Tanzania ya leo na makengeza ya elimu ya viongozi

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,544
934
Imekuwa ni desturi yangu kulaani na kukemea taaluma ambazo viongozi wetu wameipata kwa kusomeshwa na kodi za wananchi wa nchi hii,lakini zikakosa mashiko na kuleta tija kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa na watu wake.Ukijaribu kuangalia katiba ya TANU kuna kipengele kinasema,nitatumia elimu yangu kwa faida yangu na kwa faida ya watu wote.Lakini leo hii elimu hiyo imekuwa kaburi la fikra endelevu katika kuikomboa nchi yetu.

Najua kuna watu watauliza hivi nchi hii haijakombolewa?Ni kweli nchi hii ina ombwe la viongozi wenye uwezo mkubwa wa kuidhalilisha elimu yetu kwa kiwango cha juu kwa makusudi ambayo leo hii ndiyo yanayo liangamiza taifa letu.Mifano ipo mingi,sipendi kuamini wakati tunaandika mikataba ya migodi ya madini na umiliki mbalimbali wa ardhi viongozi hawakuwa na taaluma ya kutosha.Tumeona sakata la Richmond na tuzo ya Dowans jinsi serikali kwa kutumia makengeza ya elimu ya viongozi wa umma ikiendelea kuitesa serikali ilhali kuna wasomi lukuki ambao hatuoni umuhimu wa elimu yao ambayo waliapa kuitumia kwa faida ya taifa zima.

Huwezi kujua ipi elimu ndogo na ipi elimu kubwa ambayo inalete tija kwa maendeleo ya taifa hili.Wasomi waliobobea wamekuwa ndiyo wachimba kaburi na wazikaji wa mama Tanzania.Haitaji elimu ya chuo kikuu kutambua hata aina ya muungano tulionao kati ya Tanganyika na Zanzibar, nao unasabaishwa na ombwe na makengeza ya elimu waliyoipata viongozi wetu.

Tangu lini kwa akili ya haraka haraka vitu viwili vikiungana badala ya kuwa kitu kimoja au kuwa vitu vitatu ili vipate haki sawa vinageuzwa na kuwa viwili na kumkandamiza mmoja.Tumeona muungano wetu una mashaka makubwa lakini kwa kujaliwa akili zaidi ya viumbe wengine binadamu huyu wa Tanzania haoni mapungufu na kutetea ujinga bila hata kutaka kujali wengi wana semaje.

Makengeza haya ya elimu na kutokujitambua kwa watawala ndiyo leo hii wananchi wanataabika hawajui siku yao ya leo itaishia vipi, lakini viongozi wao wana kuja na kauli ambazo hazina suluhisho la matatizo ya wananchi hawa.Hivi kadi ya CCM aliyonayo Dr. Slaa ina saidiaje kutatua matatizo ya mtu wa Kashozi ama matatizo ya mtu wa Giliku huko Bariadi mkoani Simiyu.

Hivi ni kweli kulikuwa na haraka gani ya kugawanya mikoa na wilaya kwa kuiongezea serikali mzigo wa matumizi ilihali serikali ipo taabani kiasi cha kutegemea bajeti ya wahisani kwa zaidi ya asilimia 40.Umakengeza huu tusipokuwa makini kwa kuukata kwa nguvu zetu zote ipo siku nchi yetu kwa kuongozwa na viongozi wenye ombwe la elimu na kutokujitambua watatuingiza kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya tuliyo nayo leo hii.

Watanzania sasa tujitambue,tuweke mambo yetu kwenye mstari kwa kuwakataa wale wote ambao wameshindwa kutumia elimu yao kwa faida ya taifa letu.Mungu ibariki Tanzania Mungu zibariki harakati zetu za kujikomboa katika kujiletea maendeleo yetu.

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom