Nchi ya Tanzania iliyotokana na muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 mwezi wa Aprili tarehe 26 imetawaliwa au kuongozwa na marais 5 au awamu 5 za urais. Katika awamu zote hizo tumeshuhudia awamu moja tu ya 2 ikiongozwa na mtanzania kutoka Zanzibar, ingawaje hilo si sehemu ya hoja ya andiko hili.
Mwalimu Nyerere aliongoza nchi ikiwa ndiyo imeoka kupata uhuru, uhuru uliopatikana chini ya uongozi wake. Kipindi cha utawala wa mwalimu, kilikuwa ni kipndi cha vuguvugu la kudai uhuru katika nchi nyingi za kiafrika. Hivyo ni kipindi ambacho Mwalimu alipata upinzani mkubwa sana kutoka nje na ndani ya nchi. Mwl amejaribiwa kupinduliwa zaidi ya mara 20. Pamoja na majaribio yote hayo, kipindi cha Mwalimu ndicho kipindi watanzania walikuwa na umoja, mshikamano na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yao. Vita ya Kagera ilikuwa ndiyo kielelezo kikuu cha uzalendo wa watanzania.
Bila kuwachosha, vipindi vya Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi, Ben Mkapa na Kikwetwe vilikuwa na changamoto zake ambazo angalau wananchi walikua na maisha yanayoeleweka, wanachi walikuwa na amani ya mioyo.
Kwa muda mfupi wa uongozi uliopo umedhihirisha kwamba kuna mdororo mkubwa wa uzalendo, furaha na amani ndani ya mioyo ya watanzania. Katika vipindi vyote vitano vya uongozi wa nchi hii, haijawahi tokea wananchi kwa wingi wao wakajitokeza kupiga kelele kwa maumivu yatokanayo na utawala wao.
Upinzani wa wakati wa Nyerere ulikuwa ni wa watu wachache ndani ya mfumo wa kiutawala lakini upinzani wa sasa ni wa wananchi dhidi ya utawala wa vitisho, hotuba zenye maneno mengi huku utekelezaji ukiwa hafifu, matamko, makatazo, uzuiaji wa ajira, uhamisho, kupanda vyeo na madaraja.
Awamu hii imetokea kuchokwa mapema mnoo kuliko awamu zilizotangulia. Mara zote NIA hudhihirishwa na MATENDO. Unaposema hutaki wezi wa vyeti basi uhakikishe kweli wezi wa vyeti wanachukuliwa hatua bila upendeleo.
Awamu hii ndiyo iliyochokwa mapema kuliko zote.