Tanzania ya pili duniani kwa vivutio asilia vya utalii, tulikwama wapi?

Umeongea kitu cha msingi Sana, Wenye namba ya Mama mpelekeeni hii comment

QUOTE="Red Giant, post: 40207894, member: 73501"]
Nafikiri kila taasisi na kila mtu anatakiwa kushiriki kuendesha na kufaidika na biashara ya utalii. Hapo ndipo tutaukuza. Utalii isiwe kazi iliyohodhiwa na TANAPA na TTB tu
Good comment
 
Brazil kitu kingine kinachochangia wapate watalii wengi ni sex tourism na km mnavyojua brazil ilivyobarikiwa kuwa na wasichana warembo. Vidume vyenye uchu kila mwaka vinaenda kuchuja sehemu ambayo kupata mwanamke sio kitu kigumu

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Ata ukitangaza vip utalii tanzania kama huduma ziko vile vile usitegemee jambo jipya.Hapa kwetu wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kwa maana ya tour company na wakala mbalimbali wamefanya kazi kubwa sana yakuvitangaza vivutio tulivyonavyo pamoja nakutoa huduma kwa sehemu zao changamoto iko uko kwenye huduma zinazotolewa uko kwenye hivyo vivutio vyenyewe bado ni tatizo kubwa.

Kwa mfano TANAPA ndiye msimamizi wa hifadhi za Taifa ila hebu nenda kaangalie huduma zinazotolewa uko mahifadhini alafu uniambie kwa hali hiyo hao watalii wataongezekaje.kama unakutana na mtoa huduma ambaye hata kujieleza vizuri mbele ya mtanzania mwenzake ni changamoto vip kuhusu mtalii kutoka nje.

Kwahiyo matangazo yalitakiwa yaende sambamba na maboresho ya huduma husika na miundo mbinu yetu.Kinachofanyika sasa hivi ni kwamba wakishachukua fedha yako hawajali tena kiwango cha huduma utakacho pata.sasa kwa hali hiyo mambo lazima yawe vile yalivyo maana bado hatujawekeza vyakutosha kwenye hiyo sekta.
 
Are your sure watu wanavifahamu vivutio vilivyopo Tanzania?

Polisi kumsumbua Tour Operator kuna mzuiaje mtali kurudi tena...
Si kweli ufahamu wa vivutio vya utalii ni mkubwa huko nje, tatizo letu ni huduma na ubunifu, mapato ya utalii yanatokana na siku anazokaa mtalii kwenye nchi husika na akikaa siku nyingi ndivyo mapato yataongezeka.

Sasa sisi tunakosa ubunifu tunafikiri wageni wa utalii wote wanataka kuja kuangalia serengeti na kilimanjaro tu, tunasahau kuwa kuna cultural tourism pia!

Lakini kama ulivyosema kwenye andiko la msingi, Brazil inategemea zaidi utalii wa ndani kuliko wa nje, kwanini nasi tusijikite huko?
 
Brazil kitu kingine kinachochangia wapate watalii wengi ni sex tourism na km mnavyojua brazil ilivyobarikiwa kuwa na wasichana warembo. Vidume vyenye uchu kila mwaka vinaenda kuchuja sehemu ambayo kupata mwanamke sio kitu kigumu

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Inawezekana, kwani basi isiongoze Thailand ambako sex tourism ni kubwa kuliko Brazil?
 
Wazawa kula yenyewe shida wataweza kweli kutembelea vivutio vya utalii?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app

..Mosi, tunatakiwa tukuze vipato vya wananchi.

..Uchumi wa Kati uonekane kwenye mifuko na matumizi ya Mtanzania mzawa.

..Pili, tujenge UTAMADUNI wa Watz kusafiri kwa malengo ya kutalii.

..Lazima tuwe na wazawa ambao wanatamani kwenda Serengeti, Ruaha, Zanzibar, Kigoma, etc kwa ajili ya kutalii.

