Tanzania ya Majimbo, nini hatima ya maendeleo ya majimbo ambayo bado yako nyuma na yana uhaba wa rasimali?

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
5,154
2,000
Leo hii Kenya inakimbia kwa kasi kwasababu ya County Government, sisi tumekalia mikoa kama vile tupo vitani

Mikoa inaminya uwakilishi, uwajibikaji, ushiriki, maamuzi na maendeleo ya watu...
Mikoa huleta utumwa, ujinga, ubaguzi na kujipendekeza...
Mikoa huleta udumavu na umasikini...
 
CHAZA

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
7,972
2,000
Ni ukweli mtupu! Karibia maswali yote ya mtoa mada ni ya kijinga na kitoto! Yamejaa hofu tu ya kuhisi kukosa ulaji hasa kwa vyeo vya kupeana, vilivyopitwa na wakati na tulivyorithi kwa Wakoloni kama vile vya Ukuu wa Wilaya na Mkoa!

Kwa Nchi iliyobarikiwa kama Tanzania, kuna eneo ambalo halina raslimali kweli kiasi cha kuwa mzigo kwa maeneo mengine? Kama lipo naomba litajwe hapa jukwaani!

Taifa kubwa duniani la Marekani linatumia mfumo wa Majimbo, na limepiga hatua kweli kweli ya kimaendeleo!

Sisi huku wanasiasa uchwara wa CCM wanatisha Wananchi mbumbumbu eti mfumo wa Majimbo utaleta mgawanyiko na kuondoa Umoja tulio nao!

Mbona Wamarekani ni Wamoja! Na hata wanapokuja huku, tunawatambua kwa Umarekani wao, na si kutokana na Majimbo watokayo?

Watanzania tukubali kubadilika. Tukiendelea kuifanya siasa kuwa kipaumbele chetu na kuwaacha wanasiasa hasa wa CCM kutuamulia kila kitu kwenye maisha yetu, basi ni wachache tu watao endelea kuifaidi keki ya Taifa huku wengi tukitaabika.

Bado ninaukumbuka sana Mchakato wa Katiba ya Wananchi namna ulivyotekwa na kuwa mali ya Wanasiasa na mwisho wa siku kupotelea kusikojulikana.
Muuliza swali nae ana hoja. Lakini Tanzania tukiwa na rafiki kama China, nae ana mfumo wa majimbo na anaendelea kusonga mbele kiuchumi. Lililo la msingi ni kuwa uwe mfumo wa sasa au uwe mfumo wa majimbo, lililo la msingi ni kuweka utararibu.
Kwa mfano kwa sasa majukumu ya serikali za mitaa kama yangezingatiwa hayapishani sana na sera za majimbo. Swali ni je serikali za mitaa zina majukumu gani, zinatimiza?
 
CHAZA

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
7,972
2,000
Kwanza huyo ulimuunga mkono kaandika andiko lefu lakini hajui lolote. Usa sio majimbo yaliyogawanywa. Bali ni states zilizoungana, ukija nchi kama Kenya au nigeria mendeleo ya jimbo moja au lingine ni tofauti tusidanganyane. Hata Usa ni hivyo hivyo. Huwezi kusema utajiri uliopo Chicago ni sawa na New york.

Kwa nchi kama Tanzania wanachokitaka chadema hakina mantiki. Kwani mpaka hivi sasa hakuna serikali za majimbo nini kimekwama katika kutawala na kuleta maendeleo?
Je hoja hiyo, kwa sasa utajiri uliopo Morogoro ni sawa na utajiri uliopo Arusha kwa hali hii ya sasa ya mikoa?
Sidhani kama suala la kubalnce uchumi kila jimbo na kwa sasa kila mkoa ni tatizo, tatizo kubwa ni jinsi ya kugawanya sawa rasilimali. Mkoa/ jimbo lenye hali mbaya linatakiwa kuboostiwa ili kutoachwa nyuma. Hali ya jimbo/mkoa mmoja kurundikiwa cake kubwa huku baadhi ikiwa hoi kiuchumi nadhani hadi sasa hatujaweza kubalnce. Kwa ufupi ikifanyika balance, iwe kwa sasa mfumo wa mikoa au kama hilo la majimbo, cha msingi ni kuweka MIZANIA iliyo sawa, yule aliyeko nyuma asiachwe!
 
Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,534

Huna akili we bwege. Unajua maana ya kuwa na serikali za majimbo? Hiyo mizania utaiweka vipi? Mfano Kenya, Nairobi county isaidie maendeleo Garissa kwa mizania ipi? kama serikali ni moja kufanya diversifivation of economy ni rahisi kuliko unapokuwa na serikali za majimbo.
 
mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,031
2,000
Kama nchi haizalishi hata uje na mfumo gani wananchi watabaki maskini.

