Tanzania ya leo si ya jana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ya leo si ya jana!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mutekanga, Aug 26, 2009.

 1. M

  Mutekanga Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yale yaliyotokea Dodoma, ya CCM kumgombeza Sitta, ni ya Tanzania ya jana. Kuna wanaojifanya vipofu na kutufanya tufikiri bado tunaishi Tanzania ya jana. Ukweli ni kwamba Tanzania ya leo si ya jana! Leo hii tuna mfumo wa vyama vingi, leo hii Bunge letu ni la vyama vingi- haiwezekani tena NEC ya CCM, inatoa maelekezo kama ilivyokuwa ikifanya wakati wa chama kimoja.

  Wajinga, amboa wanafikiri Tanzania, itaendeshwa tena kwa mtindo wa chama kimoja, wamepotea njia. Wabunge wetu wengi wasubiri uambiwa hapana kwenye majimbo yao. Watashangaa sana pamoja na fedha zao hawatachaguliwa.

  Kwamba mkakati ni wa kutaka kumsafisha Lowassa. Ili atakate awe nani? Rais wa Tanzania? Hayo yalikuwa ya Tanzania ya jana. Leo watu wanahoji na kusema kweli watamzomea sana akijaribu kutaka kusafishwa au kujisafisha. Kuna watanzania wengi wa ku weza kuiongoza nchi yetu, si lazima awe Lowassa au watoto wa viongozi walio madarakani leo hii.

  Watanzania wapole, lakini amini usiamini wale wa jana si wa leo! Mambo yamebadilika. Ni njinga peke yake, anaweza asione ukweli huu. Kwamba Spika, anyamazishe uovu? Hizo ni ndoto! Tuwe macho kabisa , tanzania ya leo si ile ya jana!
   
 2. k

  kasogwe Member

  #2
  Aug 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo ccm wamechemsha
   
Loading...