Cc mulwanaka
 
Utalii sio priority
kwa wTz wengi, watu wanakosa pesa ya chakula tena uambie watalii hiyo pesa haipo
Ni kweli kwa watu wa chini..lakini amini nakuambia hata hao wenye kipato cha unafuu ambacho kinawapa ziada ya kufanya utalii...hawafanyi hivyo kwa sababu si utamaduni wetu...ni kama alivyowahi sema hayati Nyerere wakati wa ile Arusha declaration.

kuwa yeye anashangaa wazungu wanatoka huko kuja kuangalia mamba! yeye hawezi fanya hivyo, lakini pamoja na hayo aliheshimu utalii. kwa hivyo hapa tunatatizo la sisi wenyewe kuona kama utalii sio kit muhimu sana.

Yaani kwenda sehemu kaka Saadan National Park kuangalia kasa wanataga mayai ufukweni, au kwenda kaole kuangalia Magofu na kupata historia kwetu ni upotezaji wa pesa na wala sio therapy! kama wanavyoona wenzetu!
 
Maelezo safi sana haya. Ungekuwa una exposure kidogo ungefahamu kuwa utalii ni sehemu ya hospitality industry. Na hilo ndilo tatizo la tanzania. Nchi haina uwezo wa kumudu watalii.

Nenda pale airport uone hao watalii wanavyopokewa kama vile wamekosea kuja bongo. Huduma ya taxi na uelewa wa taxi driver, huduma ya hoteli tazama maliwato ya hoteli za kawaida.

Msaada wa polisi njiani nk nk. Hayo ndiyo yaanze kwanza!!!
 
Ni kweli kwa watu wa chini..lakini amini nakuambia hata hao wenye kipato cha unafuu ambacho kinawapa ziada ya kufanya utalii...hawafanyi hivyo kwa sababu si utamaduni wetu...ni kama alivyowahi sema hayati Nyerere wakati wa ile Arusha declaration...
Mtzania gani wajuu kwa kipato atakae pendelea kutalii mkoani aliko zaliwa na kusomea badala ya kukwea pipa Dubai, London Johannesburg nk.....kuna vitu ni impossible kwa ss wazawa
 
Kama ni kweli natujuzwe ziko wapi pesa zinazoingia kwa kupitia visa applications na makato ya serikali katika mahoteli na huduma nyengine kama usafiri wa ndani wa meli na ndege? Tanzania mtalii ana bei yake tafauti kwenye vyombo vya baharini na anga! Ziko wapi pesa zooote hizo?
 
Mtzania gani wajuu kwa kipato atakae pendelea kutalii mkoani aliko zaliwa na kusomea badala ya kukwea pipa Dubai, London Johannesburg nk.....kuna vitu ni impossible kwa ss wazawa

..it is not impossible.

..tunatakiwa tu-promote utalii miongoni mwa wazawa.

..pia hili suala halitakiwa lifanyike kwa mtindo wa "zimamoto."

..tuanze kushawishi Watz wanaokwenda kula raha Dubai, J'Berg, nk baadhi ya utalii wao wafanyie hapa nyumbani.
 
Mtzania gani wajuu kwa kipato atakae pendelea kutalii mkoani aliko zaliwa na kusomea badala ya kukwea pipa Dubai, London Johannesburg nk.....kuna vitu ni impossible kwa ss wazawa
Mkuu sio lazima uende uliko zaliwa hii nchi imejaa historia ya kutosha, mfano tumesomeshwa mengi juu ya historia ya hii nchi kwanini mfano usitamani siku moja kwenda kuangalia jiwe alilokanyaga Mwanamlundi wa Usukumani na kuacha nyayo, kwanini usitamani kwenda kuona nyao inayosemekana ni ya binadamu wa kale zaidi kule Ngorongoro, kwanini usitamani kwenda Kigoma kuona ziwa refu kuliko yote Afrika na la pili Duniani, kwanini usitamani kwenda kule Udzungwa kuangali water fall ndefu kuliko zote Tanzania, na Nyani wanaopatikana Tanzania tu na si kwingine kokotte duniani? mambo ya kutamani kutalii hapa hapa Tanzania ni mengi sana na sio kukimbilia Dubai kuangalia Bujri Kharifa au ile Aquarium kubwa kabisa ambavyo vyote ni manmade, kwanini uone kwenda Eiffel Tower Ufaransa ni bora sana kuliko kwenda kuangalia magofu ya Kilwa, kwani uone kwenda beach za Ibisa Hispania ni bora kuliko kwenda beach za Zanzibar...mkuu ni utamaduni wa fikra tu!
 
Back
Top Bottom