Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Declaration of interest
*********
Interest 1. Mimi ni moja ya watu wanaoamini kuwa, pamoja na changamoto zake, bado mfumo wa demokrasia ndio mfumo bora zaidi wa kiutawala unaopaswa kufuatwa na mataifa yote duniani kwa sababu ya ubora wake ukilinganisha na mfumo mingine. Kwa mantiki hiyo, natamani tuwe na nchi yenye demokrasia makini na imara.
*******"
2. Naamini chini ya uongozi wa Rais huyu wa awamu ya sita, demokrasia itaimarika 'relatively' na hapo kabla licha ya presha ya makundi maslahi. Hii ni kwa sababu mama ni mtu muungwana na mwenye hekma.
*********
Hoja yangu sasa, pamoja na uzuri wa demokrasia, kuna hatari mbaya sana kutokana na jamii yetu ilivyo ambayo kwa bahati mbaya huwa haijadiliwi sijui ni kwa nini.
Ikumbukwe kanuni mama ya demokrasia ni 'kuendeana na upepo wa wengi huku wachache wakivumiliwa na kulindwa'.
Kwa mantiki hiyo, katika demokrasia iliyokomaa;maamuzi ya wengi ndio hutakiwa kutekelezwa bila kujali ni mazuri au mabaya. Aidha, ili uchaguliwe kuongoza umma kwa mfano, unatakiwa kuendeana na mapigo ya wengi hata kama hao wengi wanataka ufanye jambo la kijinga.
Sasa basi, kwa bahati mbaya kwenye jamii yetu iko hivi:-
Tuna watu wengi wanaopenda kushangilia ujinga kuliko mambo ya maana. Kwa mantiki hiyo, kama kuna demokrasia kamili kuna hatari kubwa mbili.
Kwanza, wanaotaka kuchaguliwa watajikuta wakiwajibika kufanya mambo ambayo hayaingii akilini na pengine ya kijinga kabisa ili kuliridhisha kundi hili kubwa tu ili wachaguliwe na
pili, tunaweza kufika hatua tukakuta nchi inasimamia mawazo ya ajabu sana simply kwa sababu ndio mawazo ya wengi.
Aidha, tuna watu wengi sana ambao hupenda kusikia story mbaya kutoka kwa wenzao kuliko story za mafanikio. Watu hawa hupata raha sana kuona waliko juu wanashushwa chini kuliko wanavyofurahi wao wenyewe wakinyanyuliwa juu.
Kwa mantiki hiyo, katika mazingira ya fully democracy kwenye jamii ya namna hii, kiongozi anaweza kujikuta akilazimika kuwashusha waliofanikiwa ambao ni wachache ili kuwaridhisha wengi waliokwama badala ya kinyume chake. Wakati flani kiongozi mwenyewe anaweza kuwa hapendi, lakini ndio demokrasia inataka.
Nitaomba nitoe mifano kadhaa zaidi ili kuweka vizuri mada hii.
Tanzania tuna watu ambao hawakubali kabisa hoja za ukweli bali wanakubali sana propaganda, na ndio maana tumekuwa watu wa cheap propaganda ili kuridhisha kundi hili ambalo ni kubwa kweli.
Tuna watu wanapenda 'ubuyu' kuliko hoja za maana. Ndio maana hata kwenye social media mijadala ya maana haina wafuatiliaji wala wachagiaji.
Kwa hiyo katika democrasia kamili ambayo ni upepo wa wengi, ukitaka kushika wengi unatakiwa uwe unaongea umbea ujingaujinga na uzandiki. Just think about it!
Tanzania tuna watu ambao wako tayari kumsapoti darasa la saba kwa kuwa anachekesha na kumkataa profesa ambaye amefanya reserch kwenye jambo 'profesional' pengine kwenye mjadala juu ya namna ya kudhibiti mtungi wa neuclear usivuje.
Ikumbukwe hata kwenye tume ya kuwauliza watanzania kama wanataka vyama vingi au la? Wengi walisema hawataki. Kwa hiyo Nyerere asingetumia logic binafsi kuforce viwepo, ungekuta hakuna vyama vingi hadi leo na ni maamuzi ya kidemokrasia.
Mifano ni mingi, haiwezi kuisha.
Sasa Swali ni je! Wakati tunaitetea Tanzania ya kidemokrasia kwa upande mmoja, Tunashugulikia je Janga hili la kijamii kwa upande wa pili?
Kwa upande wangu, nadhani tunatakiwa kupigania kutoa elimu kwa jamii na kuishawishi ibadilike kuliko hata nguvu tunayotumia kuipigania demokrasia yenyewe. Hata hiyo hii haimaanishi kwamba hatuhitaji Tanzania ya kidemokrasia, tunaihitaji sana.