huu wa maombolezo - kuwa ajenda ya Magufuli ya "hapa kazi tu" ipo pale pale! Hili halijawafurahisha sana ndugu zetu kwani wanataka aikane ajenda ya mtangulizi wake, aibeze, aipangue na kuitupilia mbali kama yale mapapai yaliyoambukizwa korona! Samia achukue ajenda ya wapinzani na kutawala nayo nchi huku akitupilia mbali mambo yote ya Magufuli!

Hata hivyo, wananchi wametuma salamu zao wazi, kamili, na hadharani; wamemlilia Magufuli kwa sababu walimuelewa. Hawakujificha wala kuona haya kujitokeza kumuombolezea Rais wao na kumlilia. Walimuaga kama shujaa aagwavyo. Ndugu zetu hawakutarajia hili wala kulitegemea. Wanaamini ukosoaji wao ndio pekee umejaa ukweli, maneno yao ni ya kuaminika tu na madai yao ndiyo pekee yenye kukubalika. Hawatakiwi kupingwa wala kukataliwa kwani ukiwafanyia hivyo wewe si muumini wa demokrasia. Kwamba, demokrasia ni kukubali, kukumbatia na kutetea yote yasemwayo nayo. Kwamba njia pekee sahihi, bora na ya kukubalika ya kutawala nchi ni ile inayopendekezwa nao. Usipoifuata njia hiyo basi wewe ni hatari kwa maslahi yao.

Huu ndio mtego wanaomtegea Mama Samia; kwamba aingie kwenye anga zao vinginevyo hawatochelewa kumgeuka. Hawa hawa ambao leo wanamuita "ni mama yao" ndio hawa hawa watamgeuka na kuanza kutukumbusha "uzuri" wa Magufuli. Hawa hawa wenye kumsifia ndo hawa hawa watamshukia siku viongozi wao watakapotiwa pingu kwa makosa au watakapozuiliwa kufanya wavitakavyo. Hatokuwa tena Rais wao na walimuita Magufuli "Jiwe" hawa hawa wataanza kumuita mama huyo "Chuma" a.k.a "Iron Lady". Na Samia asipokaa nao na kuwasikiliza na kuwakubalia na kuwapa matakwa yao ndugu zetu hawa wataanza tena kuzunguka duniani kutuambia "Yule Mwanamke Hawezi Kutawala Tanzania Angalau Magufuli...".

Bahati nzuri tupo ambao bado tunaamini ajenda ya Magufuli bado ni ajenda yenye nguvu, ya uhakika, na salama zaidi kwa Tanzania kupiga hatua ya haraka ya maendeleo. Kuiacha ajenda hiyo ni kuwaacha Watanzania zaidi ya asilimia 80 pembeni. Kuiacha ajenda hiyo itakuwa ni kuirudisha nchi yetu nyuma miaka ishirini na ushee. Na ni wazi kuiacha ajenda hiyo ni kukubali kushindwa. Samia akiacha ajenda ya Magufuli wapo wenye Wana-Magufuli (Pro-Magufuli) ambao nao watamuacha. Lakini hata yeye akiamua kuiacha haina maana hakuna watu walioiona na kuikubali ajenda hiyo ambao wanaweza kuisimamia na kuifufua huko mbeleni. Aliyekufa ni Magufuli na si ajenda yake ya "Tanzania Tunaweza". Samia akilirudisha taifa katika kuombaomba na kutokujiamini tena, akilirudisha taifa katika kujishukushuku basi Tanzania itaenda kuwa katika ubaya kuliko tunaoufikiria.

Tunapozungumzia ajenda ya Magufuli tusichanganye na namna Magufuli alivyotaka kuitekeleza ajenda hiyo. Samia asiwe kama Magufuli; hatutaki azungumze kama Magufuli au afanye kila kitu kama Magufuli. Kila mtu ameumbwa tofauti na ana hulka tofauti. Mama Samia anaweza kuitekeleza na kuipeleka mbele Tanzania bila kufanya kila kitu kama Magufuli. Na hapa ni muhimu Mama Samia awaweke sawa wote; wale wanaoombea asiwe kama Magufuli na wale ambao wanataka awe zaidi ya Magufuli; ni lazima atengeneza njia yake mwenyewe bila kufunikwa na kivuli cha Magufuli wala kujaribu kuvaa viatu vyake. Ni lazima awaweke sawa wale wanaotaka achague Makamu wa Rais ambaye ataweza kufanya naye kazi, atakayeweza kumuamini, na ambaye likitokea lolote basi anaweza kuishikilia nchi. Na muhimu zaidi ni lazima awe mtu ambaye aliamini katika ajenda ya Magufuli na si NJE ya hapo. Mama Samia awe huru kumteua Makamu wa Rais anayeweza kushirikiana naye na kusimama naye; kuwa msiri wake, na afanye hivyo bila kuangalia Jinsia au Dini ya mtu huyo na kwa maoni yangu ni lazima awe mtu ASIYEUTAKA URAIS au aliyewahi kuonesha kiu na hamu ya kuwa Rais.