Nani amekwambia haizalishi inazalisha lakini hakuna motisha ya kuzalisha sababu matumizi anaamuwa mtu mmoja bila kushirikisha wananchi kwa hiyo anakuwa na vipaumbele vyake peke yake. Ndiyo sababu wananchi wanazidi kuwa masikini wakutupwa.
 
mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,031
2,000
Ni sera fulani ambayo msingi wake ni hulka za kichoyo na kibinafsi za hao walioibuni na kuiweka katika makaratasi.

Kwao binti aliyeolewa na mtoto wao wa kiume huwa hana faida baada ya mtoto aliyemuoa kuwa amefariki dunia, atafungashiwa virago akionekana hana tena sababu ya kuwepo pale nyumbani.

Ni sera ya kibaguzi isiyo na misingi ya utu isiyofundisha umuhimu wa kuvumiliana kama taifa.

Ni sera isiyo na upendo yenye fikra kwamba kila mtu aishi mpaka afe kivyake.

Inakuwaje sera inayotaka wananchi waamuwe kuhusu namna ya kujiletea maendeleo yao useme ya kibaguzi. Ubagusi ni huu unaofanywa sasa wakuchukuwa pesa za korosho na kwenda kujengea uwanja chato kwa sababu ni kwenu huo ndiyo ubaguzi ambao kwenye seriakali ya majimbo hauwezi kuwa na nafasi.

Au ule wa kukusanya kodi ya wananchi na kukataa kuwapelekea maendeleo kwa sababu wananchi walichagua upinzani huo ni ubaguzi mbaya sana ambao kwenye seriakali za majibu hauwezi kuwa na nafasi.

Ubaguzi ni pale pesa inapokusanywa kuwekwa kwenye mfuko Mkuu wa seriakali halafu mtu mmoja anajihomlea trillion 1.5 kwa ajiri ya kampeni zake binafsi za uchaguzi na kuwaacha wananchi wanahangaika kudai nyongeza ya mishahara yao bila mafanikio. Huo ndiyo ubaguzi ambao hautakiwi.
 
ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
5,421
2,000
Sijasoma hata mada yako maana heading tu inaonesha hauko informed.Kwa Tzn hapa hakuna Kanda ambayo ina uhaba wa rasilimali,imagine Burundi ina ishi sembuse majimbo ya Tzn.
Akili zako mtoa mada ni unadhani rasilimali kwako ni madini,gesi na bandari,unasahau kwamba hata Geografia ya sehemu ni rasilimali tosha.Kabla sijajibu swali lako tujiulize mbona kwa system ya mikoa Bado Kuna mikoa iko nyuma ya mingine,tatizo ni rasilimali? Tujiulize tena Leo hii Singida town iliyokuwa mji mdogo umekua na kuendelea kuzidi hata Songea,Sumbawanga,Shinyanga,Kigoma na Lindi,kwamba hiyo mikoa niliyotaja haina rasilimali kuzidi Singida? Kwa Nini iko nyuma ilhali mingine ina gas ,bahati/ziwa nk nk? Jibu ni moja location ya sehemu ni rasilimali tosha .
Kujibu swali lako angalia wanachofanya Ujerumani kuzusogeza mbele majimbo yaliyokuwa Ujerumani mashariki ili yafanane na Ujerumani magharibi,hivi ndivyo itafanyika
 
mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,031
2,000
Kenya inakimbia wapi?
Sasa Kenya walianzisha majimbo kwa sababu ya ukabila.

Ami I usiamini hizo ni mbinu za kuombea kura, Ila hata Lissu mwenyewe hataweza kufanya hicho kitu.

Sasa unajilinganisha na kenya kwa kitu gani hasa Bandari yao ya Mombasa ni zaidi ya mara mbili ya Bandari Dar es Salaam mapato yanayokusanywa na KRA ni mara tatu ya mapato yanayokusanywa TRA kwa mwaka halafu unabeza bila hata takwimu ukiambiwa unaongea hewa tu unakataa.

Sasa Kenya inazo rasilimali za kuishinda Tanzania, kwanini sasa ina maendeleo kuliko tanzania sababu ya mfumo mzuri wa utawala. Tanzania kila siku tunajisifia ni nchi tajiri sana wakati wananchi wetu ni masikini wankutupwa sababu ya kutoshirikishwa kwenye maamuzi ya matumimizi ya rasilimali zao.

Hatuwezi kuendelea na sera hizo hizo kila mwaka na kutegemea kupata matokeo tofauti. Ati kila mwaka mkichagua CCM itawajengea shule itawajengea hospital itawaletea maji itawajengea reli siju nini nini lakini baada ya miaka 59 bado maadui zetu ni wale wale umasikini, ujinga na maradhi na tunasema nchi yetu ni tajiri.

