Tanzania ya pili duniani kwa vivutio asilia vya utalii, tulikwama wapi?

Unajua mtanzania analipa shs ngapi kuingia national park na mtu asiye mtanzania analipa shs ngapi?

Ukijua Hilo huwezi beza jitihada za kujitangaza nje

..sijabeza jitihada za kujitangaza nje.

..ninachoshauri mimi ni kwamba jitihada za kujitangaza nje, ziende sambamba na jitihada za kuwezesha ongezeko la watalii wazawa.

..tujiwekee malengo kwamba ktk miaka 10 ijayo wazawa wawe 50% ya watalii wanaotembelea vivutio vyetu.
 
Ukiangalia dubai mbinu zao za kujitangaza ni za hali ya juu sana. Wana majina yao kwenye viwanja na jersey za Arsenal, AcMilan, wanajitangaza kwenye TV stations nyingi za Ulaya, US, on google, billboards, kwenye magazeti, competitions ukishinda unaenda holiday bure.

Umuhimu wake unawafanya watake kujua, kujifunza na kutembelea zaidi kuhusu nchi husika na vivutio vyake.

Hata Kenya wametupita kwenye kujitangaza.



Unaongea vitu genuine Sana wewe jamaa
 
..sijabeza jitihada za kujitangaza nje.

..ninachoshauri mimi ni kwamba jitihada za kujitangaza nje, ziende sambamba na jitihada za kuwezesha ongezeko la watalii wazawa.

..tujiwekee malengo kwamba ktk miaka 10 ijayo wazawa wawe 50% ya watalii wanaotembelea vivutio vyetu.


Mzawa akaangalie nini?? Tembo au swala, ujue utalii ni hobby bro, -- mtu mlo wake wa siku shida, tozo na kodi kibao, ada za hospitali na za shule nk, atapata wapi pesa ya kutalii.

Nature ya mzungu ni Curiosity katika mambo mengi na utalii ni moja ya Curiosity., Mwafrika naturally is not curious, one of the factors which enhances our underdevelopements is lackal of curiosity.
 
Rais Samia ni mnyenyekevu | Mpole| anastaha | mpenda watu, | Mpenda maendeleo | mchamungu | Mzalendo wa kweli
 
Hao hao chini ya milioni moja wanatosha ,ulizia hao kiduchu hela yao inayokusanywa ni kiasi gani ndio utaona kama hii nchi ina mashimo mengi ya panya buku.
 
Mzawa akaangalie nini?? Tembo au swala, ujue utalii ni hobby bro, -- mtu mlo wake wa siku shida, tozo na kodi kibao, ada za hospitali na za shule nk, atapata wapi pesa ya kutalii.

Nature ya mzungu ni Curiosity katika mambo mengi na utalii ni moja ya Curiosity., Mwafrika naturally is not curious, one of the factors which enhances our underdevelopements is lackal of curiosity.


Unaeleweka lakini karibu kila mkoa kuna sehemu ya Utali, kweli tunashindwa hata hivyo?
 
Unaeleweka lakini karibu kila mkoa kuna sehemu ya Utali, kweli tunashindwa hata hivyo?


Utalii ni hamasa iliyomo moyoni mwa mtu pamoja na umaskini wetu lakini pia sisi hatuna hamasa ya utalii, kumbuka kwamba kabla ya Wakoloni hawajafika huku Africa wazungu waliwatuma wapelelezi wao kwanza, kumbuka katika zama hizo za giza 1800s mtu anatumwa kuja Africa, Bara jipya kabisa kwao na mtu anajitoma kuja bila kujali hatari itakayomkuta; hii ndiyo nature ya hamasa ya moyoni ya kutalii na kutembea sehemu mbalimbali, hamasa hiyo Wazungu wanayo, baada ya hao wapelelezi kuja na kupeleka taarifa huko kwao kilichofuata unajua; kugawanywa kwa Africa na hatimaye ukoloni. Sisi Waafrica hatukutoka kwenda nje au hata ndani kutafuta makoloni kwasababu hatukuwa na bado hatuna hamasa ya kutalii, kutembea na hata kupeleleza mambo si tu ya kiuchumi bali hata kupeleleza/kutafiti mambo ya kisayansi.

Nimeandika hiyo historia kukazia kwamba Utalii ni jambo la moyoni au hobby ambayo sisi Waafrika wengi wetu hatuna.
 
Wanasema gharama za kutalii tza ni kubwa sana gharama ya siku 1 moja TANZANIA ukienda Morroco unatalii wikii.
KILA kitu bei juu kwa mentality za kizamani za wazungu wanapesa.
 
Mama anatoa Tsh 23.8BL kwaajili ya elimu bure | Mimi Mama Samia hata akiongoza hadi 2035 ni poa to,
 
Ndani ya Uongozi wa Rais Samia,
Mahakama huru,
Bunge huru,
NGOs huru
Media huru

TanzaniakwaniSisi tunatakaje?
 
Mungu Ibariki Africa,
Mungu ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais Samia,

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
DUNIA INAJUMLA YA WATALI 1.5BL WANATAFUTA WAPI WAKALE BATA KILA MWAKA | TANZANIA NI YAPILI KWA VIVUTIO ASILIA DUNIANI TUNAPOKEA WATALI CHINI YA 1M, IKOJE HII!?

________________________________________

Niseme kidogo kuhusu Rais Samia na "Royal Tour. "Tanzania ni nchi ya Pili kwa Vivutio vya asili duniani baada ya Brazili. Tofauti na nchi zingine 80% ya Watali wote wanaozuru Vivutio vya Brazili ni Wabrazili. Ni watali 6.5m ndio wanatoka nje ya Brazili kwa mwaka. Mwaka 2018|19 Brazili ilijikusanyia kiasi cha $97.11BL karibu Tshs 215 trilioni kama mapato yatokanayo na Utali.