Kama nilivyosema hapo juu ajenda ya Magufuli ndiyo inaongoza nchi hadi 2025. Kama Mama Samia au MwanaCCM yeyote mwingine ana ajenda nyingine basi huyo ajiandae 2025. Mama Samia anaweza kuwa na ajenda yake; lakini hiyo itabidi aiandae 2025 (na wengine tayari tupo nyuma yake kwani tayari tunamuaini kwa vile tu alikuwa nyuma ya Magufuli). Kwa sasa hata hivyo, yeye na uongozi mzima wa nchi unatakiwa kuendelea na ajenda ya Magufuli. Na ili afanikiwe ni lazima ipange serikali yake kwa namna yake yeye na jinsi anavyoweza kuona inamfaa kuongoza nchi kuelekea 2025. Si lazima arithi na kuendelea na kila kiongozi aliyeteuliwa na Magufuli; wale ambao anaona wanapwaya au tayari walishaona wanapwaya ni lazima AWAPANGUE bila aibu. Sasa hivi ni lazima atume ujumbe wa haraka kuwa HAKUNA aliyesalama kwenye cheo chake; kila mtu ni lazima astahili kuwepo kwenye serikali yake. Na katika kufanya hivyo ndio anaweza KUSAHIHISHA makosa ya Magufuli, kujenga katika MAFANIKIO yake na kuongoza kuelekea MALENGO yote yaliyokuwa yanawezekana chini ya AJENDA YA MAGUFULI.

Hii ni kwa sababu AJENDA YA SAMIA ni bado AJENDA YA MAGUFULI hadi 2025.

#TukonaSamia2025.
Nimesoma mpaka katikati naona pumba tu.
 
yaani, unafikiri kuna mtu anaweza kunituma kuandika kitu? yaani wiki hii tu tayari mmejua hakuna tena ubabe au kutishana maisha... ngoja awageuka mtamsemaaaa...
Hawa jamaa ni wajinga sana jamani!

Yani sasa hivi kama ikitokea tupige kura leo ccm inaweza kupata ushindi wa 99%

Hawa mimi huwa nasema ni kuwaacha tu, akili zao huwa zinarudi mwezi oktoba ya kila mwaka wa 5 wa uchaguzi
 
Mh.Rais mama Samia anajulikana toka akiwa m/kiti wa binge la katiba ni mtu wa Fairness. Anapenda haki.

Anaeona hana tofauti na Jiwe atasubiri sana meli ubungo.
Rais Samia hawezi kufanana na Magu.

Ni either atakuwa bora kuliko Magu au mbovu.

Lakini hawawezi kabisa kufanana. Dunia haiko hivyo.

Marais wote wametoka CCM lakini hawajawahi kufanana hata kidogo.

Na kama Samia anataka kupata tabu, na yeye ajifanye anataka kuwa Magufuli number 2.

Urais ni miaka 9, asihangaike kuishi kwenye fikra za mtu juha.

Awe Rais Samia kwa 100%.

It's time to build her own legacy.

Jambo kubwa la msingi kwasasa ni Utawala wa sheria, haki, utu na UBINADAMU.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Wale ndugu zetu waliombea, waliongojea, na hata waliosubiria Magufuli afariki akiwa madarakani leo wanataka tuendelee kuamini kuwa chaguo lao limeingia madarakani sasa. Ndugu zetu hawa ndio wale huko nyuma na si mara moja wamekuwa wakisubiria kwa hamu "kitu" kitokee ili "mama" aingie madarakani. Tunawakumbuka hawa jinsi walivyosubiria kwa hamu wakati ule huku wakiposti picha za Makamu wa Rais kuwa ni suala la muda tu. Kama nitakavyoonesha katika makala yangu ya wiki hii (Gazeti la Raia Mwema) kwa baadhi ya watu kifo cha Magufuli hakikuja kwa mshtuko kivile; watu waliombea kisije kutokea lakini uwezekano wake ulikuwa mkubwa zaidi kuliko watu wengi walivyokuwa wanafikiria. Kwamba, sasa Rais Magufuli amefariki dunia basi ujio wa Mama Samia kwa ndugu zetu ni kama sala, dua, na maombi yao yamejibiwa. Katika kushangilia na kufurahia kwao ndugu zetu sasa wamekaa 'mkao wa kula' wakitegemea kuwa ndoto zao zote za Tanzania ya Samia zitatimia kwani haitokuwa ya Magufuli tena!

Yule mbaya wao, yule adui yao, yule kiongozi ambao hawakumtaka hayupo tena na sasa ameingia waliokuwa wamemtaka. Ndugu zetu hawa kwa uzuri au kwa ubaya sasa wamefikia mahali ya kutoa maelekezo, maombi, manuio, na hata matamanio yao chini ya Samia. Wanamuambia afanye nini kwanza, wanataka amtumbue nani kwanza, wanataka aanzie wapi kwanza ili waweze kuamini kuwa yuko nao. Wengine kwa wazi kabisa wanasema - tena siyo kusema wanamtaka aachane na 'mambo' ya Magufuli na akifanya hivyo basi wanaahidi kumuunga mkono na kuwa naye pamoja. Kwamba, hawatamnanga kama walivyomfanyia Magufuli na kuwa watampima Samia kwa jinsi gani anaenda mbali na siasa, mwelekeo, malengo na ajenda ya Magufuli. Ndugu zetu wanataka Samia awe "Rais" wao.

Wameacha kujipanga na uchaguzi, hawataki tena kutengeneza ajenda yao itakayowashindia uchaguzi, na hawataki kupambana kisiasa kushindana na CCM nyuma ya Samia. Wanataka kutengeneza "mgombea" wao na kudandia ajenda mpya ya Samia. Kwa kweli, inabidi tuwarudishe kwenye mstari wao ili wajipanga na kupambana na hali zao. Ajenda ya Samia bado ni ya Magufuli! Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, hana ajenda yake tofauti na ya Magufuli. Samia hajauza ajenda yake katika uchaguzi wowote na hajapigiwa kura ya peke yake nje ya Magufuli. Kwa maneno mengine ni kuwa - na yeye mwenyewe ameshaelezea wakati huu wa maombolezo - kuwa ajenda ya Magufuli ya "hapa kazi tu" ipo pale pale! Hili halijawafurahisha sana ndugu zetu kwani wanataka aikane ajenda ya mtangulizi wake, aibeze, aipangue na kuitupilia mbali kama yale mapapai yaliyoambukizwa korona! Samia achukue ajenda ya wapinzani na kutawala nayo nchi huku akitupilia mbali mambo yote ya Magufuli!

Hata hivyo, wananchi wametuma salamu zao wazi, kamili, na hadharani; wamemlilia Magufuli kwa sababu walimuelewa. Hawakujificha wala kuona haya kujitokeza kumuombolezea Rais wao na kumlilia. Walimuaga kama shujaa aagwavyo. Ndugu zetu hawakutarajia hili wala kulitegemea. Wanaamini ukosoaji wao ndio pekee umejaa ukweli, maneno yao ni ya kuaminika tu na madai yao ndiyo pekee yenye kukubalika. Hawatakiwi kupingwa wala kukataliwa kwani ukiwafanyia hivyo wewe si muumini wa demokrasia. Kwamba, demokrasia ni kukubali, kukumbatia na kutetea yote yasemwayo nayo. Kwamba njia pekee sahihi, bora na ya kukubalika ya kutawala nchi ni ile inayopendekezwa nao. Usipoifuata njia hiyo basi wewe ni hatari kwa maslahi yao.

Huu ndio mtego wanaomtegea Mama Samia; kwamba aingie kwenye anga zao vinginevyo hawatochelewa kumgeuka. Hawa hawa ambao leo wanamuita "ni mama yao" ndio hawa hawa watamgeuka na kuanza kutukumbusha "uzuri" wa Magufuli. Hawa hawa wenye kumsifia ndo hawa hawa watamshukia siku viongozi wao watakapotiwa pingu kwa makosa au watakapozuiliwa kufanya wavitakavyo. Hatokuwa tena Rais wao na walimuita Magufuli "Jiwe" hawa hawa wataanza kumuita mama huyo "Chuma" a.k.a "Iron Lady". Na Samia asipokaa nao na kuwasikiliza na kuwakubalia na kuwapa matakwa yao ndugu zetu hawa wataanza tena kuzunguka duniani kutuambia "Yule Mwanamke Hawezi Kutawala Tanzania Angalau Magufuli...".