Huu ujinga sijui utatutoka lini na kubadilika kufikiria namna ya kuondokana na huu mfumo wa kutufanya masikini. Sasa kama kuna seriakali kuu si ndiyo itasaidia hayo majimbo yasiyo na rasilimali. Lakini ni jimbo gani lisilo na rasilimali hapa tanzania. Tuache kuwa wajinga na kuogopa mabadiliko bila sababu.
 
Kambulanga

JF-Expert Member
Jun 1, 2020
221
225
Nimesikia, nimetafakari sipati jibu la kuigeuza Tanzania iwe ya Majimbo, anavyonadi Lissu, mgombea Urais wa CHADEMA. Anadai, kurudisha utawala wa majimbo utawapa wananchi wa majimbo hayo mamlaka ya kuchagua viongozi wao, kupanga maendeleo yao (miundo mbinu na huduma za jamii).

Je, Utaifa uliojengwa na Baba wa Taifa ndio tuuzike rasmi?

Je, jukumu la Mihimili mitatu ya Dola (Serikali, Bunge na Mahakama) litakuwa ni lipi?

Je, nini itakuwa hatima ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Je, ni nini hatima ya maendeleo ya majimbo ambayo bado yako nyuma na yana uhaba wa rasimali maliasili na miundo mbinu isiyo bora?

Je, ni kwa vipi pato la Taifa litagawanywa?

Maswali ni mengi yakihitaji majibu. Kwako Lissu na CHADEMA
Sera ya majimbo ni Sera rasmi ya jinsi gani ya kuiuza nchi kwa mabeberu
 
ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
5,421
2,000
Kama nchi haizalishi hata uje na mfumo gani wananchi watabaki maskini.
Nchi haizalishi kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala ambao umejikita kwenye itikadi za kijamaa.Mfumo wa majimbo ni Kama mfumo wa ubepari yaani unareward wale wenye ufanisi.Nchi zote duniani zinatumia hii system sio tunagandamizana kisa fulani hapendi.
 
mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,031
2,000
Nakubaliana na wewe Phillipo. Hivi sasa baada ya miaka mingi ya uhuru kune sehemu zimeendelea kuliko nyingine kwa kutumia pato la Taifa. Mfano Shinyanga pamoja na kuzalisha pesa nyingi kwa almasi na dhahabu haijaendelea ukilinganisha na Moshi. Sasa haiingii akilini kwamba sasa Moshi hawataki kuchangia maendeleo y a Shinyanga kwa kujitenga katika mfumo wa majimbo. Kweli kabisa huu ni ubaguzi. TL anataka ma RC na DC wachaguliwe; hii inaleta ukabila kabisa maana hivi Msukuma anaweza kuchagulika kuwa RC au DC Moshi. Mfumo wa sasa unaruhusu mtu yeyote kuwa RC au DC popote; jambo ambalo linaleta utaifa. Kwenye mandeleo nchini kwetu tuende pamoja kwa kugawa pato la Taifa bungeni. Akina TL wasikimbie mijadala ya Bungeni mahali ambapo ni sahihi kwa kugawa pato la taifa kwa Watanzania wote. Sera ya majimbo ni usaliti kwa sehemu ambazo hazijaendelea lakini rasilimali zao zilitumika kuendeleza sehemu zilizoendelea.

Kwanini asichaguliwe kama anasifa Kwani na wanahitaji mtu wa kuwaletea maendeleo, yaani sijui kwanini watu mna kuwa negative wakati wananchi wamefanywa omba omba ati rais tunashida ya maji tunashida ya kituo cha afya wakati kodi wanalipa halafu Rais anasema siwezi kuwaletea huduma za jamii sababu mmechagua mpinzani hapo tutapataje maendeleo kwa mtindo huu.
 
mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,031
2,000
Hivi nyinyi nyumbu mnahabari ugomvi unaotokea Kenya ni sababu ya hiyo takataka yenu ya majimbo aka counties.
Msituletee balaa hapa.
Insha ndeefu na mafeelings juu, kumbe utopolo tu

Mbona unazungumzia Kenya tu hauzungumzii Zambia au afrika kusini au Ujerumani
 
ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
5,421
2,000
Ni ukweli mtupu! Karibia maswali yote ya mtoa mada ni ya kijinga na kitoto! Yamejaa hofu tu ya kuhisi kukosa ulaji hasa kwa vyeo vya kupeana, vilivyopitwa na wakati na tulivyorithi kwa Wakoloni kama vile vya Ukuu wa Wilaya na Mkoa!