Fedha hii inaweza gharamia bajeti ya Serikali ya JMT kwa miaka 5 mfululizo tena bila ya Mtanzania yeyote kutozwa kodi|tozo,Namaanisha hadi Vyoo vya kulipia viwe bure.Je,tumewahi kujiuliza kwanini hawa Brazili wakusanye Tshs 215trilioni kwa mwaka na Sisi tukusanye Tshs 5.3trilioni kwa mwaka sawa na tofauti ya Tshs 210trilioni ili hali Sisi ni Wapili baada ya wao kwa Vivutio duniani, Yaani Kwanini Wao!!? Rais Samia Suluhu amekuja na jibu ambalo ni "Royal Tour Film " na hapa lazima tutambue Tanzania Kiutali haifahamiki kabisa duniani heri ya Bongo Zozo.

Leo kwa mwaka Tanzania inapokea watali chini ya 1m pamoja na utitiri wa Vivutio ilivyonavyo, Chaajabu Ufaransa inayoongoza kwa Utali duniani haina twiga wala Simba inamagofu na Mnara ( all are man-made ) lakini inaingiza zaidi ya watali 89m na €56.2BL kwa mwaka sawa na Tshs 154trilioni,Hivi kwa vivutio tulivyonavyo nikweli tumeshindwa kuinyanga'nya hata Watali 5m tu kwa mwaka waje Tanzania!? Lazima tufahamu duniani kwa Sasa Utali ni biashara kipaumbele na msitegemee nchi yeyote duniani kutangaza vivutio vyenu zaidi ya Sisi wenyewe kwa Platform hizi za " Royal Tour Film. " Tatizo la Uhaba wa watali Tanzania sio tu Corona hata "Ushawishi " pia uko chini, Kwaakili ya kawaida ni ngumu zaidi kwa Mtali anayefahamu "Nini Kipo Tanzania " aache kuja kumtazama nyumbu|tembo "Live " pale Serengeti aende kumtazama tembo wa kwenye michoro kule Versailles Ufaransa,

Siku Mungu akitupa walau watali 5m tu kwa mwaka nchi yetu itaingiza zaidi Tshs 10trilioni kama mapato yatokanayo na Utali, Pesa hii inakwenda moja kwa moja kwa wanachi kwa njia ya kuwahudumia Watali na serikali itapata kiasi kama tozo ya Utali, Nchi hii inaweza kuendeshwa kwa Utali tu kama tu dunia itafahamu "Nini Kipo Tanzania. " Zaidi ya 50% ya watali wanaofika Kenya kwa Utali wamevutiwa na Vivutio vilivyopo Tanzania, inauma Sana na lazima tumshukuru Rais Samia kwaajili ya "Royal Tour Film "

Mfano, Mwaka 2017|18 mapato yetu yatokanayo na Utali yalifikia $2.4BL sawa na Tshs 5.5trilioni wakati rekodi ya Watali ikiwa 2m,Lakini tunafahamu duniani kila mwaka kuna zaidi ya Watali 1.5bl wanatafuta wapi waende kula bata,Lakini Sisi Tanzania pamoja na kuwa Wapili kwa Vivutio tena vya asili duniani tunaambulia watali 2m tu,Nadhani kunasehemu tulikwama na ndio Sababu ya Mungu kumleta Rais Samia na yeye kutuletea "Royal Tour Film. "Mnaolalamikia gharama za Tour rudieni kusoma andiko hili,


.........Kazi iendele.........

Viva Tanzania |Viva Samia |Viva CCM

View attachment 1935888


C&P
Watalii hawaji mpaka demokrasia itakapotamalaki Tanzania. Chungu kumeza but ndiyo ukweli.

Watalii hawataongezeka hadi pale katiba mpya itakapoandikwa. Unadhani JK (ambaye alikuwa ana interact sana na watalii wakati ule akiwa rais) alikuwa mjinga kuanzisha mchakato wa katiba mpya?
 
Hivi unadhani Watalii wanapenda kila baada ya km 10 polisi wanawasimamisha na kuomba rushwa?

Hivi nani asiyeijua Serengeti dunia hii?

Au unadhani huko duniani hakuna mawakala wanaotafuta watalii kuja huku tz?

Sent using Jamii Forums mobile app

watu wengi sana hawajui serengeti, hata uku uku tanzania kuna watu hawaijui! hata huo mlima the same story, kutanganza ndo kunahitajika mengine yapo kawaida tu

- and on the same time preference znatafautiana kuna wengine wanapenda utalii kupanda milima tu haswa mirefu, wengine mambo ya kale tu huezi mpangia mtu
 
Watalii hawaji mpaka demokrasia itakapotamalaki Tanzania. Chungu kumeza but ndiyo ukweli.

Watalii hawataongezeka hadi pale katiba mpya itakapoandikwa. Unadhani JK (ambaye alikuwa ana interact sana na watalii wakati ule akiwa rais) alikuwa mjinga kuanzisha mchakato wa katiba mpya?


Kwani katiba hii hairuhusu watalii kuingia nchini?!
 
Kwani katiba hii hairuhusu watalii kuingia nchini?!
Ya sasa ni ya mapolisi....inaruhusu mapolisi kuwanyang'anya watalii mali zao pale IGP atakapojisikia kufanya hivyo.
Ni watalii wenye roho ya paka tu (ambao si wengi kama takwimu zinavyothibitisha) ndiyo wanaoweza kuja katikati ya mazingira kama haya!!
 
Mwanamke wa kwanza kuhutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa la 76 tangu tupate uhuru ni Mama Samia Suluhu Hassan,

We Proud on you Mama
_________________________

IMG-20210918-WA0036.jpg
 
Back
Top Bottom