Bahati nzuri tupo ambao bado tunaamini ajenda ya Magufuli bado ni ajenda yenye nguvu, ya uhakika, na salama zaidi kwa Tanzania kupiga hatua ya haraka ya maendeleo. Kuiacha ajenda hiyo ni kuwaacha Watanzania zaidi ya asilimia 80 pembeni. Kuiacha ajenda hiyo itakuwa ni kuirudisha nchi yetu nyuma miaka ishirini na ushee. Na ni wazi kuiacha ajenda hiyo ni kukubali kushindwa. Samia akiacha ajenda ya Magufuli wapo wenye Wana-Magufuli (Pro-Magufuli) ambao nao watamuacha. Lakini hata yeye akiamua kuiacha haina maana hakuna watu walioiona na kuikubali ajenda hiyo ambao wanaweza kuisimamia na kuifufua huko mbeleni. Aliyekufa ni Magufuli na si ajenda yake ya "Tanzania Tunaweza". Samia akilirudisha taifa katika kuombaomba na kutokujiamini tena, akilirudisha taifa katika kujishukushuku basi Tanzania itaenda kuwa katika ubaya kuliko tunaoufikiria.

Tunapozungumzia ajenda ya Magufuli tusichanganye na namna Magufuli alivyotaka kuitekeleza ajenda hiyo. Samia asiwe kama Magufuli; hatutaki azungumze kama Magufuli au afanye kila kitu kama Magufuli. Kila mtu ameumbwa tofauti na ana hulka tofauti. Mama Samia anaweza kuitekeleza na kuipeleka mbele Tanzania bila kufanya kila kitu kama Magufuli. Na hapa ni muhimu Mama Samia awaweke sawa wote; wale wanaoombea asiwe kama Magufuli na wale ambao wanataka awe zaidi ya Magufuli; ni lazima atengeneza njia yake mwenyewe bila kufunikwa na kivuli cha Magufuli wala kujaribu kuvaa viatu vyake. Ni lazima awaweke sawa wale wanaotaka achague Makamu wa Rais ambaye ataweza kufanya naye kazi, atakayeweza kumuamini, na ambaye likitokea lolote basi anaweza kuishikilia nchi. Na muhimu zaidi ni lazima awe mtu ambaye aliamini katika ajenda ya Magufuli na si NJE ya hapo. Mama Samia awe huru kumteua Makamu wa Rais anayeweza kushirikiana naye na kusimama naye; kuwa msiri wake, na afanye hivyo bila kuangalia Jinsia au Dini ya mtu huyo na kwa maoni yangu ni lazima awe mtu ASIYEUTAKA URAIS au aliyewahi kuonesha kiu na hamu ya kuwa Rais.

Kama nilivyosema hapo juu ajenda ya Magufuli ndiyo inaongoza nchi hadi 2025. Kama Mama Samia au MwanaCCM yeyote mwingine ana ajenda nyingine basi huyo ajiandae 2025. Mama Samia anaweza kuwa na ajenda yake; lakini hiyo itabidi aiandae 2025 (na wengine tayari tupo nyuma yake kwani tayari tunamuaini kwa vile tu alikuwa nyuma ya Magufuli). Kwa sasa hata hivyo, yeye na uongozi mzima wa nchi unatakiwa kuendelea na ajenda ya Magufuli. Na ili afanikiwe ni lazima ipange serikali yake kwa namna yake yeye na jinsi anavyoweza kuona inamfaa kuongoza nchi kuelekea 2025. Si lazima arithi na kuendelea na kila kiongozi aliyeteuliwa na Magufuli; wale ambao anaona wanapwaya au tayari walishaona wanapwaya ni lazima AWAPANGUE bila aibu. Sasa hivi ni lazima atume ujumbe wa haraka kuwa HAKUNA aliyesalama kwenye cheo chake; kila mtu ni lazima astahili kuwepo kwenye serikali yake. Na katika kufanya hivyo ndio anaweza KUSAHIHISHA makosa ya Magufuli, kujenga katika MAFANIKIO yake na kuongoza kuelekea MALENGO yote yaliyokuwa yanawezekana chini ya AJENDA YA MAGUFULI.

Hii ni kwa sababu AJENDA YA SAMIA ni bado AJENDA YA MAGUFULI hadi 2025.

#TukonaSamia2025.
Bandiko refuuu, unapiga ramli.
Unajivunjia heshima tu mkuu.
Hata Kama mwanao atafanana na wewe haiwezi kwa100%
 
Back
Top Bottom