Kwa Nchi iliyobarikiwa kama Tanzania, kuna eneo ambalo halina raslimali kweli kiasi cha kuwa mzigo kwa maeneo mengine? Kama lipo naomba litajwe hapa jukwaani!

Taifa kubwa duniani la Marekani linatumia mfumo wa Majimbo, na limepiga hatua kweli kweli ya kimaendeleo!

Sisi huku wanasiasa uchwara wa CCM wanatisha Wananchi mbumbumbu eti mfumo wa Majimbo utaleta mgawanyiko na kuondoa Umoja tulio nao!

Mbona Wamarekani ni Wamoja! Na hata wanapokuja huku, tunawatambua kwa Umarekani wao, na si kutokana na Majimbo watokayo?

Watanzania tukubali kubadilika. Tukiendelea kuifanya siasa kuwa kipaumbele chetu na kuwaacha wanasiasa hasa wa CCM kutuamulia kila kitu kwenye maisha yetu, basi ni wachache tu watao endelea kuifaidi keki ya Taifa huku wengi tukitaabika.

Bado ninaukumbuka sana Mchakato wa Katiba ya Wananchi namna ulivyotekwa na kuwa mali ya Wanasiasa na mwisho wa siku kupotelea kusikojulikana.
Ni wapuuzi tu hao maccm yanahofu kukosa ulaji,sheria mama za kitaifa kuushi ,kuoa nk popote ilimradi huvunji sheria ziko palepale na hakuna Jimbo litatunga sheria za kukinzana na sera mama za kitaifa .Isitoshe kwa nchi yetu ilivyo na makabila mengi hii ni njia rahisi ya kuondoa ukabila uliojengwa kwenye vimikoa na wilaya
 
Kiwarhoapandenga

JF-Expert Member
Aug 10, 2019
2,078
2,000
Nimesikia, nimetafakari sipati jibu la kuigeuza Tanzania iwe ya Majimbo, anavyonadi Lissu, mgombea Urais wa CHADEMA. Anadai, kurudisha utawala wa majimbo utawapa wananchi wa majimbo hayo mamlaka ya kuchagua viongozi wao, kupanga maendeleo yao (miundo mbinu na huduma za jamii).

Je, Utaifa uliojengwa na Baba wa Taifa ndio tuuzike rasmi?

Je, jukumu la Mihimili mitatu ya Dola (Serikali, Bunge na Mahakama) litakuwa ni lipi?

Je, nini itakuwa hatima ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Je, ni nini hatima ya maendeleo ya majimbo ambayo bado yako nyuma na yana uhaba wa rasimali maliasili na miundo mbinu isiyo bora?

Je, ni kwa vipi pato la Taifa litagawanywa?

Maswali ni mengi yakihitaji majibu. Kwako Lissu na CHADEMA
Jimbo la Calfonia,oklohama,sijui Chicago bado hujaelewa nini

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,557
2,000
Nchi haizalishi kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala ambao umejikita kwenye itikadi za kijamaa.Mfumo wa majimbo ni Kama mfumo wa ubepari yaani unareward wale wenye ufanisi.Nchi zote duniani zinatumia hii system sio tunagandamizana kisa fulani hapendi.
Dhana ileile ya kwamba utajiri wa eneo moja km kilimo cha korosho, kunufaisha Dsm ni tatizo, vivyo hivyo litaibuka pale utajiri wa eneo moja la jimbo utakapotumika kunufaisha eneo lingine, kata kwa kata, kijiji kwa kijiji, kitongoji kwa kitongoji, hadi kaya kwa kaya.

Nawaza kwa sauti, NIA NI NINI HASA YA UTAWALA WA MAJIMBO? Au nia ni kuyapa majimbo mamlaka ya hata kuuza sehemu ya ardhi yao kwa wageni? Au nia hasa ni kuyapa majimbo mamlaka ya hatimaye kutaka kujitenga pale yatakapokuwa na nguvu kiuchumi?
 
ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
5,421
2,000
Hivi Singida kama Singida Ina rasilimali gani yakuleta maendeleo jimboni kwa mfano?
Kama haina rasilimali,nambie unakuaje Singida ni mji mkubwa kushinda Moshi,Shinyanga,Sumbawanga,Kigoma,Lindi nk? Usiwe kiazi mkuu hujui hii nchi,kwa mfano pori la akiba la Rungwa liko sehemu kubwa Singida/Manyoni na Lina vitalu vingi vya uwindaji,ardhi ya kilimo ikiwemo alizeti,asali nk nk.
Na uwepo wa majimbo utafanya kila watu waangalie kile kinachoweza kufanywa kwa ufanisi kwa eneo lao na kikaleta tija na hii ndio sifa ya majimbo maana kusaidiwa inakuwa ni fedheha
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom